mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,049
- 4,904
. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema chama tawala, CCM kinapaswa kulaumiwa kwa maumivu yote ambayo Watanzania wameyapata katika miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
Amesema katika muda huo, Tanzania imepitia vipindi tofauti, lakini kipindi cha kati ya mwaka 2015 – 2021 kilikuwa cha maumivu makali kwenye demokrasia na athari zake kila Mtanzania alizishuhudia.
Hoja hizo za Mbowe zilijibiwa na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Stephen Wasira akisema CCM haiwezi kulaumiwa kwa kila jambo kwa sababu mambo mengine yanatokea kwenye vyama bila chama chenyewe kuhusika.
Mbowe alitoa lawama hizo juzi jioni, wakati akichangia mjadala kuhusu hali ya siasa ya vyama vingi na maendeleo nchini, ulioandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Sera Afrika (CIP) na kufanyika kupitia mtandao wa Clubhouse.
Mjadala huo ulioanza saa 11:00 jioni ulimalizika saa 3:00 usiku na kushirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo wanasiasa wakongwe Wasira, Zitto Kabwe na Hamad Rashid Mohammed.