Mbunge aliyeshinda kimizengwe Kibaha (m) apora ukumbi wa Kiwanda cha Urafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge aliyeshinda kimizengwe Kibaha (m) apora ukumbi wa Kiwanda cha Urafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MKL, Jul 14, 2012.

 1. MKL

  MKL Senior Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Koka Francis Silivestry Mbunge wa Kibaha Mjini amekodishishiwa ukumbi wa kiwanda cha Urafiki Maarufu kama Ukumbi wa Social Hall ambao historia yake ni Kuwa ukumbi huu ni mali ya Kiwanda cha Nguo cha Urafiki ambacho ni Mali ya Serikali ya Tanzania na China.Sina Uhakika wa kiasilimia kuwa kati ya Nchi hizi mbili ni ipi inamiliki asimia nyingi kuliko ingine, ila ilimradi mradi huu wa kiwanda ulikuwa ni nchi mbili basi na ukumbi huu wa Kiwanda nao ni mali ya kiwanda ulitegemewa kuwanufaisha wafanyakazi wa kiwanda hiki ambacho historia yake ni ndefu sana kwa nchi mbili hizi.

  Matumizi ya ukumbi yamebadilika.

  Sisi wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki sasa hatuna mahali pa kukutanikia na kubadilishana mawazo achilia mbali kuburudika na vinywaji kutokana na ukumbi huu kukodishiwa Mbunge wa Kibaha Mh. Koka na kuubadilisha kabisa kutoka kwenye kuwa ukumbi wa pamoja kwa wafanyakazi na badala yake kuwa ni ukumbi wa Biashara za usiku kwa matajiri kwa lengo la kututenga sisi walengwa hasa wa ukumbi huu. Kwani ili ukapate kinywaji ukumbini hapo unapaswa kulipia kiingilio cha shilingi elfu tano (5,000) kwa kile kinachoitwa kuwa ni kufidia/kurudisha gharama za uwekezaji "mkubwa" alioufanya Mh. Koka.


  Pili amezingira eneo la wazi ambao tulikuwa tunakutanika kupata upepo na kupata vinywaji vya bei nafuu ambalo lina Kibanda cha Afande Said Abdalah na kulifanya kuwa maegesho ya Magari kwa ajili ya matajiri wanaokuja kunywa na kuburudika Ukumbini hapo. Sisi wafanyakazi wa kiwanda tuende wapi kwa ajili ya vinywaji na hata chakula wakati ukumbi uliotulenga sisi umeshanyakuliwa na Bepari? Ikumbukwe kuwa bei ya Bia sasa Mh. Koka anauza Sh. 2500 wakati jirani yake Saidi bia ni Sh. 1700/= tuu Koka anafanya hivi kwa ushirikiano na Meneja wa Kiwanda maarufu kama Swai ambaye ameuza hata eneo la kiwanda linalopakana na Kanisa katoliki Manzese kwa waegesha magari ambao wameweka Kifusi kuziba mto na sasa hakuna mtiririko wa maji kuelekea Baharini kabisa
  Tunahoji mambo haya na uhalali wake. Tulipohoji kwa Swai na hata Saidi ambae anatufaa sana kwa kutuuzia vinywaji kwa bei nafuu Saidi alituonyesha Barua aliyoandakiwa na meneja wa kiwanda kuwa wanampa Koka eneo hilo la wazi ili kumsaidia Koka apate kupanua Biashara yake kutokana na "UWEKEZAJI MKUBWA ALOUFANYA" wa kukarabati na kuudurufu ukumbi wetu wa urafiki na hivyo kuubadili kimaana na matumizi kabisa kuwa ni eneo la Mabepari kujidai usiku kucha huku wafanyakazi wa urafiki tukibung'aa macho kwani si lengo la Koka sisi kuutumia ukumbi huo tena.

  Sasa tunajiuliza na hata tunawaomba Waheshimiwa Wabunge mtusaidie kuiuliza serikali kupitia wizara ya Viwanda na maswali haya kama si Koka Mwenyewe:

