Mbowe: Muungano lazima ujadiliwe

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema wananchi watajadili Katiba kadiri wanavyotaka na siyo kama anavyotaka Rais Jakaya Kikwete na kwamba hata suala la Muungano litajadiliwa kwa vile ni haki yao.

Source: Tanzania Daima.

Mbowe na misukule yake msipoteze umma hakuna mahali Kikwete ameseme Muungano usijadiliwe, kinachosemwa ni si kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuuboresha. Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu. Kama hauutaki muungano unajadili nini? si unasema tu "hatuutaki". Kwisha.

Kama unataka muungano basi kuujadili ni vipi utauboresha ruksa, hakuna aliyekatazwa.
 
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.

Kama katiba ilopo inaongelea muungano na jk anadai usiongelewe basi huenda haijui katiba ya sasa ilivyo
 
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.

Tuwe nazo tatu.
 
Mbowe na misukule yake msipoteze umma hakuna mahali Kikwete ameseme Muungano usijadiliwe, kinachosemwa ni si kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuuboresha. Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu. Kama hauutaki muungano unajadili nini? si unasema tu "hatuutaki". Kwisha.?????

Kama unataka muungano basi kuujadili ni vipi utauboresha ruksa, hakuna aliyekatazwa.

Ukisema "hatuutaki muungano" ni kuashiria kuuvunja muungano. Na kitendo cha kusema "huutaki" ni kujadili, maana huwezi kujifungia chumbani mwenyewe ukasema "huutaki". Unachosema ni Mbowe ajadili kuuvunja muungano na hapohapo unasema hilo lisijadiliwe. Jaribu kutumia akili yako kidogo kabla kuanza kuita watu misukule.
 
Suala sio mafuta tu,hatuutaki kwasababu haukufuata taratibu za kisheria nyerere (lanatullah)ametumia hadaa.hata tukitaka kuomba nje tupitie tanganyika tupewe kibali tumechoka.lazima tufe tukiwa huru.hatuutaki muungano.
 
Kwanini hakusema hilo bungeni?

Pamoja na kuwa mbunge, Mbowe ni mwenyekiti wa chama. Sio kila anachoongea lazima akiseme bungeni. Chama kina vikao vyake vya maamuzi ambavyo vinajadili mambo ya kina kuhusu mustakabali wa nchi. Na hata hivyo, Bunge sio kamati ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya.
 
Lazima Muungano huu Wazanzibar tuuvunje kwa nguvu hata kwa sheria,hatuna haja ya serikali tatu wala kumi na tatu,hakuna mtu,kiongozi wala chama chenye mamlaka ya kutupangia juu ya muungano huu.mimi nasema kwamba sisi wazanzibar kwa nguvu moja tunaukataa muungano huu hatuutaki.tugawane mbao tu wala tusilazimishwe na yeyote yule.UAMSHO WAMESHATUZINDUA TUMEAMKA SASA.IMETOSHA UKOLONI.
 
Huyu yupo RIGHT kutokana na swali alilouliza(kuuliza?!!)

nini cha kujadili kwenye muungano??

Kwa hapa;

Wewe huoni tatizo?

Ndiyo hata mimi sioni tatizo kwavile maelezo yako ni ya jumla jumla!! Hakuna aliyesema muungano hautajadiliwa....jambo la msingi nini cha kujadili kama alivyokuuliza mtotowamjini!! Kitu ambacho hakitajadiliwa ni kuvunjwa au kutovunjwa kwa muungano.....ima faima, lazima muungano uwepo, issue ni muungano wa namna gani! Suala la kujadili ni muungano wa aina gani, litajadiliwa lakini kuwepo au kutowepo, NO!!!!! Hivyo basi, Mbowe au mtoa mada mlitakiwa kuwa wazi.....ni cha kujadili!! Tujadili suala la kuendelea na muungano au kuvunjwa kwako!!
 
