Kwa sababu wana uzoefu wa kutosha, hili si la kulifanyia majaribio, si ajabu hao wapya wakawa PM7 wakavuruga sera hii nzuri ya majimboKwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?
Mkuu nakubaliana na wewe. Watake wasitake kama wanataka kuchukua madaraka lazima watake risks. You can not take down the system by acting like the system. Hata kwenye boxing mtu ukipambana na mtu mwenye nguvu hushindani nae kwa nguvu unatafuta njia nyingine. To win Chadema must be different na kama ulivyo sema CCM siyo wajinga kama baadhi ya watu wanavyo taka kujiaminisha au kuaminisha watu wengine.
Haya ndiyo maamuzi magumu katika chama. Hakuna kitu kigumu kama kubadilisha mtazamo na utendaji wote katika chama. Just imagine, CDM toka kianzishwe kimekuwa na utendaji uliokuwa CLOSED ( centralisation) halafu unaamuka kesho na kusema kuanzia sasa ni OPEN (decentralisation).
Ngoma iko kwa viongozi, hata hivyo inategemewa watafanikiwa kwa sababu huwezi kuwalipa viongozi zaidi ya Tsh 7 milion per month na wasiweze ku-deliver. They have to justfy...
Naomba uniweke sawa. Wapi hasa tofauti yetu inagonga kwa sababu mazingira ya kisiasa Tanzania ndiyo yanatoa mtazamo wa vigezo kwenye vetting ya viongozi wa kisiasa.Naona kama tunatofautiana hapa.Kumbuka hii hoja imeanzia kwenye vetting.
This is the fact, Kujuana is an added advantage kwenye vetting when it come to any political position in any unpredictable political field like Tanzania.Does the person qualify for the position?
Pia kuwa mwanachama si kweli kwamba umeingia kwenye system.
Kwa hili nakubaliana na wewe.Mkuu ni kweli mabadiliko ni magumu kwa binadamu ila kama kiongozi lazima uwe na vision na vision ni kuona mbele zaidi. Kitu mimi ambacho ningesuggest ni Chadema kuangalia wapi wenzao walipo teleza. Kama tunavyo jua historia ya nchi yetu vyama vya upinzani vyenye nguvu vimekuja na kuondoka, tuliona NCCR 1995, tukaona CUF 2000 na sasa Chadema 2010 mpaka sasa. Inarudi pale pale kwamba CCM siyo wajinga kama watu wanavyo dhani. Ni lazima Chadema ikae na kutafakari what went wrong na wenzio (NCCR, CUF) na wao wafanyeje kuepuka hilo. Mimi ningekua Chadema ningetumia haswa haswa CUF as a case study kwa sababu njia CCM walioitumia kuki assasin CUF ndicho wanacho tumia kwa Chadema which ni kupaint Chadema kama chama cha dini fulani na majimbo fulani. Kwa kiasi fulani CCM imefanikiwa kwa hilo kwa sababu kuna a significant namba of people wanao kiona Chadema kama chama cha Kikatoliki na Kilimanjaro. Hilo wasipuuzie hata kidogo haswa kuelekea 2015 ambapo hamna incumbent na hamjui CCM itamsimamisha nani.
Hii ni kweli kwa siasa za Tanzania. Angalia siasa za wenzetu hasa wa West. Kila kitu kinakuwa justfied kutolewa na kupokelewa not based on emotion kama ilivyo kwa Tanzania.Kuhusu hilo la kujustify mishahara mkuu ni a given. Halafu siasa bwana mchezo mchafu sana, ukiwa at the hight of your fame you can do no wrong (kama ilivyo kuwa kwa JK 2005) lakini watu wakisha anza kukuchoka tu (na hii humtokea kila mwanasiasa) basi hapo ndipo hata swala dogo linapo kuzwa. Sasa hivi wanaweza wakaamua kumlipa Slaa hata milioni 20 kwa mwezi na hakuna atakae hoji.
Kwa sababu wana uzoefu wa kutosha, hili si la kulifanyia majaribio, si ajabu hao wapya wakawa PM7 wakavuruga sera hii nzuri ya majimbo
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?
