Mbowe na hadithi ya Chura!

Mbowe na hadithi ya Chura!

Vp mo kapatikana.hyo ya mbowe na hamahama bdo slow slow kashasema mwisho desemba wawahi.
Nyinyi na mbowe, sisi na nchi!
Mwambieni yule mwenyekiti kichaa wa chama cha makinikia aache kutumia nguvu za dola kupambana na fikra kinzani
Kama wewe na wenzio huko mliko sio mandondocha chukueni fomu za kagombea ubunge kule ukelewe! Kabla ya kuja kwa Mbowe anza na mtakatifu Yohana anayeendesha nchi na chama chenu kama mali yake binafsi!
Ninyi wanaCHADEMA, mlijadili suala la hamahama ndani ya chama kwa jicho pevu. Majibu rahisi hayo na shutuma hizo kwa upande wa pili hayatakitakijenga chama.

Na isitoshe mnaonesha jinsi upeo wenu wa kuchambua masuala ya kisiasa ulivyo. Mnaona uovu lakini mnakuwa vipofu. Mnasikia mambo ya hovyo mnajifanya hamna masikio.

Jamii inachoshwa na kilio cha viongozi wa chama kudai ati hakuna demokrasia, Katiba inavunjwa, au kura zinaibiwa, wakati majukwaani hawanadi Sera zaidi ya vilio hivyo.

Watanzania wanahitaji vyama vya siasa vinavyoongozwa na viongozi walioiva kisiasa. Viongozi walio na uwezo na upeo wa juu kuchambua na kuzieleza, kwa ufasaha, Sera na Itakadi za vyama vyao kwa wapiga kura. Viongozi ambao hawatoi majibu mepesi kwa maswali magumu.

Jamii inataka kusikia na kuona kwa vitendo Sera na Mikakati mbadala ya kuiendeleza nchi hii kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia.
 
. Uelewa wa watanzania wengi juu ya vyama vingi ni mdogo sana, Hivi vyama ni vya umma mimi na wewe, iweje alie? Kwani ni biashara?. Kuna hasara kubwa kutokuwa na vyama imara vya upinzani. Kwani waliohama ni wanachama au mwakilishi!. Ati Mbowe alie kwa kipi cha ajabu wakati ni siasa haramu, hakuna natura death hapo. Poor mind.
Kutokuwa imara, nadhani ndiko kunakowafanya wabunge kuhamia chama imara! Jitafakarini sana kwani bila hivyo mnadhoofisha chama ambacho kimsingi kilikuwa na watu waliokuwa wanakosoa kwa hoja na sio kwa matusi.
 
Ninyi wanaCHADEMA, mlijadili suala la hamahama ndani ya chama kwa jicho pevu. Majibu rahisi hayo na shutuma hizo kwa upande wa pili hayatakitakijenga chama.

Na isitoshe mnaonesha jinsi upeo wenu wa kuchambua masuala ya kisiasa ulivyo. Mnaona uovu lakini mnakuwa vipofu. Mnasikia mambo ya hovyo mnajifanya hamna masikio.

Jamii inachoshwa na kilio cha viongozi wa chama kudai ati hakuna demokrasia, Katiba inavunjwa, au kura zinaibiwa, wakati majukwaani hawanadi Sera zaidi ya vilio hivyo.

Watanzania wanahitaji vyama vya siasa vinavyoongozwa na viongozi walioiva kisiasa. Viongozi walio na uwezo na upeo wa juu kuchambua na kuzieleza, kwa ufasaha, Sera na Itakadi za vyama vyao kwa wapiga kura. Viongozi ambao hawatoi majibu mepesi kwa maswali magumu.

Jamii inataka kusikia na kuona kwa vitendo Sera na Mikakati mbadala ya kuiendeleza nchi hii kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia.
We mgeni nchii hayo unayosema yafanyikaje wakati ni marufuku kufanya siasa
 
Mbowe angekuwa Raisi tungekuwa tunakula bata tu Daaaaaah Mungu huyu.

Kama wewe na wenzio huko mliko sio mandondocha chukueni fomu za kagombea ubunge kule ukelewe! Kabla ya kuja kwa Mbowe anza na mtakatifu Yohana anayeendesha nchi na chama chenu kama mali yake binafsi!
 
Wahenga wanasema kwamba Chura ukimuweka kwenye maji ya moto huruka mara moja na kutoka lkn ukimuweka kwenye maji ya uvuguvugu na atakaa, na ukiongeza joto la maji kidogo kidogo Chura atasikia raha na kuendelea kubakia kwenye maji huku akifurahia joto, ukiendelea kuongeza joto la maji na maji kuanza kuchemka Chura atakuja kushtuka kwamba anapaswa kuruka lkn anakuwa ameshachelewa na maji kumpika na kumuua.

Mbowe sasa hivi ni Chura ambaye yuko kwenye yanayongezeka joto pole pole huku akisikia raha, badala ya kuruka kungali mapema.

Kama kila mtu anakutaja wewe ni tatizo lkn hausikii na unang’ang’ania, una tofauti gani na Chura?
Mbowe ni Mwiba sana kwa SISIEMU,mnafanya kila propaganda kwa mbowe,sasa kama anaibomoa chadema si ndio furaha kwenu? why mnatapatapa?
 
Kila mtu ? Eti ma lumumba ndio kila mtu. Waachie CDM yaliyo ya CDM. ACHENI unafiki. Hangaikeni na mwenyekiti wenu. Kwenu huko mmekabwa hakuna ruhusa hata kushauri, ukikohoa tu Shangazi yako ndio atadhurika.
Kuna watanzania 28000 wanamtegemea kwa ajira!
Na ajira zilivyo ngumu awamu hii,acha tu!
Mbona mlisahau jimbo lenu ambalo lilipoteza nguvu kazi zaidi ya 200000 katika ajali ya kutumbukia kwa kivuko cha MV Nyerere, Ziwa Victoria, na Mbuge wenu akibaki mkiwa.

