Elections 2010 Mbowe, Marando, Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika

Dr asante sana kwa ufafanuzi mzuri, lakini tuhakikishie kuwa wabunge wetu hawatasusia vikao eti tu kwa vile JK anahutubia. CHADEMA ndio chama kikuu cha ushindani bungeni tunategemea serikali kivuli itaundwa na chadema kwa ushiriki wa vyama vingine. Kumsusia Rais wa NEC itamaanisha mmesusia serikali yake pia na hiyo itamaanisha wabunge wenu kukaa kimya kipindi chote watakapokuwa bungeni. maana wataihoji vipi serikali wasioitambua?

Kitu wananchi tunakisubiri kwa hamu ni CHADEMA kuthibitisha kuwa kweli ushindi wa JK sio halali kwa kutuonesha matokeo ya jimbo kwa jimbo kwa kulinganisha na yale NEC tujue uchakachuaji umetokea wapi na wapi.

Tunaisubiri hiyo BIG SURPRISE DR.
 
Dr. Slaa(PhD)

Kwanza nitoe shukurani zangu za dhati kabisa kwa kujitokeza ukumbini kwa mara nyingine tena ku share views na wana jamvi. Pili asante kwa majibu yako ambayo mbali ya kutoa dukuduku letu pia yanatia moyo kuwa kumbe mapambano bado yanaendelea hasa uliposema Taifa lisubiri for a big surprise.

Niliandika heading hii makusudi kabisa nikijua lazima kiongozi mmojawapo wa Chadema ataiona, na kwa kujibu kwako nafikiri ujumbe wangu umeshafika nilikokusudia sasa nitakunywa kwa raha. Ingawa umesema tusubiri for a surprise lakini nafikiri pia ndani ya hiyo surprise liwemo hili la ku boycott hotuba ya JK anayotarajia kuitoa kati ya J'nne na J'tano kama sikosei.

Kitendo hicho kitaleta impact kubwa sana kwa siasa za Tanzania sio kwake tu hata kwa mataifa marafiki zetu, hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo ni mabunge mengi yanashuhudia wapinzani wakifanya hivyo. Mfano ni CUF 2005 walivyosusia vikao na kutomtambua Karume hali ilivyopelekea kupigiwa kelele sana na mataifa ya nje na baadaye kuzaliwa kwa mwafaka no.2.

Najua Kikwete na CCM na Makamba hawataki hicho kitokee wanataka mhudhurie ili wawe na guts za kuutangazia umma na ulimwengu kuwa tayari mmeshayakubari matokeo kitu ambacho kitawakatisha tamaa waliowapigia kura nikiwepo mimi, mtaonyesha inconsistency kwenye maamuzi yenu. Mnaweza ku match-out wakati akianza na ku match-in akimaliza.

But all in all nawatakia vikao vyema vyenye busara ili mtoke na kitu kinatakacho konga nyoyo za wapiga kura wenu. Namalizia kwa kuwapongeza kwa kutoka na maamuzi ya busara kuhusu kambi ya upinzani bungeni, kwa akili ya kawaida tu huwezi kuungana na chama kilicho ndani ya serikali at the same time ukadai wewe ni mpinzani wa chama tawala.
 
What i expect CHADEMA MPs to do is to wait for Kikwete to walk in the Bunge chambers and while everyone is standing up, they(CHADEMA MPs) should just be seated and when JK is about to start his address, CHADEMA MPs should stand up and walk out in a show of defience. Once this mkwere is doen with his address, CHADEMA MPs can walk back in and take their rightful place as Official Opposition ikiwa ni pamoja na kujibu hotuba ya mkwere.
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?
 

Dr. Slaa, Peoples President! You said it all !!

Hii ni ahadi ambayo Watanzania wengi wanaisubiria. Mliitoa na mkairudia na sasa nashukuru kuwa unaitoa tena.

Tunaomba sana "Official Position na Statement" itolewe mtakapokuwa tayari. Watanzania tunaisubiri. Na hiyo statement iambatane na takwimu zitakazodhihirisha malalamiko ya CHADEMA ya kutokutambua matokeo ay Urais "beyond the reasonable doubt".

Hili likikubalika ni mtaji mkubwa sana wa 2015 ambapo inapaswa maandalizi yake yaanze sasa. CHADEMA may take all the time, but when you are ready, please come back with something very tangible, convincing and which both NEC and CCM cannot dispute, na hata kama wakidispute iwe ni katika propaganda tu.

Tuko pamoja Kamanda.

Amandla! Peoples . . . !
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?

Rainbow, wewe ni mgeni hapa JF?

Please take time hata kufanya research yako mwenyewe kwa posts za Dr. Slaa. A simple search can give u what u can believe.

Yes ni yeye. Wapo na wengine pia kama Freeman Mbowe, John Mnyika, Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo nk.
 

