Mbowe na Maalim Seif wafanya kituko kingine cha kisiasa hadharani!

Mabandiko yako yote ni ya kumpinga mtu, unaondoa maana ya great thinkers iliyofahamika kwa wadau wa Jamiiforums na Jukwaa zake.
 
Wewe mwenye maswali ya kikubwa ungetuwekea swali la kikubwa hapa kuhusu uchumi unavyodidimia ili upimwe na wanazuoni hapa kama wewe ni zaidi ya mbowe au la?
 
Natoka nje ya mada...Kwa sababu unawapenda ulio wataja sana,ungepnda kupata mtoto wa nani,yani kuzalishwa na mbowe,kingunge,lowassa au mnyika...
mawazo binafsi.
 
Jamaa mmoja alijiuzuru ghafla karudi chamani anataka vyeo vyake, wenyewe walipomshitukia wakamweka benchi sasa kila siku anajadili seifu kwenye vyombo vya habari,
badala ya kusema why alitoka sasa anarudi kimemurudisha nini,?
yeye anajadili watu wakimbana kuhusu katiba ya chama anaruka tena kumjadili mbowe ati anataka kuua chama chao.

Sasa mbowe akaja nayake kwamba bwana profesa abebe tuu msalaba wake wa usaliti maana huwezi kuwa profesa afu unatumika kijinga namna hii!!

Namimi nasema bebeni tuu msalaba wenu wanachama chakavu wa chama cha majambazi hamuwezi kuiba urais kimiujizaujiza hivi kana kwamba Hamna akili afu mnapongezana kwa ushindi wa kishindo, bebeni msalaba mpaka mwisho uwafie mgongoni.
 
Mturuhusu na sie basi kumuandika mtukufu kama ninyi nanyi mnavyowaandika na kuwaita majina viongozi wa upinzani, bila ya kubughudhiwa..
 
Jadili hoja....usiwe unapanik kwa mambo madogo.
Kunahoja Hapo? Mitoka Ukabila, Udini na Sasa Uchawi, mtaendelea na Lipi? Haya yote si hoja, na lazima muisome namba yenu.
Japo ni ukweli kuwa Mbowe si kiongozi mwenye maono lakini nampongeza jinsi anavyoweza kuwarubuni akina Prof.Baregu na wafuasi wa CHADEMA bila hata ya kumhoji. Niliwahi kubadili kauli na kusema Mbowe awe kiongozi wa kudumu CHADEMA na asisumbuliwe kwani amehodhi ufahamu wao. Kwa haya yanayoendelea lazima kuna nguvu za giza zinazohusisha mazingaombwe na ramli za hali ya juu.

Linapokuja suala la UKAWA si suala la chama cha siasa kama mwasisi wa umoja huo Prof.Lipumba alivyotaka liwe..bali alimaanisha ni vuguvugu la kudai maslahi ya wanachi kwenye katiba pendekezwa...sasa inashangaza kuona dhana ya kudai maoni ya wananchi inafifishwa na dhana ukawa kutwaa dola kama chama...Tumepotoka.

Jana usiku picha zinazagaa mitandaoni zikiwanadi wanaoijiita ''vinara wa ukawa''...wakiwemo Lowassa na Kingunge...hapa ndipo ninapopatwa na wasiwasi na 'makamanda'...kuwa hivi Kigunge na Lowassa ndio wenye kubeba dhana ya UKAWA?...hadi kupuuza wenye maono ya UKAWA akina Prof.Lipumba na Dr.Slaa kiasi cha kuwaita wasaliti?. Angalau kwenye Picha ile angekuwepo Mtatiro sababu alipata kuwa katibu wa UKAWA....ni dhahiri siasa za upinzani sasa zinatawaliwa na nguvu za giza katika kutengeneza mvuto.

