Mbowe: JK amemkosea Jaji Warioba

Mbowe: JK amemkosea Jaji Warioba

Lazima rais awe na msimamo .hongera jk umekatisha dhamira ya manyang'au hawapati kitu

Kwani ile katiba ni ya raisi au ya wananchi? Kama alijua huo ndio msimamo wake kwa nini alikubali ipelekwe bungeni?
 
Dada FAIZAFOX naomba kwa heshima na taadhima tuwekee ile picha mbowe akishangilia sana pale Bungeni wakati wa khotuba ya rais alafu tumuulize alikuwa anashangilia nini?? na leo anasema nini?? au kuna wakati alishangilia na wakati alipinga,,,, au upingaji huu umekuja baada ya kutoka nje akakuta vijana wake wanapinga na yeye akaona walau aseme chochote cha kupinga...... SIASA ZA TZ NI KAMA DRAMA

Hivi ukiona mtu anacheka ni kuwa anacheka? Anaweza kuwa anmcheka na kushangilia kuwa udhaifu alioutarajia umetimia!
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya makosa kuhutubia Bunge “kama mkutano wa CCM” na kuipinga hadharani Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba.

Kikwete alihutubia Bunge la Katiba Ijumaa iliyopita wakati wa uzinduzi wa chombo hicho maalumu cha kupitisha katiba mpya, lakini hotuba yake imechukuliwa na wapinzani kuwa ililenga kutetea maslahi na msimamo wa chama tawala.

Akizungumzia hotuba hiyo, Mbowe alisema Rais alikosea kwa kuwa yeye ndiye aliyeiunda tume hiyo, hivyo kuikosoa siyo sahihi.

Mbowe, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa ni sawa na kufungua mkutano wa CCM, kwani badala ya kuweka mbele masilahi ya taifa aliweka masilahi ya chama hicho tawala. “Rais Kikwete ametuondoa katika kutetea na kulinda masilahi ya umma katika Katiba Mpya na sasa ametetea msimamo wa chama chake,” alisema Mbowe.

Alisema badala ya kujenga maridhiano baina ya wajumbe, hotuba ya Rais imewagawa zaidi katika misimamo ya vyama vyao. “Hatujui nini kitatokea baadaye na hatma ya Katiba.. sisi bado tunajadiliana kama umoja wetu wa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) na tutatoa tamko la pamoja, lakini kikubwa tumesikitishwa sana na hotuba ya Rais,” alisema Mbowe.

Mbowe alifafanua kuwa Rais Kikwete alikuwa na nafasi kubwa ya kuwaunganisha wajumbe wa Bunge hilo, kama angehutubia kama Rais wa nchi badala ya kugeuza Bunge kuwa mkutano wa CCM.

Rais Kikwete alikosoa Rasimu ya Katiba juu ya mapendekezo ya Serikali tatu na ukomo wa ubunge.

Walipoona bunge limegeuzwa mkutano wa CCM walifanya nini? kukaa kimya wakati tembo anamkanyaga chura ni kushiriki katika mauji ya chura huyo. UKAWA mmeshapoteza dira. Kama ni goli mmeshafungwa. Muda wenu wa kuchukua hatua karibu unaisha. Msipotumia muda huo mfahamu wazi Wananchi watatafuta watu wengine wa kuwasemea. Kwa kuwa mliopewa dhamana inaonekana mmenogewa na posho ya siku.
 
Amekosea, amemkosea. Alichokosea hamkisemi, kiwanda cha uongo kinapata kigugumizi wanapoambiwa tupeni nukuu moja alipokosea Kikwete. Kimyaaa.

Zinazobaki porojo za upinzani, ni kama kelele za mlango hazimshitui mwenye nyumba. Nyie pigeni porojo akija Jakaya Mrisho Kikwete, mwenye nyumba, ndiye anaefunguwa na anaefunga mlango.

"The buck stops here" - Kikwete.

Mtahaha sana.

Ewe mola tunakuomba husitufikishe mahali wanapotaka kutufikisha kina Fayza, kwani hawajitambui hata kidogo.
 