  • Sheria ya Uwekezaji hatujui ni ya mwaka gani lakini Mnaojua sheria jazieni hapo inaruhusu uwekezaji ndani ya uwekezaji? Yaani kiwanda ni mali ya serikali ya Tanzania na China japo hatujui ni kwa asilimia Ngapi ngapi, Kiwanda kupitia meneja wake Swai na Wachina wamemkaribisha Mwekezaji Mwingine wa Vileo (KOKA) Je sheria ya uwekezaji inaruhusu hilo?· Kama serikali Inaruhusu mwekezaji ndani ya Uwekezaji wa Nchi Mbili yaani Tanzania na China sasa sisi wafanyakazi wa Urafiki tunauliza hivi, Koka ni Nchi nyingine ya Tatu? ili tujue kuwa sasa mali hii ya nchi mbili imebadili umilikishwaji na sasa imeongezeka nchi yatatu inaitwa Mh. Hon.Koka Francis Silvestry ?· Kama Koka si Nchi ila ni mwekezaji wa ndani basi tunataka kujua serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara imemmilikishaje Kuwekeza ndani ya uwekezaji ambao tayari unawamiliki (Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na China)?· Je kwa uwekezaji wa Koka ambae anajigamba kuwa amewekeza zaidi ya Bilion Moja kukarabati ukumbi, Kudurufu na mengineyo "Mwekezaji ndani ya uwekezaji" wa nchi mbili amesajili uwekezaji huo serikalini?· Kama amesajili, serikali ituambie analipa Shilingi ngapi kama Kodi serikalini kutokanana na kuvuna hela nyingi za viingilio vya kuingia ukumbini hapo achilia mbali bia ambazo anauza kwa bei ya hoteli za kitalii (Five Star hotel)?
  • Tunahoji kama uwekezaji wa namna hii unaruhusiwa na serikali kupitia wizara husika, Kwanini Koka asisajili Ukumbi huu kwenye soko la hisa (DSE) ili nasi wafanyakazi ambao ndio walengwa wakuu na ukumbi huu tununue Hisa ili tuwe tunapata gawio kwani kimsingi sisi tunaoishi karibu na ukumbi huu ndio walinzi wakuu wa uwekezaji huu na kimaantiki sisi ni wahusika zaidi yake yeye KOKA?· Je ukumbi huu ulijengwa ili kuwa ukumbi wa starehe za usiku? Maana kwa sasa ni Night Club, wafanyakazi wa Kiwanda hatuna haki kabisa kuusogelea kwa jinsi ulivyobadilishwa na kuwa ni kitengo cha anasa kwa wenye hela wanaoendesha magari makubwa makubwa. (hatuna kipato kulipia huduma za humo ndani)
  • Tunamwomba Koka aache kutunyanyasa sisi wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki, kwani huu anaouita uwekezaji mkubwa kwa mgongo wa Meneja wa Urafiki na wachina sisi ndio walinzi wake wakuu na tusipopewa majibu ya kuridhisha tutauhujumu kwa namna yeyote ili urudi kwetu badala ya kuona magari makubwa yanapaki usiku kucha hapa wenye hela wakicheza disko na kutuharibia mabinti zetu kwa zinaa na matumizi ya madawa ya kulevya. Kuingia hapa mfanyakazi mwenye kipato cha chini kama sisi wafanya kazi wa urafiki sasa ni Historia (kiingilio 5000)Kupata kinywaji hapa kwenye Kuti na hata Ndani ni sh. 1500 kwa Soda na 2500 Bila usiguse zile Spirit.

  Mnyika John John Kumbuka Historia ya Ubunge wako na Ukumbi huu Tutakushangaa kama hutatutetea kwa hili

  Kwa historia fupi tuu ya Kisiasa ni kwamba huu ndio Ukumbi ulioweka Historia kwanza kwa kumtabiria J. J Mnyika Ushindi Baada ya kumgaragaza Hawa Ngúmbi kwenye Kipindi cha Uchaguzi Majimboni Kilichokuwa kinarushwa na TBC1 mtangazaji akiwa Shaabani Kissu. Baada ya Ng'umbi Kupanick kutokana na Maswali magumu toka kwa wapiga Kura wa Ubungo KATIBU Mkuu wa CCM wakati huo Yusuph Makamba aliamua kupiga Marufuku wagombea woote wa CCM kushiriki kwenye Kipindi Hicho, Tunaweza kusema ni ukumbi huu huu ndio ulioifanya serikali ya CCM kuona kuwa TBC ilikuwa inawadhalilisha na hivyo kumfukuza kazi aliyekuwa Boss wa chombo hicho Tido Muhando baada tuu ya uchaguzi.

  Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki
  Ubungo- Dar es Salam

  Nakala:

  ·
  Mbunge wetu J.J Mnyika
  ·
  JamiiForum
  ·
  Mnashimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni
  ·
  Koka Francis Silyvestry
  ·
  Mbao zote za Matangazo Kibaha mjini Vilabuni, Sokoni, Madukani kwenye mikusanyiko, Nguzo za Umeme, na popote linapoweza kubandikwa Tangazo hili la Madhila haya ya KOKA
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo athari (hasi/chanya) za uwekezaji. Hivi TAZARA Club bado ipo na je ipo chini ya nani?
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kutothaminiana!! Mtu anayetumia mbinu yeyote kuingia madarakani muogope, kwani yuko radhi kufanya lolote ilimradi apate pesa.
   
 4. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wacha arudishe gharama za uchaguzi. Kazi iliyobaki ni kuutangazia umma huu ubaradhuli wa Koka, amabako siku hizi kuanaitwa "kumshitaki kwa wananchi".
   
