Mbowe ni kiongozi mwenye maono ya mbali

Tuchukue nafasi kumpongeza mwenyekiti wa chadema kwa kuamua kujiondoa kwenye chaguzi ndogo za marudio japo anavaa joho la ukawa lakini tunajua ukawa haipo siku nyingi

Mbowe apongezwe hapa kwa kuamua kuepusha gharama za chama katika kampeni ,japo pesa hizo si zao ila ni faida watazitumia kwa kazi nyingine ya kujenga chama
Mbowe ni kiongozi mwenye kuona mbali baada ya kugundua hawana cha kuwaambia wananchi katika kampeni, yote wanayotaka kuyasema yameshafanywa na rais pombe magufuli kwa kutekeleza ilani ya ccm

Kama ni rushwa Takukuru inafanya kazi kweli kweli mpaka walio ndani ya ccm wanaisoma namba,sekta zote zinasimamiwa kwa ufanithi,kilichobaki labda ni kwenda kumshambulia rais kwa mambo yake binafsi na hapa ndipo wanapobanwa wakasema demkrasia inaminywa .
Sababu wanataka kusimama mpaka saa moja usiku kinyume cha sheria,wakishushwa majukwaani wahuni walioandaliwa huvamia polisi nao polisi wakitaka kuwadhibiti wahuni hao wakiwa na sare za chama hulalamika wamepigwa na dola na wanaminywa uhuru wa kuongea

Tumpongeze mbowe wametumia haki kususia ,hayo marekibisho hakuna sababu hakuna mapungufu

Na mbaya zaidi hakuna la kusema lile neno kipaumbele cha chama si ufisadi linawamaliza!

Tetemeko la kata 42 bado linawatisha!
Ujue bana uzuri ni kwamba hata wewe unajua ulichokiandika ni porojo...na umetunga tu
 
Tanzania nchi yangu kweli hawa ndio vijana tunaowategemea kuwa kuna siku watanzania watajielewa na kuwa huru. Watakaojielewa na kuwa kama wenzetu waghana wanaojua maana ya demokrasia watakaojielewa na kumfanya shangazi yangu kule kolomije aweze kupata maji safi. Ebu soma mawazo ya kijana wa Kitanzania kitu anachoandika au kuwaza. Na anatumia muda wake mwingi kuandika. Ndio niseme Tanzania itaendelea kwa vichwa kama hivi vya kondoo. Watanzania wenzangu bado tunayo safari ndefu.
YAANI HUYU KIJANA AMEKUWA NA AKILI NA MAARIFA KULIKO WEWE MZEE. NI AJABUI SANA KUNA WAZEE WA KITANZANIA WASIOJITAMBUA HATA BAADA YA ELIMU YA UPE KUTOLEWA KWAO. HII INASIKITISHA SANA. KWAHERI BABU.
 
Mbowe maamuzi yake hakuna wa kuhoji sababu anao waongoza wamelala!
Sijawahi sikia unampinga/japo hata kumuuliza anaweza kuokota vichwa vya train kisa hapo hapo waziri wake anafanya mchakato wa kuvinunua
Huu ujuha usituambukize sisi.
 
Ni Kiongozi shujaa kwa sababu anakula ruzuku mwenyewe, aliuza chama kwa Lowassa

Na

Chama

Kitafia

Mikononi

Mwake
 
Wapo wanaombeza kwa kauli yake ya kugomea chaguzi mbalimbali bila kufahamu umuhimu wa hoja na kauli yake, kwanza ningependa ifahamike uchaguzi ni gharama kwa fedha za umma au za vyama.

Tunapokuwa na tume ambayo baadhi ya pande haukubaliani nayo hapa tunasema uchaguzi utakaofanyika utawezaje kuwa huru na haki, tumeshuhudia chaguzi ndogo za udiwani jinsi zilivyokuwa na kasoro.Hakuna sababu ya kufanya chaguzi ambayo matokeo yake yanajulilana.

Heko Mh.Mbowe.
 
Kuuza chama kwa mafisadi ndio maono ya mbali
Mimi ni mwana CCM ila kiukweli jambo hili huwa linanipa kichefuchefu,Ili kukata huo mzizi wa fitina naamini huu ndio ungekuwa wakati muafaka na bora sana kumfikisha huyo fisadi au mafisadi mahakamani ili mbichi na mbivu zikapate kujulikana! MUNGU IBARIKI TZ NA WATU WAKE
 
Back
Top Bottom