Nimekuelewa vyema mkuu,

Nina la kuongezea ni kuwa CHADEMA sasa wangepanga pia mpango wa kwenda kutoa shukrani kwa wananchi walio wapigia kura na ndio jinsi ya kuendelea kuijenga ngome yao na kuchukua majimbo mengi mengi next 2015.


 

kwa hiyo maana yako ni kuwa mbatia, lyatonga, maalim sef, lipumba, jk, rizwani, au makamba hawako hapa sio?
 
dr. Slaa(phd)

tendo la kutoka nje na kurudi ndani ni kinyume na kanuni za maadili ya bunge na itasababisha wabunge wa chadema wasipewe posho zao za siku ambazo zinakaribia shilingi laki moja kwa siku KWA KILA MBUNGE MMOJA!!! na kwa jinsi walivyo wabunge wapya lengo lao la mwanzo ni kujipatia fedha ili kufidia gharama walizoingia kipindi cha uchaguzi!!!

kwa hali hiyo hakuna mbunge yeyote wa chadema atakae subutu kususia vikao vya bunge wakati jk anahutubia na habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuwa jk anania ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuhudhuria vikao vya bunge mara moja kwa wiki na hii itawafanya wabunge wa chadema washindwe kususia vikao kwa kuogopa ama kupoteza posho zao za siku, au mishahara yao minono, au adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda fulani na wakati huo huo itakuwa pigo kubwa kwa chadema kupoteza vyanzo vya mapato yake na matokeo yake ni kushindwa kulipa mishahara ya viongozi wake watendaji kama vile katibu wake mkuu na baya kuliko zote ni chadema kusambaratika na mungu apishe mbali hatungependa itokee!!!
 
Hapo ndipo nitakapojua WATANGANYIKA TUMEBADILIKA NA KUWA WAKWELI NA WENYE KUMAANISHA :smile-big:
 
Hatuongelei ushabiki soma Kanuni za bunge zinasemaje si kusema Kikwete ana mpango wa kuhudhuria kila wiki hata kama kanuni hazimruhusu. Kuhusu posho hiyo si issue kubwa.
 
in this forum you seem majorit do not know how the government works. Non of you works with the government. Sheria nyingi hamjui. That is why mna shauti bila kujua mnafanya nini. You are all negative coz of your life style. Mnategemea
Changes kupitia net. Mje katika maisha halisi ya kwako binafsi. Unataka nini. What do you miss. Who is to help you. A politician or who.
 
hatuongelei ushabiki soma kanuni za bunge zinasemaje si kusema kikwete ana mpango wa kuhudhuria kila wiki hata kama kanuni hazimruhusu. Kuhusu posho hiyo si issue kubwa.

kama posho si issue kubwa kwa chadema, tunaomba ile ahadi ya elimu bure ianze sasa kwa michango ya wabunge wenu kusomesha angalau watoto mayatima ktk majimbo yao ndipo kauli ya posho sio issue iwe ni kweli!!!
 
Kaka acheni tu waendelee maana Zitto na wenzake hilo zoezi la kutoka hawatoliweza na hiyo italeta mpasuko tena. Najua akina Mnyika, Mdee, Mbowe, lema, n.k wataweza.
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?
Nikiona maelezo ya Makamba sihitaji kuwa na elimu ya mlimani kutambua kuwa alie andika/ongea ni Makamba...hivyo hivyo na shawishika kuamini hayo maelezo ni ya Dr W. Slaa rais wangu watanzania walio wengi
 

Hahahaaa hoja yako kwa wansaikolojia tunaita so objective.. Yaani woga wa kimaendeleo... Unadhani itawakost kama wakisepa mkutano sio na JK... Lakini tutambue kuwa katiba ya nchi inamtambua raisi aliyechaguliwa na wananchi vinginevyo siye.... kwa hiyo CHADEMA wanaamini JK aliiba kwa hiyo kama wanataka kulinda katiba ni lazima watetee ukweli wa katiba na si vinginevyo!!!
 

Pasco;

Wakati wa matangazo ya Tume hakukuwa na room for negotiations, Dr Slaa alipeleka pingamizi uhesabuji usimamishwe; tume haikujali iliendelea; sio kama Chadema haikufanya kitu; Naungana na Luteni; Rais akiingia, akimaliza kusalimia, basi wabunge mmoja mmoja waanze kutoka nje, na tukio hilo liwe recorded na rais mwenyewe alione kama lilivyo maana kilichofanyika ni uhuni;

Nimegundua kilichofanyika; kura za JK zilikuwa zinabakizwa zilivyi ila kura za Dr Slaa zikawa zinapunguzwa kwa kiasi kikubwa ndio maana mmpaka ikawa hiyo 42% turnout. dangerous president, thief, sickness inauma sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…