Mbowe shtuka, Mashinji anakupeleka chaka

Mbowe shtuka, Mashinji anakupeleka chaka

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Mheshimiwa mwenyekiti Wangu utakubaliana nami kuwa chama chetu taratibu kimeanza kupoteza mvuto wake wa asili uliokuwepo hapo awali. Wajinga wengi wanadhani labda ni kutokana na kile wanachokiita ni utendaji wa kiwango cha juu cha mheshimiwa sana pale white house.

Lakini sisi tunaojua fikra na itikadi ya chama chetu tunajua hiyo siyo sababu, sababu ni utendaji mbovu wa Katibu wetu wa sasa. Kuna jambo haliendi sawa katika ofisi ya Katibu.

Chadema imeanza kuporomoka kwa kasi sana kimvuto, ile dhana ya watu kupeperusha bendera za chadema Katika nyumba zao na sehemu za biashara haipo tena.

Chadema imekaa mbali sana na watu, imekuwa sawa na SAU au TADEA. Husikii kashi kashi tena kama ilivyokuwa hapo awali.

Nadhani kuna tatizo kwenye fikra mpya za Katibu wetu, kuna kasoro kwenye itikadi anazojaribu kujenga Katibu wetu. Tumehama kutoka katika imani ya chama, tunakwenda bila dira huku tukisubiria Mkuu pale white house ataamka na lipi dhidi ya vyama vya upinzani. Inatakiwa sisi vyama vya upinzani tumuamshe Mkuu pale white house na si yeye kutuamsha sisi.
Nakupa mifano michache tu:

1. Hakuna kesi iliuofunguliwa kupinga katazo la kufanya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa kinyume na katiba ya nchi. Hii si chadema ninayoijua mimi

2. Hakuna tamko makini wala wazo mbadala dhidi ya hama hama ya wabunge, madiwani na viongozi wetu wengine wa chama. Hii si chadema ninayoijua mimi

3. Kupokea kila mwanachama anayekuja chadema pasi na kujali mwenendo wake wa kimaadili wa siku za nyuma. Tena tunawapokea hata kama tuliwahi kuwashutumu vikali huko nyuma. Hii si chadema ninayoijua mimi

4. Kususia chaguzi ndogo za marudio za wabunge na madiwani. Brother, pale umeingizwa chaka, ndiyo maana wale chadema asili waliipinga kamati kuu ya chama kwa kutoa matamko na baadhi ya sehemu kusimamisha wagombea kinyume na tamko la chama. Hii si chadema niijuayo

5. Chama hakijulikani kinasimamia itikadi ipi kwa sasa. Mtaji wetu mkuu wa kisiasa ulikuwa ni ufisadi, kinyume chake, wale tuliokuwa tukiwatuhumu sasa ndiyo wapo upande wetu. Hapa ndiyo maana hutaona mtu kama Mnyika anafungua mdomo wake tena kusema, wala hatutaona makeke yake ya mwanzo kwa kuwa itakuwa ni sawa na kujipaka kinyesi chake mwenyewe.
Turudishe kwenye mstari Mwenyekiti, tunahitaji Katibu ambaye anaijua vyema itikadi na imani ya CHADEMA.

Tunahitaji katibu ambaye ameshiriki kushusha bendera za ccm siku za nyuma na kisimika bendera za CHADEMA.

Mtu ambaye ameshiriki kikamilifu katika kuchora fikra za chadema kwenye mioyo ya watu.

Binafsi, mashinji hatoshi hata kidogo kuwa Mtendaji Mkuu wa chadema. Anaweza kuwa na fikra nzuri lakini zitachukua muda mrefu kututoa hapa tulipo.

Mpeni gari Mnyika atupeleke kule tulipokuwa tukienda
 
Mhhh!! Ngoja waje wenye chadema yao
Usimbebesha Mashinji lawama hasizostahili. Mapungufu uliyoyataja ni makubwa sana na hayajasababishwa na Mashinji.

Kama ungekuwa mkweli lawama zingeenda kwa Mbowe, kiongozi mkuu na aliyehodhi madaraka ya maamuzi.

Hata hivyo sema matatizo yalianza pale mwenyekiti alipokiongoza chama kubadili gia angani. Mengine yote ni tafuta mchawi.
 
Kwa pamoja tuseme Joyce ...
Matatizo ya familia sio vizuri kuyahusisha na chama as long ni vitu tofauti, je mke wa mbowe akija akasema mbowe ana kibamia mtaanzisha harakati kumtoa uenyekiti kisa hata akili itakuwa ya kibamia!?..
 
Mashinji atakuwa scapegoat mpya kwa matatizo ya chadema. Japokuwa yeye ameshindwa kuvaa viatu vya Dr Slaa, lakini sio sababu ya uzorotaji wa Chadema.

Tatizo liko kwa Katibu mkuu NA siasa zake za kiburi.

Mashinji mnamuonea kapewa gari bovu alafu mnataka ashindana NA gari lilokarabatiwa vizuri
 
Kumbuka mashinji ndiye mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku za chama
 
Ngoja waje, watakuogesha mitusi mpaka utajilaumu.
Ila kusema ukweli una hoja nzuri na za msingi, ingawa umesahau kwamba mbowe ndo anaiua chadema. Tumeshayasema haya muda mrefu, tulichoambulia ni matusi tu. Wafuasi wa [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] ni watukanaji kama kiongozi wao.
Na watukane lakini ukweli haujifichi kwenye chungu
 
Ngoja waje, watakuogesha mitusi mpaka utajilaumu.
Ila kusema ukweli una hoja nzuri na za msingi, ingawa umesahau kwamba mbowe ndo anaiua chadema. Tumeshayasema haya muda mrefu, tulichoambulia ni matusi tu. Wafuasi wa [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] ni watukanaji kama kiongozi wao.
Hahaha eti [HASHTAG]#lissumsaliti,[/HASHTAG] uwiii
 
Hahaha eti [HASHTAG]#lissumsaliti,[/HASHTAG] uwiii
Hovyo sana, tunakuwa na chama kikuu cha upinzani ambacho kina viongozi waoga waoga
 
Matatizo ya familia sio vizuri kuyahusisha na chama as long ni vitu tofauti, je mke wa mbowe akija akasema mbowe ana kibamia mtaanzisha harakati kumtoa uenyekiti kisa hata akili itakuwa ya kibamia!?..
Ehh
 
Usimbebesha Mashinji lawama hasizostahili. Mapungufu uliyoyataja ni makubwa sana na hayajasababishwa na Mashinji.

Kama ungekuwa mkweli lawama zingeenda kwa Mbowe, kiongozi mkuu na aliyehodhi madaraka ya maamuzi.

Hata hivyo sema matatizo yalianza pale mwenyekiti alipokiongoza chama kubadili gia angani. Mengine yote ni tafuta mchawi.
Katibu ndiye mtendaji wa chama
 
Chadema bado kuizika tu ishakufa yule masizi hata kuongea hajui yani viatu vya slaa vina mpwaya kabisa
 
Huyo unayemshauri akipitia huo Uzi wako atakuwa anasoma mistari kadhaa anakaa anacheka kidogo kisha anaendelea na baada ya mistari kadhaa mingine anacheka zaidi hadi anakung'uta viganja. Hadi aje kufika mwisho atakuwa mbavu hana amelala chini na machozi yanamtoka. PENGINE NA WEWE HUIJUI CHADEMA YA SASA!
 
Back
Top Bottom