Mbowe na wabunge wengine waikubali bajeti, waipongeza

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
BAADHI ya wabunge wamepongeza mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/17, yaliyowasilishwa na Serikali kutokana na bajeti hiyo kwa mara ya kwanza, kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa fedha za nje, lakini pia kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha katika matumizi ya maendeleo.

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.

Alisema mambo matatu makubwa yakitekelezwa, itakuwa imetibu kiu ya watanzania ya muda mrefu, moja ni kupeleka fedha nyingi kwa maendeleo na kubana matumizi ya kawaida na pili imepunguza utegemezi wa wafadhili, kufadhili bajeti ya nchi. Alisema hilo ni jambo jema na kusisitiza kuwa msingi iwekwe ya kuimarisha.

“Ukomo wa bajeti ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, hili nalo katika serikali ya awamu ya tano wameliona na kweli tuwaunge mkono, sio kila kitu tuone kibaya, cha msingi tuwape nafasi tuone watamalizaje huko mbele kwenye utekelezaji”, aliongeza Mbowe.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) alisema serikali imethubutu kupanga kiwango kikubwa cha bajeti na ni vyema kuwatia moyo na kuacha tabia ya kukosoa jambo kwa hatua ya awali.

Alisema kitendo cha kuweka asilimia 40 kwenye bajeti ya maendeleo ni hatua kubwa na kwamba mpango wa serikali kurasimisha sekta isiyo rasmi, wakiwemo wafanyabiashara ndogo na wengine ambao hawakuwa wakilipa kodi, utasaidia kuongeza mapato ya kodi.

“Ni hatua kubwa sana, cha msingi ni kuhakikisha bajeti ya maendeleo ambayo imetengewa asilimia 40 ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatekelezwa, ni vyema tuwatie moyo”, alisema Zitto .

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), alisema mapendekezo hayo yametoa mwanga na unafuu kwa watanzania kwa kuwa kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17, ambao umegusa maeneo mengi nyeti yanayowagusa wananchi.

“Ni bajeti nzuri, kwa kweli imezingatia zaidi matakwa ya wananchi hasa katika eneo la matumizi ya maendeleo. Si kwamba bajeti za nyuma zilikuwa mbaya. La hasha. Lakini kutokana na utegemezi mkubwa wa fedha za nje, zilionekana kuwa hazitekelezeki,” alisema Ngeleja.

Kwa upande wa Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (CCM) alisema mapendekezo hayo, yametoa matumaini na mwanga mpya kwa watanzania, kwani kwa mara ya kwanza Serikali inaonyesha nia ya dhati ya kuachana na utegemezi.

“Bajeti imeweka wazi utegemezi wa wahisani uko asilimia 12 tu ya bajeti yote, miradi mingi ilikuwa haitekelezeki au kumaliza kutokana na wahisani wengi kutotimiza ahadi zao, lakini sasa Serikali imeamua kujikita katika ukusanyaji wa mapato yake na kutegemea zaidi fedha za ndani,” alisisitiza Mapunda.

Mbunge huyo alipongeza hatua za Serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha matumizi yote ya fedha za Serikali yanafuatiliwa, ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa kuhakiki matumizi na mapato yake kila mwezi ili kuona kama yanawiana.

Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM) alisema kwa sasa yapo matumaini ya miradi ya maendeleo kukamilika kutokana na bajeti nzima kujikita katika fedha za ndani, kwani kiasi kinachotarajiwa kutoka kwa wahisani, hata kisipotolewa, upo uwezekano wa fedha hizo kupatikana kupitia mapato ya ndani.

“Hata hao wahisani mara nyingi wamekuwa wakitoa ahadi, lakini utekelezaji wao unaambatana na masharti mengine ambayo hayana hata msingi. Na upatikanaji wa hela yao umekuwa mgumu. Sio hata hizi Shilingi trilioni tatu hata wasipoleta tuna uwezo wa kuzikusanya kutoka humu ndani,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Mimi naunga mkono jitihada za serikali ambazo zimefanya na kutuondoa katika utegemezi wa misaada sana. Mimi naamini kuwa nchi yetu ni tajiri ina vitu vingi sana, ambavyo vinaweza kutufikisha mahala tukajitegemea”.

Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema mapendekezo ya bajeti hiyo, hayana uhalisia na huenda yasitekelezeke, kwa kuwa yameegemea zaidi katika mafanikio ya muda mfupi yaliyopatikana katika ukusanyaji wa kodi na faini za wakwepa kodi.

Kuhusu ushauri wake wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya bajeti hiyo, mbunge huyo alisema “waulizeni CCM, hiyo si kazi yangu”.

Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) alisema baada ya kumaliza habari ya faini za kodi na wale waliokwepa kulipa kodi, makusanyo yatashuka kwa kiasi kikubwa. Alishauri kuibuliwa kwa maeneo mengi, yaliyotekelezwa yanayoweza kulipishwa kodi, ikiwemo eneo la bahari ambalo kwa mujibu wake kwa sasa limegeuzwa kama shamba la bibi.

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM), alisema mpango na mapendekezo ya bajeti ni mzuri, kwa kuwa vitu vingi vimelenga mahitaji ya wananchi na sasa kiu ni kuona utekelezaji wake.

Chanzo: Habari Leo
 
Mbunge wa Korogwe V, Profesa Maji Marefu (CCM) amesema anaipinga bajeti na ataendelea kuipinga watakapokuwa bungeni
 
Kama ni kweli wamepongeza basi ni maajabu ya Musa, hawa wazee wa kuponda wakopongeza inatakiwa ujiulize kulikoni!
 
Magufuli ameishasema maendeleo hayana vyama wewe wa lumumba...

Nashangaa hakuna mtu anaongelea ukusanyaji kodi kwenye nyumba za kupangisha. Una nyumba 10 za kupangisha laki tano kwa mwezi unavuta milioni tano yako kila mwezi au milioni 60 kwa mwaka TRA hawagusi hata shilingi toka kwako, mbaya zaidi umemwambia mpangaji wako nitumbukizie kwenye akaunti kabisa.... Duniani kote hii imebakia Tanzania pekee na kuna hela nyingi sana hapa wale wazee wanapiga draft tu mchana kutwa wanajua hela ya kodi ipo. Lakini pia lazima uongezwe wigo wa walipa kodi na ikibidi kodi ya kichwa irudishwe
 
20160407_0733460.jpg

Muda si mrefu Mbowe atakiri kuwa Magufuli ni bora kuliko Lowassa ha ha haaaaa,
 
Bajeti zilizopita zilikuwa hazitekelezwi kwani hela zilizotengwa hazikupatikana ama kwa wakati au kutopatikana kabisa.Sasa mwaka huu tumeongeza bajeti kwa kiasi kikubwa, na wakati huo huo tumepunguza utegemezi na pia kuna fedha za misaada tumezikosa.Sasa kwa hali hii,bajeti hii itatekelezeka kweli?Mabadiliko haya ndani ya mwaka mmoja tu yatawezekana kweli?

Tuache kuandaa bajeti za kisiasa kufurahisha watu tuende na reality huku tukifanya mabadiliko hatua hatua na sio kutoa matumaini makubwa kwa wananchi huku mkitarajia kutekeleza mabadiliko hayo makubwa just overnight kitu ambacho si rahisi.

Kama umeongeza vyanzo vipya vya mapato huwezi kujiamini sana maana ndio kwanza utakuwa unaanza kuvitumia na bila shaka vitakuwa na changamoto zake na utakuwa huna uzoefu wake katika kukusanya mapato kutoka katika vyanzo hivyo vipya hivyo si busara kuweka matumaini makubwa katika eneo la kodi ambalo huna uzoefu nalo na ambalo hata data zake za makusanyo ni kama ziko kwenye majaribio kwani unaweza kukusanya tofauti na ulivyotarajia.

