Mheshimiwa mwenyekiti Wangu utakubaliana nami kuwa chama chetu taratibu kimeanza kupoteza mvuto wake wa asili uliokuwepo hapo awali. Wajinga wengi wanadhani labda ni kutokana na kile wanachokiita ni utendaji wa kiwango cha juu cha mheshimiwa sana pale white house.
Lakini sisi tunaojua fikra na itikadi ya chama chetu tunajua hiyo siyo sababu, sababu ni utendaji mbovu wa Katibu wetu wa sasa. Kuna jambo haliendi sawa katika ofisi ya Katibu.
Chadema imeanza kuporomoka kwa kasi sana kimvuto, ile dhana ya watu kupeperusha bendera za chadema Katika nyumba zao na sehemu za biashara haipo tena.
Chadema imekaa mbali sana na watu, imekuwa sawa na SAU au TADEA. Husikii kashi kashi tena kama ilivyokuwa hapo awali.
Nadhani kuna tatizo kwenye fikra mpya za Katibu wetu, kuna kasoro kwenye itikadi anazojaribu kujenga Katibu wetu. Tumehama kutoka katika imani ya chama, tunakwenda bila dira huku tukisubiria Mkuu pale white house ataamka na lipi dhidi ya vyama vya upinzani. Inatakiwa sisi vyama vya upinzani tumuamshe Mkuu pale white house na si yeye kutuamsha sisi.
Nakupa mifano michache tu:
1. Hakuna kesi iliuofunguliwa kupinga katazo la kufanya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa kinyume na katiba ya nchi. Hii si chadema ninayoijua mimi
2. Hakuna tamko makini wala wazo mbadala dhidi ya hama hama ya wabunge, madiwani na viongozi wetu wengine wa chama. Hii si chadema ninayoijua mimi
3. Kupokea kila mwanachama anayekuja chadema pasi na kujali mwenendo wake wa kimaadili wa siku za nyuma. Tena tunawapokea hata kama tuliwahi kuwashutumu vikali huko nyuma. Hii si chadema ninayoijua mimi
4. Kususia chaguzi ndogo za marudio za wabunge na madiwani. Brother, pale umeingizwa chaka, ndiyo maana wale chadema asili waliipinga kamati kuu ya chama kwa kutoa matamko na baadhi ya sehemu kusimamisha wagombea kinyume na tamko la chama. Hii si chadema niijuayo
5. Chama hakijulikani kinasimamia itikadi ipi kwa sasa. Mtaji wetu mkuu wa kisiasa ulikuwa ni ufisadi, kinyume chake, wale tuliokuwa tukiwatuhumu sasa ndiyo wapo upande wetu. Hapa ndiyo maana hutaona mtu kama Mnyika anafungua mdomo wake tena kusema, wala hatutaona makeke yake ya mwanzo kwa kuwa itakuwa ni sawa na kujipaka kinyesi chake mwenyewe.
Turudishe kwenye mstari Mwenyekiti, tunahitaji Katibu ambaye anaijua vyema itikadi na imani ya CHADEMA.
Tunahitaji katibu ambaye ameshiriki kushusha bendera za ccm siku za nyuma na kisimika bendera za CHADEMA.
Mtu ambaye ameshiriki kikamilifu katika kuchora fikra za chadema kwenye mioyo ya watu.
Binafsi, mashinji hatoshi hata kidogo kuwa Mtendaji Mkuu wa chadema. Anaweza kuwa na fikra nzuri lakini zitachukua muda mrefu kututoa hapa tulipo.
Mpeni gari Mnyika atupeleke kule tulipokuwa tukienda