Mbowe: CCM ni Mbugi

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amekifananisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mchezo wa ‘Mbugi’.
Wakati Mbowe akiwaita CCM Mbugi, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliwaita CCM Intarahamwe.
Kwa mujibu wa Mbowe, Mbugi ni mchezo wa soka usio na sheria, wala refa.
Alisema kwenye mchezo wa Mbugi hakuna idadi kamili ya wachezaji, kila mchezaji akiingia anachezea timu anayotaka, katikati ya mchezo anaweza kubadilisha timu na kuchezea timu nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza Baraza jipya la Mawaziri Kivuli lenye ya wajumbe wa UKAWA, Mbowe alisema wanachosema na kufanya CCM kwa sasa ni sawa na Mbugi, kwani hawana kanuni na kila mtu anaweza kusema anachotaka.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na kauli na misimamo tofauti kuhusu UKAWA zinazotolewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Akitolea mfano alisema hivi karibuni Kamati Kuu ya CCM ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni mjumbe, wamepitisha azimio la kutoshughulika na UKAWA kwani wameamua kutoka kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
“Pinda huyo huyo akihitimisha hotuba yake, anawasihii UKAWA kurudi bungeni. Juzi Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano), anasema UKAWA walitoka bila sababu, watarudi bila sababu, lakini ukimsikiliza Nape Nnauye na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana wanasema UKAWA wasibembelezwe, waachwe wabaki nje ya Bunge. Hii ni Mbugi.
“Kinana kaja kavua shati kaingia kwenye Mbugi, Nape naye Mbugi, Wassira katoa shati kaingia kwenye mchezo Mbugi, hawana kanuni, sheria. CCM ni Mbugi,” alisisitiza Mbowe.
 
Mbowe ni mzinifu. Je akiitwa hivyo atafurahia au atachukia?
 

Ukiwasikiliza CCM utastaajabu kama vichaa huwezi jua nani ni nani yaani ni Mambugi kweli kweli
 
Wananchi wanataka kusikia namna ambavyo wataweza kuyafikia maisha wanayotamani huku wakisaidiwa na sera za vyama vya hao viongozi wa kakikundi kanakoitwa UKAWA.

Badala ya kuwa politically serious, wao wanaleta mipasho ya majina ya msimu. Ndiyo maana vyama vyao vinawafia na sasa wameamua kuficha udhaifu wao ndani ya kikundi wanachokiita UKAWA. Eti CHADEMA imeungana na CUF. Are they serious?.
 
Kinachoonekana hapa ni Mbowe kujitafutia umaarufu baada ya kuona kuwa Prof anatamba
 
Hakika Mkuu. Wameona vyama vyao vinakufa na sasa wanatafuta umaarufu kupitia UKAWA
 
Baada ya cdm kudoda mbowe sasa anajishikiza cuf na nccr
 
Baada ya cdm kudoda mbowe sasa anajishikiza cuf na nccr

Huu muongano unawatoa pofu kwl, wengine waungane nyie muumie changaza,
Hv vyama si kama ccm rais wenu kila cku kuomba misaada nchi za ushago na inavyosemeka kasain ila kitu xo hapo mnatetea haki zenu hii misaada hii lazima kuna vigogo wanabutuliwa hapo!!
 

kajifunze kiswahili kule ferry hata sikuelewi unasemaje
 
Mbowe ni mzinifu. Je akiitwa hivyo atafurahia au atachukia?
Lizaboni wewe huwa unapenda kwenda nje ya mada kwa kuweka mipasho yako, ndiyo maana watu wanakutukana. Ama ni janja yako ya kuwatafutia watu kula ban?
 
Last edited by a moderator:

mkuu mwanadiwani, vip update za nzega, ujarusha hapa jukwaani, mapictures
 
Lizaboni wewe huwa unapenda kwenda nje ya mada kwa kuweka mipasho yako, ndiyo maana watu wanakutukana. Ama ni janja yako ya kuwatafutia watu kula ban?
Mkuu, sina sababu ya kuwatafutia watu ban. Wao wamehiari kutukana sisi tunajenga hoja. Nadhani sikueleweka hapo. Mbowe na Lipumba wamekuwa maarufu sana wa kuwapachika majina mabaya wenzao tena kwa matendo wasiyofanya. Wao wanafanya matendo mabaya kama ya uzinifu na...... Na jamii inajua. Tukiwaita majina mabaya ya matendo yao mabaya tutakuwa tunakosea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…