Mtakaonibishia mjiulize kwanza ni nini kimetokea kwenye swala la elimu bure ambalo nalo lilifanywa kisiasa zaidi pasipo kuzingatia reality.

Tusubiri.
 
Upinzani sio kupinga kila kitu wala kujenga uhasama, nampongeza Mbowe kwakuwa mkweli tofauti na Mchungaji
 
Siku zote sera ya upinzani ni kuhakikisha tunajitegemea na kuacha kukopa na kuomba, na hii ndio heshima ya nchi inapokuja. sio kuzurura ulimwengu mzima kutembeza bakuli kisa eti hao wanahela nyingi sana, khaa si zao na wewe tafuta zako, JK hakuwa na washauri wazuri.
 
Kama ni kweli wamepongeza basi ni maajabu ya Musa, hawa wazee wa kuponda wakopongeza inatakiwa ujiulize kulikoni!

Umekariri kama amabavyo wangejiandaa kulazimisha safi hautakiw kutabilika.
 
BAADHI ya wabunge wamepongeza mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/17, yaliyowasilishwa na Serikali kutokana na bajeti hiyo kwa mara ya kwanza, kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa fedha za nje, lakini pia kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha katika matumizi ya maendeleo.

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.

Alisema mambo matatu makubwa yakitekelezwa, itakuwa imetibu kiu ya watanzania ya muda mrefu, moja ni kupeleka fedha nyingi kwa maendeleo na kubana matumizi ya kawaida na pili imepunguza utegemezi wa wafadhili, kufadhili bajeti ya nchi. Alisema hilo ni jambo jema na kusisitiza kuwa msingi iwekwe ya kuimarisha.

“Ukomo wa bajeti ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, hili nalo katika serikali ya awamu ya tano wameliona na kweli tuwaunge mkono, sio kila kitu tuone kibaya, cha msingi tuwape nafasi tuone watamalizaje huko mbele kwenye utekelezaji”, aliongeza Mbowe.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) alisema serikali imethubutu kupanga kiwango kikubwa cha bajeti na ni vyema kuwatia moyo na kuacha tabia ya kukosoa jambo kwa hatua ya awali.

Alisema kitendo cha kuweka asilimia 40 kwenye bajeti ya maendeleo ni hatua kubwa na kwamba mpango wa serikali kurasimisha sekta isiyo rasmi, wakiwemo wafanyabiashara ndogo na wengine ambao hawakuwa wakilipa kodi, utasaidia kuongeza mapato ya kodi.

“Ni hatua kubwa sana, cha msingi ni kuhakikisha bajeti ya maendeleo ambayo imetengewa asilimia 40 ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatekelezwa, ni vyema tuwatie moyo”, alisema Zitto .

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), alisema mapendekezo hayo yametoa mwanga na unafuu kwa watanzania kwa kuwa kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17, ambao umegusa maeneo mengi nyeti yanayowagusa wananchi.

“Ni bajeti nzuri, kwa kweli imezingatia zaidi matakwa ya wananchi hasa katika eneo la matumizi ya maendeleo. Si kwamba bajeti za nyuma zilikuwa mbaya. La hasha. Lakini kutokana na utegemezi mkubwa wa fedha za nje, zilionekana kuwa hazitekelezeki,” alisema Ngeleja.

Kwa upande wa Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (CCM) alisema mapendekezo hayo, yametoa matumaini na mwanga mpya kwa watanzania, kwani kwa mara ya kwanza Serikali inaonyesha nia ya dhati ya kuachana na utegemezi.

“Bajeti imeweka wazi utegemezi wa wahisani uko asilimia 12 tu ya bajeti yote, miradi mingi ilikuwa haitekelezeki au kumaliza kutokana na wahisani wengi kutotimiza ahadi zao, lakini sasa Serikali imeamua kujikita katika ukusanyaji wa mapato yake na kutegemea zaidi fedha za ndani,” alisisitiza Mapunda.

