Mbowe na Sugu wanatumia pesa zao gani kupeleka maendeleo majimboni kwao?

Dunamist

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
474
682
Amani iwe kwenu wakuu!

Jana tar. 13 sept. kwenye gazeti la Mwananchi la mtandaoni kulikuwa na habari yenye kichwa kilichosomeka "WAITARA ADAI AMEKATAA KUWA KENGE CHADEMA"

Mwananchi ilimnukuu mgombea ubunge wa CCM jimboni Ukonga akisema "Mbowe jimboni kwake Hai kuna umeme hadi migombani, Mbeya mjini halikadhalika, ila mimi nikitaka kuonana na waziri husika kwa ajili ya maendeleo jimboni kwangu nakatazwa''.

Waitara aliendelea kusema kuwa CDM ni msafara wa mamba, hivyo yeye amekataa kuwa kenge.

Swali langu ni;

-Mbowe na Sugu wanatumia pesa gani kupeleka maendeleo majimboni kwao, kama hawaruhusiwi kuonana na mawaziri husika?

-Je! Mbowe na Sugu wanaonana na mawaziri kimya kimya ila wanawakataza wabunge wengine wa CDM kufanya hivyo?
 
Kweli siasa ni mchezo wa kijinga sana na wajinga tu ndio wanao amini, Mbeya ni jiji, sasa ulitaka jiji lisiwe na umeme!? By the way, Mbeya ina umeme nadhani since when Sugu hata hajazaliwa, Sugu anaweza kua kafanya jambo linguine jiji Mbeya lakini sio la UMEME. NAdhani siku, Watanzania tukiwa werevu, wana siasa wa namna hi ya kina Waitara itabidi tu, watafute kazi nyingine, maanake kutakua hakuna mtu wa kumdanganya UONGO wa kijinga kama hu. But all in all, huyu atakua Mkurya academia, sio Mkurya original.
 
Amani iwe kwenu wakuu!

Jana tar. 13 sept. kwenye gazeti la Mwananchi la mtandaoni kulikuwa na habari yenye kichwa kilichosomeka "WAITARA ADAI AMEKATAA KUWA KENGE CHADEMA"
Mwananchi ilimnukuu mgombea ubunge wa CCM jimboni Ukonga akisema "Mbowe jimboni kwake Hai kuna umeme hadi migombani, Mbeya mjini halikadhalika, ila mimi nikitaka kuonana na waziri husika kwa ajili ya maendeleo jimboni kwangu nakatazwa''.
Waitara aliendelea kusema kuwa CDM ni msafara wa mamba, hivyo yeye amekataa kuwa kenge.
Swali langu ni
-Mbowe na Sugu wanatumia pesa gani kupeleka maendeleo majimboni kwao, kama hawaruhusiwi kuonana na mawaziri husika?
-Je! Mbowe na Sugu wanaonana na mawaziri kimya kimya ila wanawakataza wabunge wengine wa CDM kufanya hivyo?
Mimi nipo jimbo la Hai. Linaongozwa na Mbowe. Huo umeme hadi migombani Mbowe ameukuta.
Labda tusaidie ni maendeleo gani M/kiti wenu wa maisha ameyaleta?

Binafsi namkubali Mbowe,kwa jambo moja tuu..
Hajawah kuleta vurugu wala maandamano Hai. Hataki kuharibu chochote home . Kama alivyowahamasisha sehemu nyingine
 
Mkuu acha majungu weka orodha ya wabunge wote ukionyesha kila Mbunge anavyotumia fedha kuleta maendeleo ktk Jimbo lake kushindwa kufanya hivyo acha chuki binafsi
 
Soma kwanza uelewe ndo u-comment. Aliyeyasema hayo ni mgombea wa CCM,sio Mbowe wala Sugu
 
Aliyesema hayo ni Waitara, mgombea wa CCM Ukonga, nafikiri data atakuwa nazo yeye. Mimi nmeleta Uzi kama swali fikirishi.
 
Soma kwanza uelewe ndo u-comment. Aliyeyasema hayo ni mgombea wa CCM,sio Mbowe wala Sugu
Bila shaka wewe ndio hujamuelewa Waitara. Yeye kasema majimbo hayo mawili yana maendeleo. Lakini hakusema Sugu na Mbowe ndio walioyaleta.
Rejea swali lililoulizwa na alichokisema Waitara uone nani hajaelewa
 
waitara ni moja ya wanaume wenye tabia za kike kike kawaida mume au mke ukisha achana nae hauna sababu ya kumsema hovyo huko ulipo , hajifunzi kwa zitto alikaa kimya na hao ndio walioijenga chadema kwa jasho na damu.
 
Bila shaka wewe ndio hujamuelewa Waitara. Yeye kasema majimbo hayo mawili yana maendeleo. Lakini hakusema Sugu na Mbowe ndio walioyaleta.
Rejea swali lililoulizwa na alichokisema Waitara uone nani hajaelewa
Mwambieni apunguze obsession zake kwa Mbowe na Sugu sasa.
 
Mimi nipo jimbo la Hai. Linaongozwa na Mbowe. Huo umeme hadi migombani Mbowe ameukuta.
Labda tusaidie ni maendeleo gani M/kiti wenu wa maisha ameyaleta?

Binafsi namkubali Mbowe,kwa jambo moja tuu..
Hajawah kuleta vurugu wala maandamano Hai. Hataki kuharibu chochote home . Kama alivyowahamasisha sehemu nyingine
Watu mnajua kusoma tu ila kuelewa mlichosoma hapo ndio zoezi lilipo.
Soma tena uelewe kabla hujajibu kitu utaonekana na wewe una GPA ya 32.
 
Back
Top Bottom