Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Nimevutiwa sana na mahojiano ya EATV na mbunge mstaafu wa Kilwa kusini, ndugu Suleiman Abdallah, almaarufu Bwege ya tarehe June 9, 2025.
Mahojiano hayo yaliyohusu mambo mengi ikiwemo, hali yake kiafya, vyama vya siasa na madai ya reforms kuelekea uchaguzi mkuu October 2025, nafasi ya ndugu Freeman Mbowe na ujio wa CHAUMA. Hili la mwisho ndilo ningependa kulizungumzia leo.
Katika mahojiano yake, ameeleza kuwa katika kulea vifaranga; utamaduni wa mama kuku ni kutangulia na vifaranga kumfuata lakini utamaduni wa bata ni vifaranga kutangulia na mama bata hufuata. Kwa maoni yake mpaka kufikia August, kwenye hili la CHAUMA, tutajua Mbowe kacheza kama bata au Kuku?
Ndugu Suleiman Abdallah anahitimisha kwa kusema, fumbo mfumbie mjinga, mwelevu ataling'amua. Amehoji; fumba na kufumbua, CHAUMA ya akina Kigaila imepata wapi uwezo wa kukodi Helikopter, kununua magari na kuanza kampeni nchi nzima?