Mbowe: Nitamzungumzia Dk. Slaa muda ukifika

Mbowe: Nitamzungumzia Dk. Slaa muda ukifika

Dupe

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
1,668
Reaction score
813
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (pichani) amezungumzia kukosekana kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa katika vikao vya chama hicho vinavyoendelea jijini, akisema: "Nitazungumzia suala hilo muda muafaka ukifika."

Mbowe alisema hayo jana katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach kilipokuwa kinafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema jana.

"Siwezi kusema zaidi ya hapo," alisema Mbowe alipoulizwa sababu za kutokuwapo Dk Slaa katika vikao hivyo muhimu na kuongeza atatoa baadaye, mrejesho wa kikao hicho.

Kauli hiyo ya Mbowe haikuondoa wingu zito lililotanda Chadema baada ya kutoonekana hadharani kwa kiongozi huyo katika matukio manne muhimu ya chama hicho kikuu cha upinzani, tangu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ajiunge nacho.

Tofauti na Dk Slaa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika alionekana jana kwa mara ya kwanza katika kikao hicho na kufuta uvumi uliokuwa umesambaa kuwa alikuwa na mpango wa kuachana na Chadema kama inavyodaiwa kwa Dk Slaa.

Viongozi hao walianza kutoonekana katika shughuli za chama tangu Lowassa alipojiunga na Chadema Julai 28 na kukabidhiwa fomu ya kugombea urais Julai 30 na juzi Agosti Mosi alipozirejesha.

Hata hivyo, viongozi waandamizi wa Chadema wamesema suala la kutokuwapo kwa Dk Slaa halipaswi kukuzwa kwa kuwa ‘anafanya kazi nyingine za chama.'

Alipoulizwa jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema: "Suala la kutokuwapo Dk Slaa ni kitu cha kawaida, anafanya kazi nyingine huko, lakini pia kuna wasaidizi wake hapa ambao ni sisi manaibu. Mlikuwa mnazungumzia Mnyika naye haonekani, si huyo. Hatuwezi kuendelea kujibu ‘rumors' (uzushi) wa kwenye mitandao… nyie subirini si tupo mtaona kama yupo au la."

Mnyika atinga kikaoni

Jana, Mnyika alionekana katika viwanja vya hoteli hiyo lakini alikataa kuzungumzia kwa undani suala hizo.

"Siwezi kuzungumza chochote," alisema Mnyika na hata alipoulizwa ni lini atawaeleza Watanzania juu ya kutoonekana kwake alisisitiza mara tatu kuwa "Siwezi kuzungumza chochote."

Chama hicho kinaendelea na mfululizo wa vikao vya vyombo vya juu ambapo leo kinatarajia kutafanya kikao cha Baraza Kuu kabla ya Mkutano Mkuu kesho kumpitisha mgombea wa urais kesho.

Kura za maoni Kibamba zaahirishwa

Mchakato wa kura za maoni wa kumpata mgombea wa ubunge wa chama hicho katika Jimbo Kibamba utafanyika leo baada ya kuahirishwa juzi.

Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa kichama Kinondoni, Rose Mushi alisema kura hizo zitapigwa leo kuanzia saa nne asubuhi, Kimara Baruti. "Kila kitu kinakwenda vizuri, nadhani kesho (leo), tutafanya mchakato huu wa kura za maoni, kama kutakuwa mabadiliko nitakutaarifu," alisema Mushi.

Awali, Mratibu wa Chadema Kanda Pwani, Casmir Mabina alisema: "Jana (juzi), tulishindwa kufanya kwa sababu mmoja wa watia nia alikuwa mgonjwa. Hakupata taarifa za mchakato huo, tukatumia demokrasia ya kuahirisha."

Mwenyekiti wa Jimbo la Ubungo, Boniface Jacob alisema kura za maoni katika jimbo hilo (Kibamba) huenda zikafanyika leo baada ya kupokea taarifa kutoka kanda. "Sisi kazi yetu ni kuratibu mchakato wa kura za maoni ila maelekezo yote yanatoka juu, inawezekana ikiwa kesho (leo) jioni sina uhakika," alisema Jacob.

Juzi, hali ya sintofahamu iliwakumbuka wajumbe na watia nia wa jimbo hilo baada ya kufika kwenye ukumbi wa mikutano na kuambiwa kuwa mchakato wa kura za maoni umeahirishwa kwa madai kuwa mmoja ya watia nia hakupewa taarifa.

Hatua hiyo ilizua minong'ono miongoni wa wajumbe na watia nia ambao waliokuwa wamejiandaa kwa mchakato huo wakidai kuna hujuma zinataka kufanyika.


Chanzo: Mwananchi
 
Kamanda Mbowe mwaga tu ubuyu tujue kama dr. Slaa kakatwa au hajakatwa.
 