Kweli wanasiasa wanaongoza kuota ndoto za mchana..Tena wanasiasa wa Tz kama wamelogwa hawataki kuongea ukweli kabisa.Mmelaniwa wote mnaoota Chadema kushika nchi 2015
Mbowe mbona unataka kuwaadaa wafuasi wenu mtashika dola kirahisi saabu mmeigawa nchi kikanda. Unadhani Watanzania ni wajinga wawape nchi kanda ya kaskazini.
Siku chache zilizopita, asha dii alikuja na mjadala mzuri juu ya kwanini yeye binafsi anadhania CCM itashinda uchaguzi mkuu wa 2015; Mwendelezo wa kauli kama hizi kutoka kwa Mbowe (ukiachilia ile ya mwaka jana kwamba CCM ikishinda 2015 atajiuzulu siasa), inaonyesha kwamba aidha kwa kujua au kutojua, kuelekea 2015, kutakuwa na more rhetoric (from chadema leaders) kuaminisha wananchi kwamba CCM itaanguka, kuliko effective practice/action ya kushirikiana na wananchi mapema kufanikisha hilo, hasa kwa Chadema kuachana na strategy ya kuvua wanachama milioni tano wa CCM and recruit them kuongezea idadi yao (chadema) ya wanachama takribani milioni mbili - tatu, na badala yake kujikita na swing voters bila ya kuhangaika kuwageuza kwanza kuwa wapiga kura wenye political affilitions na chadema; Kwa mujibu wa takwimu za wapiga kura 2010 ambao ilikuwa ni watanzania millioni kumi na nane, ukitoa wanachama wa CCM milioni tano, na wa chadema na vyama vingine vya siasa ambao sidhani kama wanazidi milioni tatu in total, it means column ya swing voters ni zaidi ya idadi ya wanachama wa vyama vyote vya siasa Tanzania, na hawa ndio watakuwa key to victory ya chama chochote baina ya hivi viwili iwapo turn out itakuwa ni kubwa 2015;
Unless chadema imefanya utafiti na kubaini kwamba ili kupigiwa kura na watanzania, ni lazima kwanza watanzania hao wawe wanachama wa Chadema; vinginevyo mimi kama mwanachama wa CCM pamoja na wengine wengi, tulipigia kura mgombea wa Chadema jimbo la Kawe - Halima Mdee kwani tuliona anatosha zaidi ya wagombea wa CCM na NCCR, huku kura yetu ya urais ikienda CCM kwa Kikwete kwani tulikuwa na imani nae kwamba atatekeleza mambo mengi kwa kasi zaidi baada ya serikali kuanguka 2008; mwenendo wetu wa kupiga kura kwa chadema 2010 (ubunge) means Chadema ina kura nyingi zaidi katika column ya swing voters (let alone ccm members) hata kama hawatakuwa wanachama wa Chadema by 2015; all Chadema needs is to engage them kisaikologia na kuwahamisha wajitokeze 2015, hasa kwa kuwa na rekodi zao ili wawe in constant communication kuliko kuhangaika kukusanya kadi za CCM; isitoshe, enzi za mass - based political parties zimeshapitwa na wakati, it no longer works for CCM, so Chadema should stop copying something which is already obsolete;
Vinginevyo, kama ya 2010 yatajirudia ambapo zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakujitokeza kupiga kura, Chadema wasisahau kwamba a low voter turn out 2015 itakuwa ni ushindi wa CCM kwenda ikulu;
nani asiyejua wote wanao kishabikia magamba kwa sasa wana maslai,nani asiyejua njaa na hujuya wa kutokujua wapi mnapokwenda,kwa kupewa kofia,kanga,pilau,2000,mjinga atabaki na ujinga wake werevu watajua wapiana kwenda,ashukuriwe mungu wajinga wamebaki wachache,kuliko werevu ndiomaana leo ccm hawalali maana mtaji wao wajinga wamebaki wachache,tuliatu utapata akili 2015 rais kutoka cdm akila kiapo cha kuongoza nchi,Kweli wanasiasa wanaongoza kuota ndoto za mchana..Tena wanasiasa wa Tz kama wamelogwa hawataki kuongea ukweli kabisa.Mmelaniwa wote mnaoota Chadema kushika nchi 2015
Umelaaniwa wewe unayedhani mpaka leo CCM ni chama cha siasa kumbe ni bendi ya taarabu na genge la wahuni fulani.
