Mbowe awashangaa watanzania... Uwanja wa Ndege Kilimanjaro unakodishwa kwa Dola 1,000 kwa MWAKA!

Mh Mbowe amesema dunia inashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu ambayo watu hawajui kuhoji mashirika yao yanavyofilisiwa na watu wachache. ametolea mfano kukodishwa kwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) kwa Dola za kimarekani 1000 kwa mwaka.

Nawasilisha

DU hata kodi yangu ya nyumba kwa mwaka imezidiwa!!
 
usd 1000 kwa mwaka naomba tuache utani jamani hili sio jukwa la jokes. siamini kama kweli ni viongozi wetu IQ zao zinafanya kazi au pengine roho zao hazipo tanzania au kunambengu zilizalishwa kwa wazazi wao i mean walipigwa pair kutoka nje ya tanzania ndio maana wanafanya kitu kama hiki wakijua sio watanzania
 
Dola 1000,ATC yetu jaman tunakwenda wap...?? m nakereka sana na hao n CCM tu si ndo walio in power...! Wenye SERA mbovuu..! 'Baadh ya waTz bado nao wanaendelea kuokota mawe badala ya Almas lakn ipo siku watangundua walkuwa busy wakiokota kisicho' Siwatukani maana ninyi ndo VOTES mtakaobadilisha haya yote kwa kura za ndiyo kwa CHDMA!tubadlke jameni 2015 ilee imekaribia.Lazma haya yote yaishe siyo kwa kuvua Gamba ila kwa kutoa ile SUMU. inayosababisha yote haya.....!
 
Mh Mbowe amesema dunia inashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu ambayo watu hawajui kuhoji mashirika yao yanavyofilisiwa na watu wachache. ametolea mfano kukodishwa kwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) kwa Dola za kimarekani 1000 kwa mwaka.

Nawasilisha

kumbe huu ugonjwa wa kushangaa unaambukiza??
pinda alishangaa
JK akashangaa
sasa Mbowe anashangaa
basi na mimi nashangaa
 
dola 1000 kwa mwaka mbona hata mie ningeweza kulipa. Pambafu kabisa wote waliofanya hivyo
 
Mleta mada unajua dola 1000 ni shilingi ngapi za Tanzania? Au unapima kiwango cha akili za wachangia hapa JF! Naona umewapata sana wazee wa kukurupuka!
 
Mimi nawashangaa Watanzania kwa kuwa mahiri zaidi wa kulalamika badala ya kutenda.
 
Tunamhitaji Jerry Rawlings wa kitanzania. Jeshi mko wapi mrudishe heshima? Ondoeni hawa majitu, itakuwa lesser evil
 
Mh Mbowe amesema dunia inashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu ambayo watu hawajui kuhoji mashirika yao yanavyofilisiwa na watu wachache. ametolea mfano kukodishwa kwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) kwa Dola za kimarekani 1000 kwa mwaka.

Nawasilisha

Sawa......lakini je amesemaje kingine zaidi ya kuwashangaa waTZ?

Maana haitoshi kushangaa tu bila ya kutoa ufumbuzi.
Naona hata sisi wachangiaji ni dhahiri tunaonekana kuunga mkono kushangaa kwa kamanda Freeman!

Tunaendekeza sana kuwahukumu wengine (mikia, mikono, tumbo, viuno, vidole kama akina Jairo, etc) lakini tunaacha kichwa cha tatizo - JK!!

Kuna watu huko nyuma tulishaonyesha nia ya kuanzishwa kwa mchakato wa impeachment (unashangaa?...ndiyo, impeachment ya JK!!).
Nani atabisha kuwa jamaa hajavunja katiba (directly and/or indirectly) kwa haya yote aliyotufanyia tangu aingie pale Magogoni 2005??

To me, a call for impeachment from any section of this society is a very strong message to the rulers and an eye opener to waTZ tunaondelea kushangaza na kushangaa. Hata kama impeachment attempt ita-hit snag, hizo shock waves zake will make hell break loose!

Try me...
 
Mbowe, mboweee. A. Mbowe, KUB! Kesho muulize 1 kwa 1 PM, Kuhusu haya mashirika yetu ya umma. Tutampima na ajipime baada ya majibu yake. Aaaaaggrrrrrr...
 
Mleta mada unajua dola 1000 ni shilingi ngapi za Tanzania? Au unapima kiwango cha akili za wachangia hapa JF! Naona umewapata sana wazee wa kukurupuka!
Mkuu haka kakibanda ninakoishi nalipa dola 1500 kwa mwaka sasa ukiniambia KIA ni $ 1000 lazima nipate kizunguzungu na kushangaa
 
Mh Mbowe amesema dunia inashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu ambayo watu hawajui kuhoji mashirika yao yanavyofilisiwa na watu wachache. ametolea mfano kukodishwa kwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) kwa Dola za kimarekani 1000 kwa mwaka.

Nawasilisha

Ukihoji ama ukijaribu kuwaelimisha watu basi unaambiwa eti ni mdini, na kuna wengine hudiriki hadi kuandamana kupinga udini. Akili za watu zimetekwa na kufanywa mazuzu hadi wanashindwa kutofautisha kati ya ufisadi na udini.
 
Mh Mbowe amesema dunia inashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu ambayo watu hawajui kuhoji mashirika yao yanavyofilisiwa na watu wachache. ametolea mfano kukodishwa kwa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) kwa Dola za kimarekani 1000 kwa mwaka.
Nawasilisha

Samahani mleta mada naomba ufafanuzi kidogo, kichwa cha mada kinasema Mbowe awashangaa Watanzania lakini kwenye maelezo unasema Mh. Mbowe asema dunia inashangaa Tanzania ! Yupi hasa ulitaka kusema anashangaa ?

Mleta mada unajua dola 1000 ni shilingi ngapi za Tanzania? Au unapima kiwango cha akili za wachangia hapa JF! Naona umewapata sana wazee wa kukurupuka!

Hatukurupuki. USD 1 ya Marekani ni Tsh. 1,600/-, hivyo USD 1000 kwa mwaka ni Tsh. 1,600,000/- kwa mwaka sawa na Tsh. 130,000/- kwa mwezi ! Maana yake ni kuwa unakodisha uwanja wa ndege kama vile unakodisha kiosk ! Sasa hapa Mzee wa Posho ni vizuri umwombe radhi mleta mada na wachangiaji halafu ukiri kuwa kama ni kukurupuka hakuna kama Mzee wa Posho !
 
Back
Top Bottom