Mbowe, Lissu, Heche, Lema, Mnyika na Sugu wanazeeka, sioni Chipukizi mwenye Hekaheka na uwezo mwenye miaka 25-40. CHADEMA wanampango upi?

Mbowe, Lissu, Heche, Lema, Mnyika na Sugu wanazeeka, sioni Chipukizi mwenye Hekaheka na uwezo mwenye miaka 25-40. CHADEMA wanampango upi?

Wewe ndiyo MTU wa kwanza duniani kuwa na mashaka na vijana wa CHADEMA....
Pale CHADEMA kuna utajiri wa viongozi mahiri Kwa miaka 100 mbele
 
Wananchi wameshahama huko kwenye kuweka imani yao kwa vyama vya siasa...wana amini katika umoja wao na nguvu ya umma...ndio mana unaona hata chadema ilipofungiwa na viongozi wake kufungwa ,haikuweza kufuta mawazo na madai ya wananchi.

Si lisu alikuwa gerezani.

Wananchi wote wataunganishwa na mawazo yao uanoyofanana KUDAI HAKI na kupinga MAOVU yote na Ufisadi,bila kujali vyama vyao wala dink zao.

vyama vya siasa havina nafasi tena ,sasa hivi nguvu ipo kwa wananchi na madai yao.

Nguvu ipo kwenye AKILI ZAO vijana ,baada ya kufuta UJINGA ULIOKUWEPO kichwani.

ELIMU imehawakomboa ,elimu ya mazingira,elimu ya uraia,na uzoefu wa nchi jirani,na utandawazi,na elkmu bure ya shule za kata ,na general knowldege ya dunia kupitia utandawazi.

DAWA PEKEE
NI SERIKALI kufanya maridhianao na WANACHI WOTE makundi yote ,siyo maridhiano na chadema pekee.
 
Uko sahihi kabisa.

Mfumo wanaoutumia hasa wa matusi na uzushi unawaweka Kona mbaya kimaadili

Wanategemea zaidi chuki kuliko maarifa na hoja.
Tofauti na kaka na dada zao wakubwa kina Lisu na Heche
Yani mwanaccm anashauri uongozi wa chadema nenda kawashauri ccm wenzio ambao walishajifia wakabaki kutegemea polis fake.
 
Gentleman,
taasisi isiyo na maono na iliyojaa waropokaji na watu wa kuhitaji kusaidiwa maisha kila uchwao, haiwezi kamwe kua na maandalizi ya aina hiyo.

na kwa ubinafsi walionao hao wangwana, sidhani kama wanahitaji kua na mpango wa kumuandaa yeyote yule kushika hatamu za uongozi ndani ya taasisi hiyo isiyoaminika na iliyopeteza kabisa uelekeo wa kisiasa nchini.
Chizi karogwa tena nonsense kama mama yako huko ccm.
 
Hao pia sio vijana. Pia hao ni watu wasioweza siasa za majukwaani. Wao ni mtandaoni tu. Hilda na Mwaipaya pia huwezi kuwaita wanasiasa... hao ni wanaharakati za kipumbavu. Malisa na Martin jukwaani wabovu mno. Pia waoga kupitiliza.

Ndio maana nikawaambia bado sijaona kijana ambaye akisimama hata watu waccm wanasema Leo KAZI ipo.
 
Ndio maana nikawaambia bado sijaona kijana ambaye akisimama hata watu waccm wanasema Leo KAZI ipo.
Ila Mtibeli kwa sasa idara za vijana za vyama vyote ziko hoi balaa. Hata huko UVCCM sioni anayeweza kuwa kiongozi mkubwa. Wengi hawana sifa. UVCCM ya kina Beno Malisa, Masauni, Nape, hata kina Sabaya zilikuwa zina uhai. Walikuwa na amsha amsha. Kwa sasa idara za kina mama (UWT & BAWACHA) zina nguvu kuliko idara za vijana.
 
