TimeStope
Member
- Mar 12, 2021
- 80
- 125
Wakati taifa letu likiwa katika usingizi mzito usiokuwa na njozi, "Muungano wa Falme za Kiarabu" (UAE) walianzisha mpango wa mda mrefu wa kuwa na mbuga za kisasa mfano wa mbuga za Tanzania, na kisha kuzipa majina yaleyale (Serengeti, Ngorongoro, Manyara, na Mikumi) kisha kununua wanyama chungu nzima, wa kila aina kutoka huku huku Afrika na kuwaweka katika mbuga hizo katika mpango wao wa mda mrefu.
Mwezi 2 au 3 kama sikosei, walizindua mbuga hizo maridadi na wanazitangaza duniani kote, watalii wengi hivi sasa wanaelekea huko.
Mbuga hizo hazina tofauti na mbuga zetu, kile kinachopatikana Serengeti, Ngorongoro, Manyara, na Mikumi; ndani ya "Sharjah Safari Park" kinapatikana vilevile.
Waarabu hao wameenda mbali zaidi, wameanzisha mji mkongwe mfano wa Zanzibar; na unaitwa Zanzibar.
Mji huo hauna tofauti na mji wa Zanzibar, mitaa ni ileile, majina ya mitaa, mandhari ileile, lakini yote ndani ya Sharjah.
Sasa leo tumeshtuka kutoka katika usingizi huo, tunajaribu kuanzisha mpango wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii kimataifa, lakini "it's too late!"
Hivi nani aliye turoga!?