Mbunge huyo alipongeza hatua za Serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha matumizi yote ya fedha za Serikali yanafuatiliwa, ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa kuhakiki matumizi na mapato yake kila mwezi ili kuona kama yanawiana.

Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM) alisema kwa sasa yapo matumaini ya miradi ya maendeleo kukamilika kutokana na bajeti nzima kujikita katika fedha za ndani, kwani kiasi kinachotarajiwa kutoka kwa wahisani, hata kisipotolewa, upo uwezekano wa fedha hizo kupatikana kupitia mapato ya ndani.

“Hata hao wahisani mara nyingi wamekuwa wakitoa ahadi, lakini utekelezaji wao unaambatana na masharti mengine ambayo hayana hata msingi. Na upatikanaji wa hela yao umekuwa mgumu. Sio hata hizi Shilingi trilioni tatu hata wasipoleta tuna uwezo wa kuzikusanya kutoka humu ndani,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Mimi naunga mkono jitihada za serikali ambazo zimefanya na kutuondoa katika utegemezi wa misaada sana. Mimi naamini kuwa nchi yetu ni tajiri ina vitu vingi sana, ambavyo vinaweza kutufikisha mahala tukajitegemea”.

Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema mapendekezo ya bajeti hiyo, hayana uhalisia na huenda yasitekelezeke, kwa kuwa yameegemea zaidi katika mafanikio ya muda mfupi yaliyopatikana katika ukusanyaji wa kodi na faini za wakwepa kodi.

Kuhusu ushauri wake wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya bajeti hiyo, mbunge huyo alisema “waulizeni CCM, hiyo si kazi yangu”.

Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) alisema baada ya kumaliza habari ya faini za kodi na wale waliokwepa kulipa kodi, makusanyo yatashuka kwa kiasi kikubwa. Alishauri kuibuliwa kwa maeneo mengi, yaliyotekelezwa yanayoweza kulipishwa kodi, ikiwemo eneo la bahari ambalo kwa mujibu wake kwa sasa limegeuzwa kama shamba la bibi.

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM), alisema mpango na mapendekezo ya bajeti ni mzuri, kwa kuwa vitu vingi vimelenga mahitaji ya wananchi na sasa kiu ni kuona utekelezaji wake.

Chanzo: Habari Leo
Wameisoma namba hao, mi bado nakomaa, ukata mtupu!
 
Hapa ndipo uzito wa upinzani unapodhihirika. Mbunge machachari wa upinzani akiweka tick kwenye mpango/pendekezo la serikali ni sherehe na habari kubwa (front page news). Kama vile wabunge wa chama tawala wapo wapo tu.
 
Hizi ni hatua za awali mimi naona sio vibaya wabunge wa upinzani kupongeza hatua hii kwakuwa bajeti inatekelezeka kutokana ikusanyaji wa kodi hasa waliokwepa hapo nyuma.

Suala la msingi sana ni kwamba je hivi vyanzo vya mapato vitatosheleza
mahitaji muhimu kwa baadae na pia bajeti zinazokuja kwakuwa katika bajeti ya sasa vyanzo vingi vya mapato vimetokana na wakwepa kodi nimewaelewa vizuri wabunge wa upinzani ila wabunge wa Ccm hawalizungumzii hili suala la msingi.
 
Magufuli ameishasema maendeleo hayana vyama wewe wa lumumba...

Nashangaa hakuna mtu anaongelea ukusanyaji kodi kwenye nyumba za kupangisha. Una nyumba 10 za kupangisha laki tano kwa mwezi unavuta milioni tano yako kila mwezi au milioni 60 kwa mwaka TRA hawagusi hata shilingi toka kwako, mbaya zaidi umemwambia mpangaji wako nitumbukizie kwenye akaunti kabisa.... Duniani kote hii imebakia Tanzania pekee na kuna hela nyingi sana hapa wale wazee wanapiga draft tu mchana kutwa wanajua hela ya kodi ipo. Lakini pia lazima uongezwe wigo wa walipa kodi na ikibidi kodi ya kichwa irudishwe
Hilo limesha zungumzwa na lipo katika mchakato wa kulifanikisha... wenye nyumba na wale wanapangisha frames za biashara wataanza kulipa kodi..!
 
