Mbunge adaiwa kupora mke

Mbunge adaiwa kupora mke

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,944
Reaction score
4,511
Mbunge wa Ziwani, kisiwani Pemba, Ahmed Juma Ngwali (CUF), amefunguliwa jalada katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akituhumiwa kuvunja ndoa ya mfanyabiashara wa mjini Unguja na kutorosha watoto wawili nchini kwenda Canada, kinyume cha sheria.
juma.jpg

Mbunge wa Ziwani, kisiwani Pemba, Ahmed Juma Ngwali

Ngwali anatuhumiwa na mfanyabiashara huyo, Khalfan Said Chondoma, mkazi wa Saateni, kisiwani Unguja, kuingilia ndoa yake na kusababisha kuvunjika na hivyo kupata mwanya wa ‘kumpora’ mkewe.

Pia anatuhumiwa kutorosha watoto wa mfanyabiashara huyo msichana (8) na mvulana (9) na kuwapeleka Canada baada ya kuwabadili ubini halali wa baba yao mzazi na kuwapachika ubini wa mbunge huyo.

Khalfan aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa aliripoti suala hilo katika kituo cha polisi Oysterbay na kufungua jalada namba OB/RB/21545/2012.

Khalfan (31), analalamikia kutoroshwa kwa watoto wake chini ya himaya ya wazazi na kuwa kabla ya matukio hayo, Ngwali alikuwa rafiki yake aliyekuwa akimtembelea nyumbani, lakini hakujua kuwa alikuwa ana lake moyoni dhidi ya mkewe.

Alidai kuwa alikuja kubaini hilo baada ya kuanza kuona uhusiano mzuri uliokuwa kati yake na mkewe awali ukibadilika ghafla.

Khalfan alidai uhusiano kati yake na mkewe uliendelea kuwa mbaya hadi ulipotokea mtafaruku mkubwa kati yao.

Alidai kufuatia mtafaruku huo, mkewe aliondoka nyumbani bila kupewa talaka na kwenda nyumbani kwa wazazi wake mkoani Tanga.

Khalfan alidai wazazi wake waliingilia kati mgogoro huo, lakini yeye akashikilia msimamo wake kwamba, ili ampokee na kuendelea kuishi naye sharti akubali kutofanya kazi kwa kuwa hana uwezo huo kutokana na elimu yake kuwa ya darasa la tano.

Alidai mkewe aliendelea kupinga sharti hilo na hivyo kukataa kurejea kwake.

Kwa mujibu wa Khalfan, wiki chache baadaye alisikia kuwa mkewe ameolewa na mbunge huyo bila kumpa talaka.

Alidai kuwa watoto wake walitoroshwa kwenda Canada, Oktoba 30, mwaka jana, baada ya mbunge huyo kuwapachika ubini wake.

“Aliwabadilisha ubini wao halali na kuwaita (anataja majina yao),” alidai Khalfan. Alidai hadi sasa watoto wake bado wanaishi Canada, ambako wao na mama yao wamejitambulisha kama wakimbizi. “Sijui wamejilipua kama wakimbizi wa nchi gani, maana Tanzania hatuna wakimbizi,” alidai Khalfan.

Hata hivyo, alidai kuwa taarifa alizonazo ni kuwa watoto wake walitakiwa kurudi nchini Novemba 7, mwaka jana, lakini haijulikani kwanini hadi sasa hawajarudi.

Alidai kufuatia kitendo hicho, aliwasiliana na Mtandao wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini, ambao aliwakabidhi vielelezo vyote vinavyohusiana na shauri hilo. Khalfan alidai Interpol walikwenda Zanzibar, pamoja na mambo mengine, walichukua vivuli vya pasi za kusafiria zilizoandikwa ubini bandia wa watoto hao.

Alidai baada ya kuchukua vielelezo hivyo, Interpol walimhakikishia kuwa wanaendelea kufuatilia suala hilo.

Khalfan alidai anachokitaka ni kujua Ngwali ana haki gani kisheria kukaa na watoto wake, pia serikali ifahamu kile alichokiita “udhalimu” aliodai kufanywa na mbunge huyo na vilevile anataka apewe watoto wake.

