Mbowe: Polisi tukutane Mahakamani ila siwapi Ushahidi

mukizahp2

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
705
Reaction score
378
IKIWA leo ni siku ya mwisho aliyopewa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Jeshi la Polisi nchini kuwasilisha ushahidi wa kuhusika kwa jeshi hilo na mlipuko wa bomu uliotokea mwezi uliopita mkoani Arusha, kiongozi huyo amegoma kuutoa.

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake leo kabla ya saa nane mchana, kiongozi huyo amewataka polisi kumpeleka mahakamani kwani hatawapa ushahidi huo.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema kamwe hawezi kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake walioamua kutoukabidhi ushahidi huo kwa polisi hata kama watawapa vitisho kama walivyozoea.

Alibainisha kuwa alipokea barua iliyomtaka aende polisi leo na ataitikia wito huo, lakini hatapeleka ushahidi wanaoutaka, kwakuwa wao ni watuhumiwa.

Alisema CHADEMA ilimwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ikimwomba kuunda tume huru ya majaji kwa ajili ya tukio hilo, ambayo wataikabidhi ushahidi wao.

Aliongeza kuwa masuala muhimu yagusayo chama na masilahi ya taifa yanafanyika kulingana na maamuzi ya vikao, hivyo yeye hawezi kwenda kinyume cha kilichoamuliwa.

Kwa mujibu wa Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, suala la Arusha linahusisha viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA, hivyo lilifikishwa kwenye vikao na kufanyiwa uamuzi wa kutopeleka ushahidi polisi.

"Nina mambo mengi ya kukutana na polisi, nitaitikia wito wao lakini kuhusu kupeleka huo ushahidi ni msimamo wa chama kwamba hatupeleki… waende mahakamani, wachukue hatua za kisheria au waamue lolote.

"Tunasubiri kauli ya rais ya ama ataunda tume ama hataunda tume huru ya kimahakama yenye majaji. Lakini pia ninamsubiri mwanasheria wa chama ambaye anakuja kutoka Tabora, polisi nitaenda tu," alisema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Barua ya polisi
Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake Julai 23 (leo) kabla ya saa nane mchana.

"Kutokana na mahojiano uliyofanya na Polisi Mkoa wa Arusha mnamo Juni 20, 2013 kuhusu mauaji yaliyotokana na ulipuaji wa bomu huko Soweto, Arusha ulidai kuwa unao ushahidi unaobainisha wahusika wa tukio hilo.

"Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 202, unaamriwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai tarehe 23 Julai, 2013 saa nane mchana bila kukosa na ulete ushahidi huo.

"…Unatahadharishwa kuwa kushindwa au kukataa kufika na kuleta ushahidi huo ni kosa la jinai chini ya sheria iliyotajwa," inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussein Laisseri, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Juni 15, mwaka huu wakiwa kwenye mkutano wa wazi uliokuwa ukihutubiwa na Mbowe katika viwanja vya Soweto mjini Arusha wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani wanne, bomu la kutupwa kwa mkono lililipuka na kusababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine 70.

Awali jeshi hilo lilituma viongozi wake wa juu mkoani Arusha kwa ajili ya uchunguzi, ambapo waliwahoji watu kadhaa akiwamo Mbowe, kwamba alisema alimwona aliyelipua bomu hilo kuwa ni askari polisi na kuweka bayana kwamba hawezi kuutoa ushahidi huo kwa polisi kwa madai kuwa watauharibu.
 
Kwani safari hii kaandaa shilingi ngapi ya kuwahonga majaji make ya lwakatare aliandaa kiasi kikubwa.
 
