Mbowe ni mjasiliamali wa kisiasa,kwake ni pesa kwanza CHADEMA baadaye.Wengi wanaimtetea Mbowe humu ni kwasababu wametawaliwa na hisia za kishabiki,wangekuwa tayari kuelewa yanayoendelea hapa nchini wangeandamana mara moja kutaka Mbowe asigombe nafasi ya KUB.Nawakumbusha kuhusu sakata la ESCROW, hivi nini kilimshawishi Mbowe kumwamini Zitto hata kuiunga mkono ripoti yake ya kupikwa ya ESCROW? Sote tunajua kwamba ile ripoti ya kamati ya akina Zitto ilipikwa kuwalinda vigogo flani ndani ya serikali,katika taasisi za dini,wanasiasa na familia za viongozi.Ina maana Mbowe na umakini wake wote hakuyajua haya au alipiga fedha za ESCROW? Mbaya zaidi Mbowe huyu huyu na huyu anayemwita hasimu wake wa kisiasa Zitto wakaungana tena kuja na maazimio yao uchwara dhidi ya serikali kumbe walikuwa wanatuzuga tu,mbona hatusikii tena kuhusu yale maazimio yao dhidi ya serikali?yalitekelezwa?Wana CHADEMA shtukeni,hapo hakuna Mwenyekiti wa CHADEMA ila kuna mpiga dili tu.