Chadema, CUF, NCCR na TLP Kuhutubia Mikutano kwa Pamoja Nchi Nzima

mkuu nakuunga mkono 100%. Huyu mleta hii thred ni msanii, na hii kitu haipo. Hakuna kiongozi yeyote wa chadema anayeweza kukubali upuuzi huu. Kwani Dr na kamanda Lema huo mtafaruku wanaoiletea ccm huko mwanza hamjasikia? Sasa ya nini kwenda kumchukua hata Mrema aliyejichokea? Cuf ni ccm B.hapo hamna logic, mods tupa hii kwenye jukwaa la umbea kama lipo!
Kumbuka hivyo vyama vilivyokufa, vilikuwa hai na wakati fulani ndivyo vilivyokuwa na nguvu bungeni.
Na moja ya sababu za kufa kwao ni sera za CCM za "wagawe uwatawale". CCM hufurahi sana wakiona upinzani unagawanyika hasa katika mambo ya msingi. Sisemi kuwa CDM haina uwezo wa siku moja kuja kuwa na nguvu na kuwa chama tawala, lakini kwa hili CDM peke yao hawaliwezi, wanavihitaji vyama vyegine, wanawahitaji Watanzania wote.
 
Hii ninaipinga.CDM kuweni makini sana.Watanzania wameshawaamini nyie acheni kushirikiana na matawi ya magamba.Hivi mtashirikiana na CUF halafu iweje?? Inaingia akilini kweli??

mkuu ila nadhani kwa kutafuta tu hizo sahihi hataleta madhara
 
Hii inaweza kuwa nzuri kama dhamira itakuwa ni moja, lakini mimi siungi mkono hoja hii maana kuna vyama ambavyo vinahitaji mgongo wa CDM ili vinyanyuke na mwisho wa siku vitaipunguzia kura CDM!!

Kuifufua CUF na TLP litakuwa ni kosa kubwa sana kuwahi kufanyika kwenye duru za siasa Tz!! Hii itakuwa ni kukirudishia chama wanachama wake ambao watatugharimu 2015. CDM kwasasa inajitosheleza kuiteka Tz kwa staili yoyote ile, haina haja ya kutafuta msaada!!

Wadau msisahau hivi vyama vingine vina mamuruki wengi na havina dhamira ya dhati zaidi ya maslahi binafsi!! Hii kete ni nzuri sana ktk kuwahisha ukombozi lakini nina mashaka sana na unafiki wa hivi vyama vingine!!
 
Jamani penye ukweli lazima tuseme kweli na kwa haki. kuna mambo ambayo CUF hawapaswi kudharauliwa. Ebu angalia wabunge wa CUF walivyo-support hoja ya Zitto na kumwaga saini zao. Bila wabunge wa CUF hizo sahihi 70 zisingetimia. Hawa ni washirika muhimu wa ukombozi wa Watanzania. CUF ya Zanzibar iliyoko kwenye Baraza la Wawakilishi tusiilinganishe na CUF iliyoko kwenye Bunge la Muungano. Kule Zanzibar ndo CCM na CUF ni pete na kidole sababu wote wana ajenda moja juu ya Muungano. Lakni hawa wa huku hawana chochote ubaya wowote. Isitoshe hata wao wanataka siku moja CCM itoke madarakani watawale wao. Wanajua kabisa kwa nguvu yao tu hawawezi kufanya chochote. Pia ni nafasi yao nao kurejeshea imani kidogo watanzania maana walikuwa wanaporomoka kwa kasi ya kutisha. Hivyo kama wanataka kueleweka kwa watanzania hawana njia ya kufanya zaidi ya kuwaunga mkono CDM ktk hii vita ya ufisadi. Na wabunge wa CCM wenye nia njema na nchi hii wangejiunga na vita hii. Lakini wamekuwa wasaliti wakubwa wa watanzania. Mungu ataipigania nchi hii kupitia kwa watu wenye mapenzi mema na nchi hii.