Khalfan alionyesha vielelezo mbalimbali, kikiwamo cheti cha ndoa kuthibitisha kuwa alifunga ndoa na Aisha Machi 11, 2004; pia vyeti vya watoto hao vya kuzaliwa kuthibitisha kuwa ni watoto aliowazaa na mwanamke huyo.

KAULI YA MBUNGE NGWALI
NIPASHE jana iliwasiliana na Ngwali kwa njia ya simu, ambaye alithibitisha watoto hao pamoja na mama yao mzazi, Aisha kuwapo Canada.

Ngwali alisema Aisha ni mkewe halali wa ndoa, lakini watoto hao ni wa Khalfan.
Alidai hakumbuki tarehe na mwezi aliofunga ndoa na Aisha, lakini anachokumbuka ndoa yao ilifungwa miaka miwili iliyopita baada ya mwanamke huyo kumkataa Khalfan kutokana na kumzuia kufanya kazi ya duka.

Ngwali alidai ndoa kati yake na Aisha ilifungwa wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, kwa idhini ya wazazi wa mwanamke huyo.

Ngwali alidai cheti cha ndoa kinachothibitisha kuwa alifunga ndoa na Aisha kipo, lakini kwa kuwa yeye husafiri mara kwa mara, hawezi kutembea nacho mkononi.
Alidai hakuwahi kuishi na watoto hao, bali walikuwa wakiishi na bibi yao mzaa mama Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

Hata hivyo, alidai kuwa hakuishi muda mrefu na Aisha, kwani mwaka jana mwanamke huyo alifanya hadaa na kuondoka kwenye himaya yake na kwenda kuishi na watoto hao Canada, kinyume cha taratibu.

Alidai kuwa kufuatia kitendo hicho, aliuandikia barua Ubalozi wa Canada, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Jeshi la Polisi kuwaelezea kilichotokea kuhusiana na mwanamke huyo.

“Nilimwamini kama mke wangu, lakini akafanya kinyume,” alidai Ngwali.
Alidai awali, walipanga na Aisha kwenda Canada, akampa jukumu la kutafuta viza, lakini akiwa bungeni, mwanamke huyo aliamua kuondoka kinyemela kwenda nchini humo.

Ngwali alisema anamshangaa Khalfan kumsikia akimtuhumu kutorosha watoto wake na kudai yeye hana shida ya watoto wa mtu mwingine, kwani tayari anao watoto wanne aliozaa na mkewe wa kwanza.

“Huyu bwana anacholilia ni wivu tu wa mapenzi. Haya mambo ukiyasikia ni ya ajabu. Kwani aliwahi kunitaka nimfidie. Hao watoto siyo wangu, vipi unilalamikie mimi?” alihoji na kuongeza: “Anataka kunichafulia jina.”

Alimshauri Khalfan kwenda mahakamani, akidai huko ndiko haki inakotolewa badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ili kumchafulia jina, kwani kwa kufanya hivyo hakuna faida yoyote anayoweza kuipata. Alidai pia anamshangaa Khalfan kumtuhumu kwamba, amebadili majina ya watoto wake bila kuthibitisha tuhuma hizo.

Ngwali alidai kwamba ni jambo lisilowezekana kubadili majina ya watoto kwani ilitakiwa aende kufanya hivyo mahakamani.

Pia alidai tangu azaliwe hajawahi kwenda mkoani Tanga na watoto hao hawamo kwenye pasi yake ya kusafiria.

“Mimi hawa watoto siyo wangu. Ninao wangu wa halali. Kama kuna mtu kabadilisha majina yao, mimi sijui. Na atoke mtu yoyote duniani athibitishe hilo, nitawajibika,” alidai Ngwali na kuendelea:

“Yule mwanamke ana asili ya Kiarabu na Khalfan ana asili ya Kiarabu. Mimi ni Mswahili. Hiyo ndiyo asili ya chuki na huyu bwana. Kwamba, kwanini Mswahili aoe Mwarabu? Sasa tatizo hapa siyo watoto, bali tumkomoe.”

Ngwali alidai kama ni uchungu, basi yeye ndiye anayeumia zaidi kwani alikuwa akiwalipia watoto hao ada ya shule Shilingi milioni tatu kwa mwaka.

“Hivyo, yote anayosema ni uwongo. Anataka aonewe huruma. Ni wivu tu wa mapenzi ndiyo unaomsumbua. Kwa hiyo, hiyo story (habari). Ni watu wanaogombea mwanamke na sote tumemkosa.”
Ngwali alidai sehemu kubwa ya maelezo hayo aliyatoa alipohojiwa na vyombo vya dola, ikiwamo interpol.

KAULI YA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kinondoni, John Mtalimbo, alisema taarifa za Khalfan kufungua jalada hilo katika kituo hicho alizisikia jana, hivyo alimtaka mwananchi huyo kwenda ofisini kwake leo asubuhi ili kujua suala lake lilipofikia.

Hata hivyo, alisema kwa jinsi lilivyo, suala hilo ni kubwa, ambalo hata kama jalada lake lilifunguliwa katika kituo hicho, bado linahusiana na Interpol. Pia NIPASHE ilijaribu kuwasiliana na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, kueleza sababu za shauri hilo kuchukua muda mrefu, lakini hakupatikana.
Alipopigiwa simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake, ambaye alisema angemfikishia bosi wake ujumbe wa kutafutwa na mwandishi.
CHANZO: NIPASHE
 
Mapenzi kitovu cha uzembe.
Ila hadi mke anaibiwa alikuwa wapi? Ukute aliwatelekeza sasa anajitafutia malipo ya bure
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mi nilikuwa nahisi hili tukio limetokea Zenj...kumbe hapa Ilala!! Muungano huu lazima tuudumishe...
 
CYCLE OF OPRESSION AT WORK!!!!!!!!!! Wale mlionitupia mishale ya sumu Hapa Mnalipi la Kusema??????? Au Lara 1 alimbebea mabegi Mrs Khalfan kuhamia kwa Pedeshee Mbunge!

Wanaume msipojipanga kiuchumi ndo kama hivi Wife anamegwaaaaaa weeeeeeee, akiwanogea wanamchukua jumla kama hivo na watoto wako wanabadilishwa ubini! Mazafantaaa kweli hawa Preditors!

IN THIS LIFE YOU ARE EITHER A PREDITOR OR A PREY!!!!!!!! Hapo Bwana Khalifa ndo prey maskini ya Mungu! Atleast he is putting a fight ingekuwa Sumu angekufa kimyakimya!
 
Last edited by a moderator:
hebu aache ujinga watoto wanasomeshwa canada kwa raha zao tena ukute wako happy kuliko walivyokua na baba yao!ataibiwaje mke mpaka aolewe kabisaaa na usipinge before marriage?huyu jamaa ni mfa maji tu
 
Sidhani kama mke anaweza kuporwa kutoka kwa mumewe bila yeye mwenyewe kuamua kuondoka.Mke kama mtu mzima mwenye akili zake timamu na mwenye maamuzi yake hawezi akachukuliwa tu kama parcel,ni lazima yeye mwenyewe ameridhia kuondoka kwa huyo x husband wake.Haikuwa na haja ya kufungua kesi kudai kuporwa mke,sana sana huyo jamaa angefungua kesi tu ya kudai watoto provided kuwa ana evidence ni watoto wake kabisa.Duniani kuna vituko.mmmhhh
 
Simple words.....usicheze na mwanamke, hujui anachoweza kufanya.
 
Huyo bwaana Khalifani , inaonyesha alimtelekeza huyo bibie Aisha na watoto, na akaamua kumkomoa kwa kutompa Talaka, na Pia alitaka sifanye kazi akae ndani, kwani yeye kawa fenicha? sasa kaona kapata mwanaume , tena mwenye nafasi yake, roho yamuuma, hana lolote, analo hilo. Na Namuombea huyo mama Mungu amuepushie balaa la kurudishwa hapa nchini, maana unaweza kuta watoto wake wanasoma kwa raha mustarehe, na wanapata kila kitu. Mimi nashangaa sana wanaume, wanataka wakikuacha utesekeeeeeeee mpaka, ili wao wawe na raha mioyoni mwao, na wanasahau kuwa wao si Mungu.
 
hapo kwenye red ,huwa wanafurahi sana kuona unaranda na njia ukifanikiwa khekhekhe wata jifanya oh bado ni mke wangu nmpenda halaaa namwambie kwenda kule hata paka wanazaaa na hawajui baba halisi fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
CYCLE OF OPRESSION AT WORK!!!!!!!!!! Wale mlionitupia mishale ya sumu Hapa Mnalipi la Kusema??????? Au Lara 1 alimbebea mabegi Mrs Khalfan kuhamia kwa Pedeshee Mbunge!