[TD="bgcolor: #ffffff"]

[TD="bgcolor: #ffffff"]
TANZANIA DAIMA 23/7/2013

[/TD]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TD]
Kauri hii siyo bure polisi wawe makini anaweza kufa mtu hawa watu kuuwa kwaokama kawa tu,polisi jiandaeni mwenzenu hamaanishi mahakama kweli ni lugha ya picha tu.
 
naona thread yako ya kijinga ya tetesi red brigade kutembea na tindikali imefutwa
hivi zaidi ya box huna kazi ingine ya kufanya?
unaandika taarabu kwenye siasa wapi na wapi?
acha majungu kama watu wa mombasa.
dunia ya leo sio ya kupayuka bila ushahidi.

Iko siku tutawanasa tu, dawa iko jikoni
 
Logic ya polisi siielewi kabisa. CDM imewatuhumu ninyi, na ushahidi unawahusu ninyi, then mnalazimisha mpewe ushahidi. Mbowe akitoa ushahidi kwa polisi yatakuwa maajabu ya karne.

Nawashauri polisi wapeleke kesi mahakamani.
 
mkuu kigezo kimojawapo cha kuwa polisi ni kufeli kidato cha nne au cha sita.
 
kwa hiyo report yao inasubiri ushahidi wa Mbowe ili kiwe kiambatanisho au vp? wasema kama wameshindwa ili kuliko kujiabisha kwa kiasi hiki yale ya kiana victor hd leo hatujui muendelezo wake, polisi na bange kimya hivi hawa wanaweza kuchunguza nn na kikaisha kwa wakati
 
mbwa hufugwa kwa kulinda binadamu na mali zake(kuna watu wameingia humu wamemla sana huyo myama)sasa kujibizana nao ni sawa kuwa una wadudu kichwani goodluck kwa wagonjwa tuliowafukuza kwenye chadema yetu
 
Kwa maana hiyo kama Mbowe asingekuwa na ushahidi, ndo basi tena, uchunguzi wa tukio la Soweto ungebaki kuwa historia bila kukamatwa mtu yeyote? Wale mapolisi waliokuwepo uwanjani wakati tukio likitokea hawakuona lolote? Mwigulu na Lukuvi si pia wanao ushahidi kuwa ni CDM imejilipua, mbona hawabughudhiwi na Polisi ili nao watoe ushahidi wao?
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, wezi wanavunja mpaka kituo cha polisi . Mijitu inashupalia siasa utafikiri ndio kazi yao .
 
uwezo wa jeshi letu la polisi ni mdogo sana, eti mpaka sasa tume iliyoundwa haina haijapata chochote. watanzania sasa tunaamini wachawi wa mikutano ya cdm ni polisi. Kwa hili polis mnajua mmehusika.
 
Rais Kikwete aliwahi kusema anayo majina ya wafanyabiashara ya madawa ya kulevya(janga la dunia nzima),naye hatujasikia akikabidhi polisi.Rais yuko juu ya sheria?Dr Ulimboka aliyetekwa na kuteswa nusu mfu,amemtaja aliyemfanyia hayo kwa kiapo,lakini hawakumhoji Ulimboka wala kumkamata aliyetajwa kwa upelelezi.Kwa nini Mbowe?Mh Mwigulu aliwahi kusema anao ushahidi CDM wakipanga mauaji na watu watakufa mikutano ya CDM.Naye hakuitwa kuhojiwa.Kwa nini Mbowe?Hivi wakosaji ni viongozi wa CDM tu?Inatia hasira.
 
Iko siku tutawanasa tu, dawa iko jikoni
Tumekusikia retired cop! Hizo nguvu mnazotaka muelekeze kwenye kumnasa Mbowe kwanini msielekeze kutafuta watesaji wa Ulimboka na Kibanda? Kwanini msielekeze kwa majambazi wanaotuvunjia na kutuibia kila uchwao? Acheni bangi nyie.
 
Logic ya polisi siielewi kabisa. CDM imewatuhumu ninyi, na ushahidi unawahusu ninyi, then mnalazimisha mpewe ushahidi. Mbowe akitoa ushahidi kwa polisi yatakuwa maajabu ya karne.

Nawashauri polisi wapeleke kesi mahakamani.
naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom