Mbowe awasili Msibani kwa Mzee Mtei

Mbowe awasili Msibani kwa Mzee Mtei

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewasili muda huu katika msiba nyumbani kwa marehemu Edwin Mtei, aliyefariki dunia Januari 19.

Mtei alikuwa ni mwasisi wa CHADEMA pamoja na mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho. Kufuatia kifo chake, CHADEMA imetangaza maombolezo ya siku saba kama sehemu ya kuenzi mchango wake mkubwa katika historia ya chama hicho na siasa za Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Ndondi Totinam, viongozi mbalimbali wa chama pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kuwasili msibani leo, huku wengine wakitarajiwa kufika kesho.

Ameenda kuhani kwenye msiba wa baba mkwe wake na sio kama mwanachadema, viongozi wa Chadema wametekwa, wamewekwa ndani na wengine kuuawa hakujitokeza.
Wakati wa uongozi wake aliwapigania sana wanachama waliouawa, kutekwa na kuwekwa ndani. Alipokamatwa Makamu Mwenyekiti wake Mbeya hakusita kwenda kumpigania. Aliitisha maandamano kupinga mauaji na utekaji lakini alitokea yeye na binti yake. Baada ya yote hayo Chadema mkageuka na kumuita mpiga dili, msaliti, mlamba asali na kuwa amewachelewesha sana. Wakati mkimsema hivyo viongozi waliangalia tu bila kutia neno.

Sasa leo mnataka ajitokeze tena kuwatetea watu ambao mumemkataa waziwazi? Muacheni apumzike wakati mkiendelea kuwapambania mliowachagua.

Sijui wakina Heche na Mnyika watamwambia nini wakikutana nae kwenye msiba wa mkwe na muasisi mwenzake? Kama wataenda.

Amandla...
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewasili muda huu katika msiba nyumbani kwa marehemu Edwin Mtei, aliyefariki dunia Januari 19.

Mtei alikuwa ni mwasisi wa CHADEMA pamoja na mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho. Kufuatia kifo chake, CHADEMA imetangaza maombolezo ya siku saba kama sehemu ya kuenzi mchango wake mkubwa katika historia ya chama hicho na siasa za Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Ndondi Totinam, viongozi mbalimbali wa chama pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kuwasili msibani leo, huku wengine wakitarajiwa kufika kesho.

Acha kujikomba kwa Mbowe. Ni lazima aende kwani mke wake ni Binti wa marehemu Mtei. Sasa niambie, unaachaje kuhudhuria msiba wa mkweo?
 
Back
Top Bottom