Mkuu wangu CUF ya bara ndiyo ipi hiyo? Ile iliyotukana matusi ya nguoni wabunge wa CDM pale bungeni walipokuwa wanapinga mswada mbovu wa katiba? CUF ile iliyoshirikiana na CCM kuhujumu kambi rasmi ya upinzani bungeni? CUF ile iliohangaika huku na kule kupinga maandamano ya CDM? CUF ile iliosema CDM inataka kuvuruga amani ya nchi hii? CUF ile iliyoungana na CCM kule Igunga kuhakikisha mgombea wa CDM hashindi? Labda kama ni CUF nyingine.Lakini kwa CUF hii ambayo katibu mkuu wake ni makamu wa kwanza wa rais hakika nitakuwa mtu wa mwisho kuunga mkono kitendo hicho.Huo utakuwa ni usaliti mkubwa kwa wanachadema wanaopigana mchana na usiku kuhakikisha chama kinaingia Ikulu.Dr Slaa tafadhali yasome maoni yangu na tambua yanawakilisha maelfu ya wanachadema kote nchini.
 
Hii ninaipinga.CDM kuweni makini sana.Watanzania wameshawaamini nyie acheni kushirikiana na matawi ya magamba.Hivi mtashirikiana na CUF halafu iweje?? Inaingia akilini kweli??

Mbona kwenye sahihi 70 wameshirikiaana?, acha maneno yako. Kwanza wafanye tu maana mimi nitakuwa wa kwanza kuweka sahihi ya kutokuwa na imani na Mkimbizi wa muda wa mara kwa mara(Mkwe.re).
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
:target:nimefurahia hiyo collabo"ila lazima CDM iwe makini" haya nanyi CCM colabo yenu mnafanya na nani?
 
CHADEMA acheni alliance za kijinga, kwani nyie pekee yenu mnaweza kusimama na kuitikisa nchi kwani mkifanya kuungana na hao CUF na TLP huo utakuwa ni usanii mkubwa sna kwani memsahau jinsi CUF ilivyo ni upande wa CCM? Kumbukeni igunga CUF iliwafanya nini? Pia kumbukeni sababu za kutokushirikiana ktk kambi ya upinzani bungeni na hivi vyama mapandakizi, hebu acheni mambo hayo bwana
.. Mungu wa isarael aepushie mbali muungano huo kama jinsi alivyoepusha kifo cha yusuph mbele ya ndungu zake.
Kwa jina la YESU. Amen

mawazo kama haya hayafai kupewa nafasi katika jamii ya watanzania wanaoamini katika mabadiliko,hongera chadema kwa kunzisha ushirikiano na vyama hivyo,kwani kuna maeneo kama ya kusini na baadhi ya mikoa ya pwani hamkubaliki,kwa kuwaweka CUF karibu naamini mtapenya
 
Nimefurahi kuona sasa chadema mmeanza kuelewa umuhimu wa kuunganisha nguvu za vyama maana mmeelewa hamna uwezo wa kuleta mabadiliko bila mbeleko ya wenzenu hasa cuf ambao huwa mnadai wameolewa na ccm,sasa sijui tuwaite wake wenza mlioamua kuungana dhidi ya bwana au?
 
Hii ninaipinga.CDM kuweni makini sana.Watanzania wameshawaamini nyie acheni kushirikiana na matawi ya magamba.Hivi mtashirikiana na CUF halafu iweje?? Inaingia akilini kweli??
nashangaa....ivi unaungana na cuf kuipindua ccm? cuf ni ccmb
 
Kuungana ni kitu ambacho hakiwezekani na wala CDM isitegemee jipya kutoka kwa CUF, NCCR na TLP zaidi ni unafiki tu wanataka kuleta.
 
Jamani chonde chonde naomba viongoz wa chadema wajifikilie mara mbilimbili kuhusu kuungana na vyama vingine kwa hili,mim naona wasimame wenyewe peke yao,hivi vyama vingine hamna lolote
 
Back
Top Bottom