Mbowe: JK amemkosea Jaji Warioba

Mbowe: JK amemkosea Jaji Warioba

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya makosa kuhutubia Bunge “kama mkutano wa CCM” na kuipinga hadharani Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba.

Kikwete alihutubia Bunge la Katiba Ijumaa iliyopita wakati wa uzinduzi wa chombo hicho maalumu cha kupitisha katiba mpya, lakini hotuba yake imechukuliwa na wapinzani kuwa ililenga kutetea maslahi na msimamo wa chama tawala.

Akizungumzia hotuba hiyo, Mbowe alisema Rais alikosea kwa kuwa yeye ndiye aliyeiunda tume hiyo, hivyo kuikosoa siyo sahihi.

Mbowe, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa ni sawa na kufungua mkutano wa CCM, kwani badala ya kuweka mbele masilahi ya taifa aliweka masilahi ya chama hicho tawala. “Rais Kikwete ametuondoa katika kutetea na kulinda masilahi ya umma katika Katiba Mpya na sasa ametetea msimamo wa chama chake,” alisema Mbowe.

Alisema badala ya kujenga maridhiano baina ya wajumbe, hotuba ya Rais imewagawa zaidi katika misimamo ya vyama vyao. “Hatujui nini kitatokea baadaye na hatma ya Katiba.. sisi bado tunajadiliana kama umoja wetu wa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) na tutatoa tamko la pamoja, lakini kikubwa tumesikitishwa sana na hotuba ya Rais,” alisema Mbowe.

Mbowe alifafanua kuwa Rais Kikwete alikuwa na nafasi kubwa ya kuwaunganisha wajumbe wa Bunge hilo, kama angehutubia kama Rais wa nchi badala ya kugeuza Bunge kuwa mkutano wa CCM.

Rais Kikwete alikosoa Rasimu ya Katiba juu ya mapendekezo ya Serikali tatu na ukomo wa ubunge.
 
JK aliudandia urais ila hakustahili kuwa rais wetu, nguvu ya pesa chafu imetufukisha hapa
 
amtumainiaye mwanadamu hana akili.
ni heri huyo mhutubia bunge asingalizaliwa, manake inasikitisha.
 
Ukawa inabidi ianze kufikiria kujitoa katika bunge hilo na kuwaachia ccm wategeneze katiba
yao kuliko kuendelea kulalamika nakupokea posho
 
  • Thanks
Reactions: Bob
inabidi maraisi wapimwe IQ zao kabla ya kupewa nchi,kikwete kadhihirisha uwezo wake kiakili ni wa kiwango gani,pia nadhani nyerere hakukosea sana kumtupa huyu bwana 1995.kama rais hajui kwanini nchi yake ni masikini then hajui athari za kuongeza deni la taifa kwa kujenga barabara zilizo chini ya kiwango kwa maslai ya taifa ewe mwenyenzi mungu tuondolee huu mzigo umekuwa mzito kwa watazania.ila siku zote nawalaumu viumbe dhaifu vilivyo mchagua dhaifu mwenzao no super human who is upstairs smart anaweza kumchagua huyu bwana nyerere included
 
Jei kei ni dhifu la karne ambaye hajitambui kifikira!
Huyu mkulu ni wakupelekwa milembe.
 
Naona aibu kusema jk ni rais wa nchi, uwezo wake wa kiakili ni mdogo sana
 
inabidi maraisi wapimwe iq zao kabla ya kupewa nchi,kikwete kadhihirisha uwezo wake kiakili ni wa kiwango gani,pia nadhani nyerere hakukosea sana kumtupa huyu bwana 1995.kama rais hajui kwanini nchi yake ni masikini then hajui athari za kuongeza deni la taifa kwa kujenga barabara zilizo chini ya kiwango kwa maslai ya taifa ewe mwenyenzi mungu jitwalie huyu bwana kama ulivyofanya kwa tupa kule mara tufanye uchaguzi mwingine anatuvuruga.

nakuunga mkono kwa 100%!
Jei kei ni zaidi ya kiroba cha sumu ndani ya taifa hili tz.
 
jk alichemka kwenye hotuba yake la msingi lazima UKAWA wakaze wasiwaache hawa maccm walioficha akili zao na kutembea peku safi sana mh. lugola karibu upinzani wewe hufai kuwepo ccm!!

 
Amekosea, amemkosea. Alichokosea hamkisemi, kiwanda cha uongo kinapata kigugumizi wanapoambiwa tupeni nukuu moja alipokosea Kikwete. Kimyaaa.

Zinazobaki porojo za upinzani, ni kama kelele za mlango hazimshitui mwenye nyumba. Nyie pigeni porojo akija Jakaya Mrisho Kikwete, mwenye nyumba, ndiye anaefunguwa na anaefunga mlango.

"The buck stops here" - Kikwete.

Mtahaha sana.
 
Amekosea, amemkosea. Alichokosea hamkisemi, kiwanda cha uongo kinapata kigugumizi wanapoambiwa tupeni nukuu moja alipokosea Kikwete. Kimyaaa.

Zinazobaki porojo za upinzani, ni kama kelele za mlango hazimshitui mwenye nyumba. Nyie pigeni porojo akija Jakaya Mrisho Kikwete, mwenye nyumba, ndiye anaefunguwa na anaefunga mlango.

"The buck stops here" - Kikwete.

Mtahaha sana.

Dada FAIZAFOX naomba kwa heshima na taadhima tuwekee ile picha mbowe akishangilia sana pale Bungeni wakati wa khotuba ya rais alafu tumuulize alikuwa anashangilia nini?? na leo anasema nini?? au kuna wakati alishangilia na wakati alipinga,,,, au upingaji huu umekuja baada ya kutoka nje akakuta vijana wake wanapinga na yeye akaona walau aseme chochote cha kupinga...... SIASA ZA TZ NI KAMA DRAMA
 
Lazima rais awe na msimamo .hongera jk umekatisha dhamira ya manyang'au hawapati kitu
 
Kuna nguvu kubwa sana inatumika kuisifia hotuba ya jk ,Warioba na kazi yote kubwa aliyoifanya kaminywa kabisa yaani najiuliza tu kati ya jk na warioba nani alipaswa kupewa shavu ?ni hotuba gani ambayo ilipaswa kurudiwarudiwa ?
Watanzania watanganyika tumeliwa vibaya mno tunatia huruma
 
Dada FAIZAFOX naomba kwa heshima na taadhima tuwekee ile picha mbowe akishangilia sana pale Bungeni wakati wa khotuba ya rais alafu tumuulize alikuwa anashangilia nini?? na leo anasema nini?? au kuna wakati alishangilia na wakati alipinga,,,, au upingaji huu umekuja baada ya kutoka nje akakuta vijana wake wanapinga na yeye akaona walau aseme chochote cha kupinga...... SIASA ZA TZ NI KAMA DRAMA

Kikwete mwanzoni alianza vizuri sana hata mimi nikaanza kuvutiwa nae lakini alipoanza kuichambua rasimu na kusema kuwa serikali mbili zinatekelezeka chini ya ccm ndipo alipoharibu. Hakutakiwa kuegemea upande wowote zaidi ya kutoa nasaha. Kama alikuwa anaona ile rasimu ina mapungufu hasa ya kitakwimu angeikataa na hivyo isingepekwa bungeni
 
Back
Top Bottom