Sitashangaa kwani Kingunge alikuwa mshauri wa siasa wa Raisi Kikwete na ni mlezi wa 'wanamazingaombwe'...na alitumia kipaji chake kwa kushirikiana na Lowassa na Marehemu Sheikh Yahya Husein.... kupiga ramli eti atakayechukua fomu kuchuana na JK 2010 ndani ya CCM angekufa yeye na kizazi chake!...labda hili ndilo limehamia CHADEMA,CUF baada ya CCM kuachana na ujinga huo ambao kimsingi ulitaka kukiuwa chama.....
Lowassa_press2.jpg

Kwa hoja hii ndio maana wameshiriki wazee na Mtatiro (Mwenyekiti wa CUF) katengwa kwani anaweza kuropoka mbele za watu,bado hajakomaa...na wahudhuriaji wakuu ni Lowassa,Mbowe,Seif,Kingunge na Prof.Baregu......hili la Prof.Baregu kushiriki miujiza hii limenishangaza...kwani huyu ni mbobezi wa sayansi ya siasa...!Amekwisha!

Wakati umefika Mbowe pia aanzishe chuo cha kufundisha ujasiriasiasa..yaani jinsi ya kutengeneza pesa kwa kutumia siasa na pia atoe na taaluma ambayo kwa kiasi kikubwa ni adimu ya mazingaombe na ramli zinazotengeneza 'misukule' wa kisiasa.Maanake jinsi anavowachezea wafuasi wake ni dhahiri amewadharau kupitiliza akiamini hawawezi kutambua ayafanyayo

Mbowe baada ya kuuliza swali la kitoto kuhusu deni la taifa bungeni siku ya alhamisi...baada ya aibu usiku huo akaamua kuja Dar ili kupiga picha na Kingunge na Lowassa na kuwaambia wanahabari kuwa hao wanamazingambwe ni vinara wa UKAWA?

Ninamalizia tu kwa kukupongeza Mbowe kwa jinsi ulivyoweza kushika ufahamu wa wana-CHADEMA..endelea hivyo hivyo..tengeneza hela kwani wakati ni ukuta.

Nawasilisha.
 
Umeshamaliza kazi yako kachukue buku 7 huko lumumba usife njaa bure naona unahangaika sana na mambo ya Mbowe yanakusu nini?
Mbowe ni public figure...mnapaniki kama mume wenu hamtaki kushea. Jadili kwa hoja na sio viroja.
 
Kweli wewe Wakudadavu
 
Hoja ya uchawi katika siasa ni hoja ya kupooza,coz siasa na uchawi bongo ni kama kiu na maji,sio tu bongo ata nchi zilizoendelea.
 
Uzuri wa ujumbe huo upo wazi...nimewaonyesha mchawi wenu,'niwewashika sikio' ...kazi kwenu
Ni lini uliwahi kutoa onyo kwa Chama chako CCM kuwa waachane na siasa za mazingaombwe na Ramli ulizodai zilikuwa zikiongozwa na Kingunge Lowassa na Sheikh Yahaya? Au hayo umeyaona baada ya Kingunge na Lowasa Kwenda Upinzani?

Narudi kwenye Hoja yako, Hakuna dhana iliyobadilika ila kwakuwa huwa nyie hamnaga akili za kupambanua mambo basi ndio maana kila kitu huwa hamuelewi kirahisi. Kwamfano ukiwa na vita na Kundi la Wapiganaji, ukifanikiwa kuwashawishi viongozi wa wale wapiganaji na baadhi wakahamia upande wako na kukuunga mkono kuwapiga wale wapiganajia huo Tunaita ni Ushindi japo bado vita inaendelea. Hiyo ndio sababu ya kuona Lowassa na Kingunge wakiwekwa hadharani katika NIA ya UKAWA (wameachana na genge la ccm na wamewaunga mkono wananchi)

USHAURI: Siku nyingine ukifikiria kuandika propaganda ni bora ukamkodi hata mtu mwenye angalau ELIMU kidogo juu ya uandishi ili akusaidie kukushauri jinsi ya kutengeneza hoja inayoleta mvuto ndani ya dhana ficho ili uweze kuwashika wasomaji wako kwani kwa staili uliyotumia ni vigumu kwa Msomaji mwenye haraka au asie na uzoefu na vihoja vya wa Lumumba kuendelea kusoma na kumaliza ujumbe wako mpaka mwisho maana unaboa na kupangika kama INSHA liyoandika mwanafunzi
 
Back
Top Bottom