“Ni hatua kubwa sana, cha msingi ni kuhakikisha bajeti ya maendeleo ambayo imetengewa asilimia 40 ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatekelezwa, ni vyema tuwatie moyo”, alisema Zitto .

Mhe. Zito pamoja na kuwatia moyo bado wangeweza kufanya zaidi ya hapo!
Bado bajeti ya matumizi ya kawaida ni kubwa kuliko uwezo wa ukusanyanji!

Tukusanye 17.8 alafu matumizi ya kawaida yawe 17 hatuwezi kusogea mbele na kupiga hatua ya maendeleo!
 
Bajeti zilizopita zilikuwa hazitekelezwi kwani hela zilizotengwa hazikupatikana ama kwa wakati au kutopatikana kabisa.Sasa mwaka huu tumeongeza bajeti kwa kiasi kikubwa, na wakati huo huo tumepunguza utegemezi na pia kuna fedha za misaada tumezikosa.Sasa kwa hali hii,bajeti hii itatekelezeka kweli?Mabadiliko haya ndani ya mwaka mmoja tu yatawezekana kweli?

Tuache kuandaa bajeti za kisiasa kufurahisha watu tuende na reality huku tukifanya mabadiliko hatua hatua na sio kutoa matumaini makubwa kwa wananchi huku mkitarajia kutekeleza mabadiliko hayo makubwa just overnight kitu ambacho si rahisi.

Kama umeongeza vyanzo vipya vya mapato huwezi kujiamini sana maana ndio kwanza utakuwa unaanza kuvitumia na bila shaka vitakuwa na changamoto zake na utakuwa huna uzoefu wake katika kukusanya mapato kutoka katika vyanzo hivyo vipya hivyo si busara kuweka matumaini makubwa katika eneo la kodi ambalo huna uzoefu nalo na ambalo hata data zake za makusanyo ni kama ziko kwenye majaribio kwani unaweza kukusanya tofauti na ulivyotarajia.

Mtakaonibishia mjiulize kwanza ni nini kimetokea kwenye swala la elimu bure ambalo nalo lilifanywa kisiasa zaidi pasipo kuzingatia reality.

Tusubiri.
Una uhakika gani kwamba hawana uzoefu katika ukusanyaji kodi sehemu hizo....!?

Usimamizi mzuri wa ukusanyaji kodi utaleta pesa nzuri... sio kwamba baada ya mwaka huu biashara zitaisha... ni zitaendelea tena kwa ubora kwani kila mtu atafanya kazi kiUeledi ili kupata faida...

Hizo pesa za maendeleo zinaenda kujenga vitu vya kimaendeleo ambavyo vitaajiri watu watakaolipwa na kufanya kazi..

Em toa mawazo yako nini kifanyike baada ya kuona mapungufu hayo...!?
 
Mambo ndio hayo
Sio kila jambo kupinga hata kama huna hoja ya maana

Tuijenge TANZANIA mpya
 
Dalili za Upinzani nchini hakika zinaanza kuonyeshaya kuwa Viongozi wa Upinzani kifikra wanaendana na Uongozi wa Awamu ya Tano.Niwaombe wasione haya kutoa mawazo mema yatayoisaidia Serikali kuwatumikia Wananchi wake wote bila ya kufuata Uchama na Wabunge wajitambue wao ni wakilishi wa wananchi wote Vyama ni Madaraja waliyopitia kufika Mjengoni lengo ni kuwatumikia Wananchi na Nchi.Hapa wasilete CCM mshindi ama UKAWA mshindi lengo ni MAENDELEO YA NCHI NA WANANCHI
 
Back
Top Bottom