Mada sahihi ni hii:

Je, Watanzania wanaona umuhimu na wako tayari kwa upinzani dhidi ya udikteta wa chama dola au wameridhika na status quo?

Kama Watanzania wengi (>80%) hawataki udikteta wa chama dola, basi upinzani wa dhati utaimarika nchini iwe kupitia CHADEMA au vinginevyo kama ilivyojitokeza 10 Oktoba. Hilo ndilo la maana kwa mustakabali wa taifa.

CHADEMA wanastahili pongezi nyingi sana hadi hapo walipofikia - against all the odds.

Lakini kujadili jinsi uongozi wa CHADEMA ulivyojijenga kupambana na CCM miaka ijayo ni kama vile sisi wengine hatuhusiki kabisa bali ni suala la “team CHADEMA” vs “team CCM”! Bizarre!

Jiulize: umesimama wapi? Unatoa ushauri upi kwa CHADEMA? Unajiona unastahili kuipa CHADEMA ushauri?
 
Waachieni akina Soka mtajua bado wapo vijana.....
Mnawafanyia ukatili akina Chakula, Sativa, Nicodemus Julius Layore chalii wa chuga mwamba wa MO29 mnahoji wako wapi watakaorithi akina Lissu na Mnyika?
 
Unajaribu kuelezea njia inayotumiwa na CCM kuidhibiti Chadema inatija na kuzaa matunda kwa CCM si ndio?

Kwamba waendelee nayo kwa sababu inawanufaisha.

Lakini upi mpango wa Chadema kujinasua dhidi ya mbinu chafu inayofanywa na ndugu zao?
Chaos ndogo ndogo, nyingi, na zenye kusambazwa maeneo yote ya nchi zinaweza kuleta matokeo yasiyotarajiwa.

Na hizi zaweza fanywa na marika yote.

Umri ni kikwazo tu kwa baadhi ya watu na hii sio tena dunia ya nabii Musa mpaka iongozwe na mtu mmoja au wawili wenye fimbo ya uchawi.
 
ila chadema imetutetea kwa mengi ni dhahiri chama kinahitaji watu wapya watakaoamsha vilivyolala
 
Hamjambo.

Nimeona viongozi wa Chadema. Asilimia tisini wapo juu ya miaka 50+ huko.

Kwa umri huo sio umri tena wa kufanya harakati zile za hekaheka. Harakati zinazohitaji nguvu kubwa ya Mwili, akili na kuongea. Viongozi hao kimsingi wamejitahidi katika maisha Yao yote ya ujana kupigania kile walichokiamini.

Lakini wakati ni ukuta. Nimewaona mara kadhaa. Ingawaje bado wana ile shauku na ari lakini baolojia inakataa. Nyuso zao na miilo yao sasa inahitaji kufanya kazi zile za mezani. Na vijana kuingia katika nafasi.

Vijana kama Malisa, Martin Maranja, John Pambalu na kina Hilda ndio wakati wao huu kupokea kijiti kusukuma gurudumu. Swali linakuja wanao uwezo wa kutosha kupambana na Dude kubwa liitwalo CCM, dude lenye mizizi mirefu, joka lenye vichwa vingi, katili lisillo na huruma?

Au wanasubiri wakati CCM ikifa kifo cha asili?

Haya mjadala upo mezani​
Naomba kufahamu umri wa makamu mwenyekiti na katibu mkuu wa sisiem
 
Chaos ndogo ndogo, nyingi, na zenye kusambazwa maeneo yote ya nchi zinaweza kuleta matokeo yasiyotarajiwa.

Na hizi zaweza fanywa na marika yote.

Umri ni kikwazo tu kwa baadhi ya watu na hii sio tena dunia ya nabii Musa mpaka iongozwe na mtu mmoja au wawili wenye fimbo ya uchawi.

Sahihi
 
Back
Top Bottom