CONFIRMED: Dkt. Slaa bado yupo Chadema na anaendelea na majukumu yake kama kawaida,kwani muda wa kuchukua fomu hadi unaisha na kuongezwa hakuwahi kwenda kuchukua fomu na wala hakuwahi kuzuiwa kuchukua fomu kwani zinatolewa ofisini kwake.
 
Nashangaa hawa prolowasa na prombowe hawachoki kumjadili mzee slaa. Jamani jengeni chama chenu slaa hawezi kuchangamana na genge la wapiga dili.
 
Wagamba mtazushaa weeee baaadae mtatulia tu. Ooh mnyika anahama, ooh Slaa anahama. Mtaangaika mwezi huu hadi kifo chenu kitakapowakuta Oct 25!
 
Cdm wapo vzur na political game. lengo kuwachanya opponents wake.
 
CCM kama vipi mchukueni tu huyo Slaa maana inaonekana mpo upande wake sana.
Na kwasasa Slaa naye anavimba kichwa saana.
 
.....mwenyewe asema kama ni Mapenzi ya MUNGU wachaa yatimie.... !!
 

Attachments

  • 1438582355970.jpg
    1438582355970.jpg
    75.7 KB · Views: 683
Kuna propaganda chafu mno zinasambazwa juu ya Dr Slaa na kinachostua ni baadhi ya vijana wa Chadema wanashiriki kuvichochea.....fanyeni mizaha wakati mwingine si huu.....vijana tutumie akili zetu vyema.....tuna safari ndefu na taifa letu.....tusiwavunje moyo watu waliosimama nasi wakati wote mgumu.....
 
Kuna propaganda chafu mno zinasambazwa juu ya Dr Slaa na kinachostua ni baadhi ya vijana wa Chadema wanashiriki kuvichochea.....fanyeni mizaha wakati mwingine si huu.....vijana tutumie akili zetu vyema.....tuna safari ndefu na taifa letu.....tusiwavunje moyo watu waliosimama nasi wakati wote mgumu.....

Propaganda. . . . .Idara ya uenezi. . . . .Afisa habari. . . . Uchochezi. . . .Kutumia akili vyema. . . .watu waliosimama nasi wakati wote mgumu. . . . .safari ndefu na Taifa letu. . . . .


Haya labda. . . .
 
mda unatupa uwanja mpana wa kung'amua mbivu na mbichi.
Tutaendelea kujua kadri mda unavyosonga. Ni kama la Lowassa lilikuwa na sintofahamu nyingi lakini ssasa tushaeelwa which is which.
 
Kuna propaganda chafu mno zinasambazwa juu ya Dr Slaa na kinachostua ni baadhi ya vijana wa Chadema wanashiriki kuvichochea.....fanyeni mizaha wakati mwingine si huu.....vijana tutumie akili zetu vyema.....tuna safari ndefu na taifa letu.....tusiwavunje moyo watu waliosimama nasi wakati wote mgumu.....

Bravo mkuu. Tunaenda kusiko kwa ushabiki
 
Nawauliza ninyi wanasiasa ambayo kwa namna moja au nyingine mmekuwa ni sehemu ya historia katika nchi hii kwa maana hatuwezi kutaja mafanikuo au kushindwa/kukwama kutaja kwa maendeleo katika taifa hili bila ninyi kwa nafasi mlizokuwa nazo hivyo kwa uzito huyo mliokuwanao mkajaribu kuomba nafasi kugombea Urais kupitia chama tawala na kura sio kwamba hazikutosha Bali hamkupigiwa kura kabisa (mkakatwa)lakini tumeshangaa hamuongei lolote kuupongeza au kuukosoa mchakato ili kumpa nguvu aliyeteuliwa badala yenu na chama kwa ujumla,au zile tetesi kuwa mlikuwa pale kwa kushawishiwa na mchakato wenu wote wa kutia nia ni kwa ajili ya kusaidia ukatwaji wa mtu fulani uonekane "si yeye peke yake"hivi kweli waziri mkuu aliyeko madarakani hafai kuliko January,membe, migiro na amina au mwandosya aliyekuwa namba 3 hakustahili kupigiwa hata kura, viti bilali,Sumaye ,wasira,Bro mako n.k hivi wote mmetumwa tuambieni basi mchakato ulikuwa fair na mliridhika pia he machozi mliyooneshwa kutoa na vyombo fulani vya habari wakati mgombea anatangazwa yalikuwa ya furaha?vp nafasi zima Armani kwa kuwa mlitumwa so mission completed,au justice was seem to be done because th
the process was fair and free,au mnaumia moyoni lakini hamuoni haja ya kusema au mnaogopa alichosema mzee NGOMBALE"kitengo"au "useme ya moyoni ukose ugali" je tuwasahau au tusubiri mtatoa tamko .
 
Back
Top Bottom