Wanaume msipojipanga kiuchumi ndo kama hivi Wife anamegwaaaaaa weeeeeeee, akiwanogea wanamchukua jumla kama hivo na watoto wako wanabadilishwa ubini! Mazafantaaa kweli hawa Preditors!

IN THIS LIFE YOU ARE EITHER A PREDITOR OR A PREY!!!!!!!! Hapo Bwana Khalifa ndo prey maskini ya Mungu! Atleast he is putting a fight ingekuwa Sumu angekufa kimyakimya!

:becky::becky::becky: naona jibu limejibilika mama
 
Huyo bwaana Khalifani , inaonyesha alimtelekeza huyo bibie Aisha na watoto, na akaamua kumkomoa kwa kutompa Talaka, na Pia alitaka sifanye kazi akae ndani, kwani yeye kawa fenicha? sasa kaona kapata mwanaume , tena mwenye nafasi yake, roho yamuuma, hana lolote, analo hilo. Na Namuombea huyo mama Mungu amuepushie balaa la kurudishwa hapa nchini, maana unaweza kuta watoto wake wanasoma kwa raha mustarehe, na wanapata kila kitu. Mimi nashangaa sana wanaume, wanataka wakikuacha utesekeeeeeeee mpaka, ili wao wawe na raha mioyoni mwao, na wanasahau kuwa wao si Mungu.

Hivi mahakama inatambua ndoa za wake wengi? huyu mwanamke tunahisi alitelekezwa mbunge akaona ganda la jana nakuamua kusimamia show nzima, sasa mahakama inatambua mtu anae miliki wake 3 mpaka anashindwa kuwahudumia?
 
Hapo sasa mimi ndiyo nashindwa kushangaa, yeye bwana Khalifani kashindwa kumtimizia , bibie Aisha kapata wa kumtimizia , sasa anapiga kelele za nini wakati kashindwa,kumtimizia haja zake na hakuna kitu nakasirika kama mwanaume anayetaka mke akae home bila kazi, ili amtawale, na anapenda uwe unaomba mpaka ped, hii makitu huwa inanitia hasira sana. :A S angry::A S angry::A S angry:
 
tatizo lipo kwenye swali langu la msingi, Je mahakama inatambua ndoa za wake wengi? Kama inatambua basi huyu Bi Aisha ni mke halali wa ustadhi Khalfan hata kama alikuwa hatimiziwi mapenzi na haki nyingine za kibanadamu alipaswa kumshtaki au kudai haki zake za msingi, hivyo basi makahama itamtia hatiani mbunge kwa kumrubuni mke wa mtu
 
Huyu bwana Khalfan anakumbuka shuka kumekuchaaa! ivi hana kazi yakufanya anaemgombania mke aloamua kwenda kwao
Hajampa talaka mda wote uwo nani alikua anampa matumizi? kama yeye alikua hapeleki vp aseme mkewe? naende zake uko
yeye alisema wanini mbunge alikua anaomba atampaka lini na yeye ....
 
hapo kwenye red ,huwa wanafurahi sana kuona unaranda na njia ukifanikiwa khekhekhe wata jifanya oh bado ni mke wangu nmpenda halaaa namwambie kwenda kule hata paka wanazaaa na hawajui baba halisi fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Na akijua unaranda na njia , basi si kujitapa huko, kuwa alikuwa anamtunza, anampa kila kitu, kakimbia mwenyewe, ona anayowayawaya, basi alimradi anamnanga tu mtoto wa watu , Mungu akipitisha Kheri zake wanaanza kupiga mayowe wanasahau kuwa Mwenyezi Mungu, huwa si Juma, wala Khamisi, hapo ndipo wanashika adabu zao, maana hutoa Riziki kwa wote bila kuangalia sura wala rangi.
 
Mama na watoto wako Canada na baba yao mpya. Huku jamaa wanaumizana.

"Know, O Vizir (to whom God be good!), that the stratagems of women are numerous and ingenious. Their tricks will deceive Satan himself..."
The Perfumed Garden - Sheikh Nefzaoui and Translated by Sir Richard Burton
 
Back
Top Bottom