UKAWA wajitoe bunge la katiba ndio njia muafaka.Hongera sana mh Lipunmba kwa kukataa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Ewe mola tunakuomba husitufikishe mahali wanapotaka kutufikisha kina Fayza, kwani hawajitambui hata kidogo.

Wewe unaejitambuwa sema ni kipi kibaya alichokiongea Kikwete. Leta nukuu, wacha porojo.

Aliokufikisha hapo ulipo ukawa huijui Tanganyika ni Nyerere, umeshajiuliza kwanini Nyerere mwenyeheri aiuwe nchi nzima na kuififirisha isiwepo duniani?
 
Dada FAIZAFOX naomba kwa heshima na taadhima tuwekee ile picha mbowe akishangilia sana pale Bungeni wakati wa khotuba ya rais alafu tumuulize alikuwa anashangilia nini?? na leo anasema nini?? au kuna wakati alishangilia na wakati alipinga,,,, au upingaji huu umekuja baada ya kutoka nje akakuta vijana wake wanapinga na yeye akaona walau aseme chochote cha kupinga...... SIASA ZA TZ NI KAMA DRAMA

Hii hapa:

mg27-w480-h58021.jpg

Na nyuzi yake hii hapa: https://www.jamiiforums.com/katiba-...yofurahia-hotuba-ya-kikwete-bungeni-jana.html

Sasa tunamuuliza:alikuwa anashangilia nini?? na leo anasema nini??
 
Hivi mnadhani kanuni ya kutaka Jakaya afungue bunge ndipo Warioba akabidhi rasimu ilitenguliwa kwa bahati Mbaya!? Huyo ndio mzee wa kung'ata na kupuliza.
 
Wewe unaejitambuwa sema ni kipi kibaya alichokiongea Kikwete. Leta nukuu, wacha porojo.

Aliokufikisha hapo ulipo ukawa huijui Tanganyika ni Nyerere, umeshajiuliza kwanini Nyerere mwenyeheri aiuwe nchi nzima na kuififirisha isiwepo duniani?

Ujinga alioongelea Kikwete. 90% ya Tanzania bara wamezaliwa baada Ya muungano kwaihiyo hawaiitaji Tanganyika. Je mbona 1960s watu wengi walikuwa wamezaliwa wakati wa ukoloni lakini walipigania ukoloni? Au mbola wapalestina maeneo yao yametawaliwa na israeli toka 47 lakini bado wanayapigani. Mtu mwenye akili timamu hawezi kusema au kutete upuuzi huo apo juu
 
Hayo umeongeza wewe.

Ni ukweli usiopingika kuwa 90% ya Watanzania wamezaliwa Tanzania, tumebaki wachache tuliozaliwa Tanganyika, hilo hata ufanye nini ndio ukweli na hakuna kosa hapo. Kosa lako ni kuongezea hayo maneno niliyokuwekea nyekundu.

Jee, hili hukuliona:

- Ningependa kama mnaamua tuwe na serikali tatu, basi ziwe tatu zinazosimama na thabiti! - Kikwete
 
Hiki mbona hamkisemi, au Warioba alikuwa sawa?

Kwa mfano, Ibara ya 2 ya Rasimu inayotambulisha eneo na mipaka ya nchi yetu. Ibara hiyo inasomeka kuwa "Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari".

Maelezo hayo yameacha kutambua, kwa upande wa Tanzania Bara, sehemu yetu ya maziwa na mito ambayo ni kubwa sana. Kwa nini tuache kuitaja? Je hatutoi nafasi kwa nchi tunazopakana nazo siku moja wakaja kupora sehemu zetu hizo na sisi kukosa utetezi kwa kuwa hata Katiba yetu haikuyatambua maeneo hayo kuwa ni yetu? Hili ni jambo kubwa ambaloBunge hili lazima mlirekebishe. Wakati ndiyo huu hakuna mwingine.

Source: SOMA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIYOITOA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA MACHI 21, 2014 ~ Father Kidevu
 
Back
Top Bottom