Mbuga zetu za wanyama zilitukosea nini...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mwamko wa kutembelea urithi wetu haupo...
Wengine mara ya kwanza kuwaona wanyama ni safari kupitia mbugani...
Sikumbuki kama nimewahi kuwaona viongozi wetu wakitembelea kama mfano na motisha...

Unadhani nini kinatukwamisha kutembelea mbuga zetu za wanyama...

Yaani mtu hadi anazeeka simba, chui, Faru, tembo kama kumuona basi ni zoo au maonyesho sio kwenye anga zake mbugani...
 
Nakumbuka tulikuwa na kaka yetu ameoa mzungu wa Sweden walipokuja likizo na mkewe na mama na baba mkwe wake wazungu wakamuomba mama yetu mswahili waambatane nae kwenye mbuga za wanyama..

Alichojibu sasa!! "Eti Wazungu wasumbufu saana twende huko kwenye mbuga za wanyama Kwani tuna ndugu huko?"

Tulicheka muda mreeefu saana na ninashukuru kwani wale wazungu hawakuwepo karibu yetu maana wangehisi tunawapiga jungu kwa kiswahili.

Hili la maza linaashiria mwamko duni wa waswahili kutalii kwenye vivutio na mbuga zetu, hakuna kabisa wa kwenda mbugani maana kwa hii scenario hata mia tulikuwa hatutoi ni wao walitaka kampani tu lakini bado mother akaishangaa ile safari?
 
Back
Top Bottom