Mbunge akombwa kila kitu gesti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge akombwa kila kitu gesti

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, amevamiwa na wezi katika nyumba ya kulala wageni na kuibiwa fedha taslimu pamoja na kila kitu alichokuwa nacho chumbani kwake.
  Tukio hilo lilitokea juzi katika nyumba ya kulala wageni ya Sangos Lodge, iliyoko mjini hapa, saa 8.00 usiku wakati Mchungaji Msigwa akiwa amelala.
  Mchungaji Msigwa ni miongoni mwa wabunge walioko katika ziara ya operesheni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
  Tayari Mchungaji Msigwa ameripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha mjini hapa, ambako jalada namba SUM/RB/3087/2011 limefunguliwa.
  Akizungumza na NIPASHE jana, Mchungaji Msigwa, alisema wakati akiwa amelala, wezi hao walivamia nyumba hiyo na kisha wakafungua dirisha la chumba alichokuwa amepanga. Alisema baada ya kufungua dirisha hilo, waliiba pochi iliyokuwa na vitu hivyo pamoja na fedha taslimu Sh. 400,000.
  Alivitaja vitu vingine vilivyoibwa kuwa ni kitambulisho cha ubunge na simu mbili za mkononi ikiwemo moja inayofanyakazi kama kompyuta, vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 1.2.
  “Kati ya simu hizo, moja ni ‘Iphone’ (simu ya kompyuta). Hiyo, niliinunua kwa Dola za Marekani 900. Ilikuwa na picha zangu nyingi,” alisema Mchungaji Msigwa.
  Vitu vingine vilivyoibwa, alisema ni leseni ya udereva, kadi za benki na waraka wa huduma ya lipa umeme kadri unavyotumia (Luku).
  Mchungaji Msigwa alisema alifika wilayani Sumbwanga siku hiyo saa 6:00 usiku na kukuta vyumba katika nyumba karibu zote za kulala wageni za mjini humo vikiwa vimejaa wageni.
  Alisema kutokana na hali hiyo, muda huo alilazimika kwenda nje ya mji kutafuta vyumba katika nyumba nyingine za kulala wageni na kufanikiwa kupanga katika nyumba hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  pole sana mchungaji, police jjitahidini kufanya uchunguz na muwafikishe mahakan watuhumiwa wote ili nao wapate haki yao..
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,608
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  Pole mchungaji
  ila nafurahi vyote vinalipika kwa mshahara wenu mmoja.....,
   
 4. koo

  koo JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole sana mchungai mungu asaidie hao wezi waliotumwa na magamba kudhohofisha maandamano wakamatwe
   
 5. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  pole kamanda bt yote kwa yote vita inaendelea
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kumbe Iphone' (simu ya kompyuta). ??
   
 7. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  hao sio wezi ni usalama wa ccm wanataka kufuatilia mawasiliano ya wakombozi wetu
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Pole sana Mchungaji Msigwa, mapambano yaendelee kama kawaida, inawezekana CCM wametuma vibaka wao ili waichukue hiyo iphone ili kupata taarifa za chama. Isije kuwa CCM walifanya uhuni ambao haukugundulika mara moja kuhakikisha unapata chumba cha kulala nje ya mji mahali ambapo security wise yake si nzuri in general
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pole sana kamanda wetu, songa mbele!!!
   
 10. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Pole sana mchungaji ila pokea hiyo kama changamoto sisi hayo yanatupata kila siku kwa vile hayafiki kwenye vyombo vya habari. Natumai kwamba utawatetea pamoja na hao vibaka wanakesha kusaka kwa njia za haramu kwa kukosa mambo muhimu ya kufanya mchana kwani ukali wa maisha unasikika zaidi kwa maskini.
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Vijana wanaiba, wanakaba, wafanye nini sasa wakati maisha yamekuwa tight! Hakuna pakupumulia.
   
 12. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Pole sana Mpiganaji wetu Mchungaji !

  Hii yote ni shauri ya CCM kulea wezi na majambazi. Badala ya watoto wetu kwenda shuleni, wako mitaani kwa kukosa ada, madawati na waalimu. Na hata wale waliomaliza elimu, wako mitaani hawana kazi !Haya sasa, bila kuiondoa CCM madarakani, Tanzania itaendelea kuwa nchi ya majanga tu ! Endelezeni mapambano huko Songea mpaka kieleweke !
   
 13. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole mchungaji.

  Endelea na kupambana,hilo lililokutokea ni mojawapo ya maozo ya serikali kulea wezi na magenge ya majambazi; system ni kubwa mno.
   
 14. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Mchungaji gani huyo kaachwa na Mlupo wa pale pale katika hiyo hotel na isitoshe Mlupo wenyewe ushasepa zake Tunduma kitambo baada ya tukio tupunguze zinaa ehhh! Hata watumishi wa mungu! Hatariii
   
 15. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Wajanja ndio wameshachukua chao,pole sana
   
 16. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole sana mchungaji, upelelezi uanze na wahudum wa hiyo lodge!
   
 17. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Red: Unawaza mbali sana na ninapenda sana watu wa namna yako. I wish wapiganaji tuwe na intelijensia iliyokwenda shule na inafuatilia mienendo yote michafu ya kuzolotesha harakati hizi za ukombozi. Naunga hoja kiongozi
   
 18. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  duh, kila baya linalotokea bongo ni ccm..tumekosa vya kusingizia mazee? japo siipend ccm lakn siyo kihivyo duh!
   
 19. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  hufahamu maana ya kompyuta mkurugenzi kweli?
   
 20. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Isije ikawa kamanda alikuwa amejizolea changu.Maana ma-Rev. nao noma.Hata hivyo pole kamanda, aluta continua.
   
Loading...