Mbu wengine waenezao malaria waibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbu wengine waenezao malaria waibuka

Discussion in 'JF Doctor' started by Bujibuji, Nov 15, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,169
  Trophy Points: 280
  WANASAYANSI wamegundua kuzuka kwa jamii nyingine ya mbu wanaoeneza malaria ambao wanatoa changamoto kwa wataalamu wa afya duniani, sasa kutakiwa kubuni mbinu mpya za kujikinga na ugonjwa huo unaoua watu wengi kuliko magonjwa mengine.

  Mbu hao wana tabia tofauti na wale ambao wataalamu wamekuwa wakielezea mara kwa mara ndio wanaoeneza malaria.
  Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya kuambukiza na Mzio (Niaid) ya Marekani, imesema kundi la wanasayansi nchini Uingereza wamegundua aina hiyo mpya ya mbu na kutoa ripoti hiyo hadharani mwezi uliopita.

  Taarifa iliyotolewa na Niaid kwa gazeti hili ilieleza kwamba katika utafiti huo, wataalamu hao waligundua kwamba katika jamii ya mbu, Anopheles gambiae; ambao wanajulikana tangu zamani kuwa ndio waenezao malaria, imezuka jamii nyingine inayotofautiana na hiyo kitabia, mfumo wa kibaiolojia na mazingira ya kuishi.

  "Katika mbu wa kundi la Anopheles gambiae limezuka jingine linalotofautiana kitabia jambo linaloashiria kwamba wote sasa watasababisha ugumu wa kujikinga na malaria kwa njia zinazotumika sasa," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Utafiti huo ambao tayari umechapishwa kwenye jarida la kumbukumbu muhimu za kisayansi duniani, umetahadharisha kwamba tatizo hilo linazidi kuiweka katika hali mbaya zaidi Afrika kwa sababu ndiyo yenye kiwango kikubwa cha kuenea kwa ugonjwa huo, duniani.
  "Anopheles gambiae ni mbu anayeeneza malaria katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara (Tanzania ni miongoni) ambazo zina kasi kubwa zaidi ya kuenea ugonjwa huo," inaeleza taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo inaeleza kwamba utafiti huo umegundua kuzuka kwa jamii hizo mbili ambazo zinawiana kimaumbo lakini zinatofautina kwa mfumo wa vinasaba (DNA) lakini wana uwezo wa kuzaliana.
  Kuibuka kwa makundi hayo mawili ya mbu waenezao malaria, wanasayansi hao wanasema moja kwa moja yatakuwepo mabadiliko ya namna wadudu hao wanavyoeneza malaria.

  "Hii inaelekea kusababisha ugumu wa kujikinga na malaria kwa kutumia njia ambazo tayari zimebuniwa na zinatumika sasa duniani kwa sababu mfumo wa kitabia wa mbu sasa umebadilika," taarifa hiyo inamnukuu mmoja wa wanasayansi walioshiriki katika utafiti huo, Profesa George Christophides.

  "Ni wakati wa wataalamu wa afya duniani kukaa chini na kuchunguza zaidi jamii hizo ili kuibua njia mpya za kujikinga na ugonjwa huo." alisisitiza.
  Kutofautiana huko kibaiolojia, wanasayansi hao wanasema hata dawa za kuua mbu pamoja na mazalia yake zinapaswa kufanyiwa marekebisho, ili ziweze kuua jamii zote.

  Katika nchi nyingi za Afrika, Tanzania ikiwa miongoni, zimekuwa zikitumia dawa aina ya pyrethroids kwenye vyandarua ili kukabiliana na mbu waenezao malaria kwa maelezo kwamba wana tabia ya kuuma binadamu usiku wa manane.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa, hao tuliowazoea tumeshindwa kuwa-contain...halafu wanakuja aina nyingine ya mbu mpaka zijulikane njia za kuwamudu na kujikinga si tutakuwa tushakufa wengine? Dah Mungu tuepushe na janga hili..
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Siku zote hao mbu walikuwa wapi isije ikawa watu wanatengeneza mbu wa aina iyo ili makampuni ya madawa yamake?
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  miezi kama mitatu hivi BBC walilipoti kuwa wanasayansi wa uingereza wamegundua mbu na kuwazalisha ambao wana uwezo wa kutafuna/kuwaua anopheles. leo wanakuja na version nyingine.

  Is this not a man made disaster?
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Africa is dying slowly.
  Wazungu hawawezi kutokomeza malaria huku kwetu, kinachopaswa kufanyika ni sisi kuharibu mazalia na vyanzo vyote vya mbu.
  vyandarua ni miyeyusho mitupu
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ebu mtu anyoshe maelezo apa hao mbu wako UK au UK ndo wamewagundua ila sio wa uko UK?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  so is the one anayejisifia kuwa safari zke za marekani zimesaidia kuleta vyandarua, ambavyo havifit hata kwenye vitanda vya 3X6
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  mbu hao ni CCM
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nasikia ata zoezi la kugawa limesitishwa kule iringa mjini sasa sijui ni baada ya CHDEMA kuchukua jimbo au ndo Tz nzima zoezi limearishwa
   
 10. d

  dotto JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mbu wa kizungu
   
Loading...