 5. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hicho Kiwanda cha Urafiki hakina viongozi? Inamaana wafanyakazi wa kiwanda hawana uthamani kama huo uwekezaji hapo?
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hakuna cha ajabu hapo.....
  Anachofanya huyo mnunge ni sahihi kabisa.... Mambo ya

  Chukua Chako Mapema hayo...
   
 7. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Afande Said Abdallah,

  Mie najua ukweli wa huo ukumbi naomba nikujibu.

  Bwana Koka kama Koka Haja GRAB ukumbi wa urafiki. Kabla ya ukarabati huo ukumbi ulikua UMATELEKEZWA kwa miaka kibao. Pakawa ni chaka la wezi na wezi na wauza unga.
  NDIVYO ULIVYOTAKA LIENDELEE? Nyie kama wafanyakazi mlikua wapi kutolichukua na kuliendeleza kwa miaka karibia KUMI?

  Kampuni iliyoichukua Urafiki kuiendeleza imeajiri watu karibu 50 wengine ikiwa ni ndugu zako na wengineo.

  Ukumbi wa urafiki una kumbi tatu, moja ni Bar na Restaurant kwa ajili yenu na wengineo ambao bei ya bia ni sawa na hapo kwako bwana Abdallah. Bei ya soda na Maji ni kama hapo kwako. Mbona hutaki kusema kuhusu huu ukumbi wa makuti na badala yake umekazania kiingilio elfu tano?

  Ukumbi wa pili na wa tatu ni za Harusi.

  Ukumbi mdogo kama ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala ni Ako La Bamba Pub and Grill. Huu ukumbi ni wa kisasa na una Karaoke na nyama choma ya kufa mtu. Mie ni mwendaji sana pale ndo maana nikauliza nikaelezewa na nakujibu.
  Huu ukumbi HAUNA KIINGILIO. Ilipoanza ilikua unatoa elfu Tano unapewa Coupons unaenda kuzitumia ndani. Ni kweli bei ya bia humu ndani kwenye AC ni 2500. Je bei ya bia kwenye 5 stars Hotel wana JF ni Tshs 2500????!!!!!!!!!!!!!!! kwa sasa hamna tena kulipia. Ndani kuna DSTV, unatazama soka huku unakula bia bariiiidiii!
  Je kwa wewe ambaye ni wa kima cha chini cha mshahara kama unavyodai huoni kua hii ni nafuu kwako?, tena hata ukumbi wa makuti wa bia bei rahisi pia una DSTV. Ukumbu huu ni wa kisasa na ni bora kuliko kumbi zote Sinza, Manzese, Ubungo nk.

  Je huyo uliemtaja bwana Koka UBUNGE wake unahusiana vipi na Uwekezaji wake? Umejuaje alipora ushindi Kibaha? mbona kesi alishinda mahakamani?

  Kiwanda cha Sigara TCC kimekodisha kwa mtu binafsi ukumbi wa Chang'ombe ili kiendelee na uzalishaji wa Sigara.

  Kampuni ya BP(Puma) wamekodisha bar yao pia

  Bandari wamekodisha kwa mtu binafsi pia bandari CLUB

  TPDC pia imetoa kwa Brajec club yao.

  Makampuni yanataka ya concetrate kwenye what they do best. Sio kuendesha ma club.

  Kwahiyo ungependa pale urafiki pafungwe pawe chaka au pori ili uendelee kuuza bia zako na wahudumu wawili kuliko kukodishiwa watu ili iajiri watu 60?, hiyo ndo sera unayotaka wewe?. Kama ndo hivyo basi hii nchi haitaendelea milele.


  Mbona wewe umekodishiwa hilo eneo lako?, kwanini husemi hilo? na mkataba umeisha, hutaki kuondoka je ni halali hiyo?
  Watu wakiwa na magari ya kifahari unachukia? unataka watu wote wawe masikini?

  Kweli JF imevamiwa. Afande, mambo binafsi malizia kibinafsi la sivyo werevu watakuona kituko.
  Angalia nimejiunga lini JF usije ukafikiri mie ndo KOKA

  Wasalaam and Ramadan kareem!
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Leo jioni nitakuwepo Ako La Bamba Pub and Grill (shekilango zamani urafiki social hall), pita nikununulie bia na nyama choma. Kisha nitakupa lift kwenye gari langu la kifahari BMW X6!!

  Ila usije chukua kiwembe uchane seats za gari bureee.
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Na wewe Afande Abdallah mbona umewekeza na ulikua unalipa kodi kila mwezi kwa wachina?, koka aanalipa kodi ya mwezi kama wewe, tofauti yenu yeye amekodisha pakubwa. Je na wewe naomba tujiulize swali ulilouliza hapo juu.

  Ukinyoosha kidole kimoja vinne.........?
   
Loading...