Mbowe na wabunge wengine waikubali bajeti, waipongeza

Mbowe na wabunge wengine waikubali bajeti, waipongeza

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/2017 pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.

Alisema mambo matatu makubwa yakitekelezwa, itakuwa imetibu kiu ya watanzania ya muda mrefu, moja ni kupeleka fedha nyingi kwa maendeleo na kubana matumizi ya kawaida na pili imepunguza utegemezi wa wafadhili, kufadhili bajeti ya nchi. Alisema hilo ni jambo jema na kusisitiza kuwa msingi iwekwe ya kuimarisha.

“Ukomo wa bajeti ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, hili nalo katika serikali ya awamu ya tano wameliona na kweli tuwaunge mkono, sio kila kitu tuone kibaya, cha msingi tuwape nafasi tuone watamalizaje huko mbele kwenye utekelezaji”, aliongeza Mbowe.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) alisema serikali imethubutu kupanga kiwango kikubwa cha bajeti na ni vyema kuwatia moyo na kuacha tabia ya kukosoa jambo kwa hatua ya awali.

Alisema kitendo cha kuweka asilimia 40 kwenye bajeti ya maendeleo ni hatua kubwa na kwamba mpango wa serikali kurasimisha sekta isiyo rasmi, wakiwemo wafanyabiashara ndogo na wengine ambao hawakuwa wakilipa kodi, utasaidia kuongeza mapato ya kodi.

“Ni hatua kubwa sana, cha msingi ni kuhakikisha bajeti ya maendeleo ambayo imetengewa asilimia 40 ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatekelezwa, ni vyema tuwatie moyo”, alisema Zitto .

Katika mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/17, yaliyowasilishwa na Serikali, Bajeti ya Tanzania kwa mara ya kwanza, imepunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa misaada ya nje , ambapo utegemezi umebaki 12% tu tofauti na 40% ya miaka ya nyuma.

Lakini pia kiasi kikubwa cha bajeti ya mwaka ujao kitaelekezwa katika miradi ya maendeleo ambapo zaidi ya 40% ya fedha zote zitatumika katika miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema mapendekezo ya bajeti hiyo, hayana uhalisia na huenda yasitekelezeke, kwa kuwa yameegemea zaidi katika mafanikio ya muda mfupi yaliyopatikana katika ukusanyaji wa kodi na faini za wakwepa kodi.

Kuhusu ushauri wake wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya bajeti hiyo, mbunge huyo alisema “waulizeni CCM, hiyo si kazi yangu”.

Source: Habari Leo
 
Mbatia anakosoa kaulizwa nini kifanyike kuondokana na hayo mapungufu uliyoyaona anasema sio kazi yake hiyo.
 
Engineer Ni yupi ? Ngosha siyo engineer Ni mwalimu wa kemia Na hesabu. Kupitia JF mwanga unamulika pale penye giza totoro.


QUOTE="BONGOLALA, post: 15798876, member: 18850"]Huyu Engineer anamzidi maarifa sana mchumi aliyepita.Sijui degree yake ilikua ya uchumi upi[/QUOTE]
 
Unakusanya 17.8 Tril. na unatumia 17 tril. Bado kuna tatizo aisee!
 
Mbowe yuko makini sana ndiyo maana gazeti la CCM limemuweka front page na leo watauza mno.
 
Upinzani sio kupinga kila jambo hata lenye manufaa kwa nchi
 
Kwani siku zote serikali ya ccm utaiweza kwa mipango mizuri ya kwenye makaratasi!
 
Magufuli ameishasema maendeleo hayana vyama wewe wa lumumba...

Nashangaa hakuna mtu anaongelea ukusanyaji kodi kwenye nyumba za kupangisha. Una nyumba 10 za kupangisha laki tano kwa mwezi unavuta milioni tano yako kila mwezi au milioni 60 kwa mwaka TRA hawagusi hata shilingi toka kwako, mbaya zaidi umemwambia mpangaji wako nitumbukizie kwenye akaunti kabisa.... Duniani kote hii imebakia Tanzania pekee na kuna hela nyingi sana hapa wale wazee wanapiga draft tu mchana kutwa wanajua hela ya kodi ipo. Lakini pia lazima uongezwe wigo wa walipa kodi na ikibidi kodi ya kichwa irudishwe

Ni kweli property tax haikusanywi ipasavyo. Si hiyo tu hata vyanzo vya mapato ya kujenga hayo majengo hayatozwi kodi ya mapato. Ni wakati muafaka kwa za nakala valuation report za majengo zinazofanyanywa na halmashauriza wilaya miji manisipaa na majiji zipelekwe TRA ili kujua kama wenye majengo hayo wanalipa kodi ya mapato.
 
Mbunge wa Korogwe V, Profesa Maji Marefu (CCM) amesema anaipinga bajeti na ataendelea kuipinga watakapokuwa bungeni
Huyo elimu yake inamponza kwani sidhani hata kama amesoma na kuelewa hiyo bajeti. Ndiyo maana rasimu ya katiba iliweka kiwango cha chini cha elimu ya mbunge iwe shahada ya kwanza.
 
Ni kweli property tax haikusanywi ipasavyo. Si hiyo tu hata vyanzo vya mapato ya kujenga hayo majengo hayatozwi kodi ya mapato. Ni wakati muafaka kwa za nakala valuation report za majengo zinazofanyanywa na halmashauriza wilaya miji manisipaa na majiji zipelekwe TRA ili kujua kama wenye majengo hayo wanalipa kodi ya mapato.
Hawa halmashauri ni mabingwa wa kuchakachua ni bora TRA wafanye valuation wenyewe
 
Back
Top Bottom