Mbunge alia na wamiliki wa viwanda vya samaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge alia na wamiliki wa viwanda vya samaki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nngu007, May 15, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145  Na Mwandishi Wetu, Mwanza
  MBUNGE wa Ilemela Jijini Mwanza, Highness Kiwia (CHADEMA),amewaonya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya samaki jijini hapa, kwa vitendo vyao vya kubana mizani na kuwapunja wavuvi wadogo mali zao halali.
  Alisema, kitendo cha wafanyabiashara hao ‘kuwaibia’ wavuvi wadogo mali zao, inapaswa kukomeshwa haraka sana, kwani ni kinyume cha sheria za nchi.
  Kutokana na hali hiyo, mbunge huyo ametoa muda wa siku saba kuhakikisha hali hiyo,inakomeshwa la sivyo hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
  Kiwia, aliyasema hayo juzi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
  kwenye mialo ya uvuvi iliyopo Igombe na Kayenze jimboni Ilemela.
  “Tumeona sote wizi huu, kwenye kilo 100 mvuvi mdogo anapunjwa kuanzia kilo 20. Hii ni hatari sana kwa maendeleo na mimi nitalifuatilia hili hadi kieleweke”, alisema Kiwia.
  Kwa mujibu wa Kiwia, Sheria ya vipimo namba 20 ya mwaka 1982, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, inakataza wafanyabiashara kutumia mizani isiyo sahihi wala vipimo visivyoruhusiwa kisheria, hivyo adhabu yake ni faini, kifungo cha mwaka mmoja hadi miaka mitano.
  Kwa upande wao, wafanyabiashara wa samaki katika mialo hiyo ya Igombena Kayenze, walimweleza mbunge huyo, kwamba wanabana mizani yao kwa sababu nao wanapopeleka samaki viwandani hukuta mizani imebanwa, hivyo hupoteza kilo nyingi.
   
 2. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Baadhi ya mafanikio ya ccm baada ya miaka 50 nikumfanya kila mtanzania awe mwizi au afikirie kuiba.
   
Loading...