BINAFSI SIELEWI FAIDA YA MUUNGANO HUU MAY BE KWA CCM wanapata faida ndo maana wanang'ang'ania mfumo huu wa muungano ila kwa sasa hawataweza kuulinda tena na ni anguko pia kwao
 
Pamoja na kutambua kuwa Znz ni NCHI, mimi hakuna kitu kinachonipa shida pale ambapo kila kitu kinahitaji USAWA badala ya UWIANO! Katika hali hii unajiuliza usawa lazima uendane na uwezo wa kuzalisha pamoja na rasilimali(asili na watu). Sasa mtu unajiuliza watumilioni 40 kwa milioni mbili kwa nini haitumiki uwiano badala ya USAWA? Angalia hata idadi ya wajumbe kwenye uundwaji wa katiba inataka nusu kwa nusu! What a mistake?
Mheshimiwa nampa mkono wa hongera 100%. Mambo hayo lazima yajadiliwe na wanachi maana matatizo makubwa yamo kwenye suala tete la muungano. Mh. Mbowe kura yangu nimekupa tayari.
 
Na wakileta katiba kielelezo yenye muungano sawa na tulio nao sasa, sitaiunga mkono kwenye referendum
 
Mbowe na misukule yake msipoteze umma hakuna mahali Kikwete ameseme Muungano usijadiliwe, kinachosemwa ni si kujadili kuuvunja muungano ni kujadili kuuboresha. Kuweni wa kweli kwenye nafsi zenu. Kama hauutaki muungano unajadili nini? si unasema tu "hatuutaki". Kwisha.

Kama unataka muungano basi kuujadili ni vipi utauboresha ruksa, hakuna aliyekatazwa.
Kitendo cha kusema hauutaki muungano tayari utakuwa umejadili huwezi kusemea chumbani 'siutaki muungano' lazima uje kwa wananchi uwa-convince. Hata hivyo unaposema Kikwete kasema tuujadili lakini tusiuvunje kwani yeye ni nani si kabakiza miaka miwili tu aondoke madarakani, je baada ya hapo amri yake itaendelea ku-hold? Nafikiri Kikwete asiingilie sana suala hili historia isije ikamhukumu yeye awaachie wananchi waamue.
 
Ndiyo hata mimi sioni tatizo kwavile maelezo yako ni ya jumla jumla!! Hakuna aliyesema muungano hautajadiliwa....jambo la msingi nini cha kujadili kama alivyokuuliza mtotowamjini!! Kitu ambacho hakitajadiliwa ni kuvunjwa au kutovunjwa kwa muungano.....ima faima, lazima muungano uwepo, issue ni muungano wa namna gani! Suala la kujadili ni muungano wa aina gani, litajadiliwa lakini kuwepo au kutowepo, NO!!!!! Hivyo basi, Mbowe au mtoa mada mlitakiwa kuwa wazi.....ni cha kujadili!! Tujadili suala la kuendelea na muungano au kuvunjwa kwako!!
Nyie mnaosema tusijadili kuvunja au kutovunja lazima mtuambie kwanini tusivunje, tuambieni faida zake tuzione. Tumeishi na muungano kwa miongo mitano sasa, partner mwenzetu Zanzibar anaona kama tunamkera, sasa nyie including Kikwete ambao hamtaki uvunjike mnatakiwa muende kwa wazanzibari na watanganyika muwaeleze faida zake na sio kuwalazimisha kuwemo kwenye chumba wasichotaka. Tofauti ya hapo hata kama katiba mpya itaandikwa manung'uniko yatakuwepo na labda yatazidi kuwa mabaya zaidi. Leo wazanzibari wanadai nchi yao kwa amani kabisa itafikia wakati wataidai kwa nguvu.
 
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.
gharama zipi jamani mnasema gharama tuuu!
na mgogoro unaendelea wazenz hawakubali kabisaa wasiwe na serikali!
 
Kitendo cha kusema hauutaki muungano tayari utakuwa umejadili huwezi kusemea chumbani 'siutaki muungano' lazima uje kwa wananchi uwa-convince. Hata hivyo unaposema Kikwete kasema tuujadili lakini tusiuvunje kwani yeye ni nani si kabakiza miaka miwili tu aondoke madarakani, je baada ya hapo amri yake itaendelea ku-hold? Nafikiri Kikwete asiingilie sana suala hili historia isije ikamhukumu yeye awaachie wananchi waamue.

Kama wewe huutaki unaujadili nini sasa? si unasusa tu, au umesahau kuwa kuna kususa?

Kusema si kujadili. Naona hujui maana ya mjadala.
 
Kuujadili muungano ndio salama yetu mbele ya safari,kila upande uridhike nao ili usionekane upo kwa kulazimishawa
 
Back
Top Bottom