ile vita ya udini mliopandikiza mmefanikiwa sana ndio maana znz sasa hivi mnavuna sasa endekezeni na hii ya ukabila! si unakumbuka wakati mzee dhaifu alipoona dr slaa kampumulia kooni akaanza ooh wakristu ooh sijui ni ni na wewe anza kuachama tuMbowe mbona unataka kuwaadaa wafuasi wenu mtashika dola kirahisi saabu mmeigawa nchi kikanda. Unadhani Watanzania ni wajinga wawape nchi kanda ya kaskazini.
Very interesting topic. Let me add my two cents into the discussion.
Kama mkuu Mchambuzi alivyo sema hapo juu kuna a lot of rhetoric coming out of Chadema na hata ukiangalia washabiki wengi wa Chadema humu ndani (kama kweli ni washabiki wa Chadema maishani au mitandaoni tu) utakuta kauli nyingi ziko based on emotions (hisia). Mwaka 2010 kuna wanaJF wengi walio kuwa wakii support Chadema (at least humu ndani, sijui mchango wao kiuhalisia) ambao walikua wana apa humu kwamba lazima Chadema itashinda 2010. Sisi ambao hatukua emotional about it tukasema its a premature declaration tuka tukanwa na kuitwa "mamluki", "mafisadi", nk. Matokeo yake Chadema ikashindwa 2010 na kwa sababu walisha jiaminisha kwamba ushindi ulikua must badala ya kujichunguza baada ya uchaguzi what went wrong kimbilio ikawa kwamba kulikua na uchakachuaje nk. Niwakumbushe tu watu kuhusu uchaguzi wa uraisi wa mwaka wa jana Marekani. Kambi ya mpinzani wa Obama, Mitt Romney na chama chake walisha jiaminisha ushindi na kujilisha data zisizo za ukweli kiasi kwamba matokeo ya uchaguzi yalipo anza kutiririka walishikwa na butwa.
Kitu kimoja nilicho gundua kuhusu siasa za Tanzania, na hii ni kwa vyama vyote, ni kwamba siasa zetu ni za kienyeji. Kwa wenzetu kama Marekani kuna kuwa na wanasiasa ambao kazi yao ni kutoa rhetoric na topic points lakini nyuma yao kuna wataalamu haswa wawe wa kukusanya data (research), wa communications (speech) nk. Kwa hiyo unakuta mgombea ndiyo mwanasiasa lakini behind him kuna team of professionals. Sisi kwenye chaguzi zetu kila mtu ni mwanasiasa kwa hiyo unakuta they has been no research done what so ever. Sijui kwa upande wa Chadema ila mimi ningekua na cheo Chadema baada ya 2010 ningetaka status report ya what went wrong. Ningetaka uchunguzi ufanyike na wataalamu siyo wanasiasa waangalie je ujumbe wetu ulipokelewaje na different groups of people (wa mjini/vijijini, wanaume/wanawake, wazee/vijana nk.). Pia ningeagiza kwamba kila baada ya muda fulani ifanyike polls kuangalia uhalisia wa kukubalika kwetu. Kumbuka kujaza watu kwenye mikutano haimaanishi kukubalika kwenye sanduku la kupigia kura. Sidhani kama kume wahi tokea mashabiki wa chama passionate kama wa CUF lakini leo chama kikoapi.
Kwa hiyo ushauri wangu kwa vyama vyote, especially CCM na Chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 ningeomba wafanye professional research na kujipima uhalisia wa kukubalika kwao. Watu wanasahau Tanzania ni nchi ya watu milioni 45 na wengi wanaishi mjini lakini watu wakiona kwenye tv mikutano ya kivyama ya mjini imejaa watu wao wana chukulia kama ishara ya chama kukubalika kiasi hicho nchini kote na hii ina tokana na too much emotions and lack of professionalism. Mfano ni huu wa Mbowe kusema ujumbe wao wa kimajimbo unakubalika na ndiyo utawafikisha ikulu 2015. Hajaonyesha any study or research kuprove so which means kauli ni either rhetoric as usual au its based on emotions.