Toeni kibanzi jichoni kwenu kwanza
 
We mgeni nchii hayo unayosema yafanyikaje wakati ni marufuku kufanya siasa
Mnachofanya humu kwenye JF, mitandao ya kijamii, na viongozi wenu kwenye vyombo vya habari, hata nje ya mipaka ya nchi ni nini?
 
Mbona mlisahau jimbo lenu ambalo lilipoteza nguvu kazi zaidi ya 200000 katika ajali ya kutumbukia kwa kivuko cha MV Nyerere, Ziwa Victoria, na Mbuge wenu akibaki mkiwa.

Toeni kibanzi jichoni kwenu kwanza

Nguvu kazi 200,000?Uko nchi gani wewe?Vilaza wengine muwe mnasoma tu kuliko kuweka ujinga wenu hapa!Waliofariki walikuwa zaidi ya 200 na si 200000!
Akina nani walisimamisha zoezi la kuokoa eti kisa giza?????
Ni akina nani waliruhusu kivuko kibebe idadi zaidi ya mara 4 inayoruhusiwa?
Wakati wa msiba,Rais wa wanyonge alikuwa akifanya tafrija na TRA wa barabarani!
 
Mbowe ni Mwiba sana kwa SISIEMU,mnafanya kila propaganda kwa mbowe,sasa kama anaibomoa chadema si ndio furaha kwenu? why mnatapatapa?
Kinachowauma ni usajili wote huo kwa gharama ya wapiga kura ila hawaoni matokeo!
Wao walitegemea wanachama wa CDM watashinikiza Mbowe atoke!!!
Ndio kwanza watu washajua mchezo wao!!!!
 
Kama wewe na wenzio huko mliko sio mandondocha chukueni fomu za kagombea ubunge kule ukelewe! Kabla ya kuja kwa Mbowe anza na mtakatifu Yohana anayeendesha nchi na chama chenu kama mali yake binafsi!
Mh Haule, Mh Nassari na Mh Mnyika kesho wataongea na wandiahi wa habari
 
Kinachowauma ni usajili wote huo kwa gharama ya wapiga kura ila hawaoni matokeo!
Wao walitegemea wanachama wa CDM watashinikiza Mbowe atoke!!!
Ndio kwanza watu washajua mchezo wao!!!!
Wapuuzi sana SISIEMU hata wawanunue wabunge wote bado CDM itasimama ,hao wanaonunuliwa mwisho wao ni 2020 tu.
 
Atafanya nini sasa na kashabanwa kotekote?

Ingekuwa mikutano imeruhusiwa angefanya operations nchi nzima kukusanya wanachama wapya
 
Nguvu kazi 200,000?Uko nchi gani wewe?Vilaza wengine muwe mnasoma tu kuliko kuweka ujinga wenu hapa!Waliofariki walikuwa zaidi ya 200 na si 200000!
Akina nani walisimamisha zoezi la kuokoa eti kisa giza?????
Ni akina nani waliruhusu kivuko kibebe idadi zaidi ya mara 4 inayoruhusiwa?
Wakati wa msiba,Rais wa wanyonge alikuwa akifanya tafrija na TRA wa barabarani!

Uelewa wako ndio huo! Hao zaidi ya 200 waliopoteza maisha wameacha wakazi wa Kisiwa cha Ukara zaidi ya 200000 wakiwa na majonzi, kwani wengi wao walikuwa ndio nguzo katika familia kiuchumi.

Majibu mepesi tena hayo kwa maswali magumu. Mnatanguliza lawama badala ya kujadili suluhisho.
 
Kama wewe na wenzio huko mliko sio mandondocha chukueni fomu za kagombea ubunge kule ukelewe! Kabla ya kuja kwa Mbowe anza na mtakatifu Yohana anayeendesha nchi na chama chenu kama mali yake binafsi!
Zanzibar hakuna wawakilishi wa cuf lakini sijasikia cuf imekufa kwa zanzibar
 
Uelewa wako ndio huo! Hao zaidi ya 200 waliopoteza maisha wameacha wakazi wa Kisiwa cha Ukara zaidi ya 200000 wakiwa na majonzi, kwani wengi wao walikuwa ndio nguzo katika familia kiuchumi.

Majibu mepesi tena hayo kwa maswali magumu. Mnatanguliza lawama badala ya kujadili suluhisho.
Kwahiyo tumepoteza nguvu kazi 200000??Hizi akili za wapi?Kama ni majonzi naamini watanzania wengi tulikuwa na majonzi tu!
Hiyo namba umeitoa kichwani kwako,umejitungia visivyokuwepo!
Turudi kwenye uhalisia,nani anasimamia usalama wa vyombo vya majini?
Msiwe wajinga wajinga!
Huyo mbunge naye hajitambui,ni nani waliyemchagua kuwaongoza?Kama ni wananchi,iweje awatelekeze?Kwani bungeni anaenda kusema kero za chama chake au anaenda kusema kero za wananchi wake?Mipango ya maendeleo jimboni kwake,je ni chama kinasimamia au yeye kwa kushirikiana na halmashauri?Sasa viongozi wajuu wa chama kutoenda msibani,ndio inatosha kuwa sababu ya kuwabebesha wananchi mamilioni ya shilingi kurudia uchaguzi?What a shame!
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Wapi huko ambapo nguvukazi zaidi ya 200000 ilipotea!?

Back
Top Bottom