Elections 2010 Mbowe atikisa mjini Arusha...

Watu ni wengi sana pale kwenye uwanja NMC kweli siku za mabadiliko zina karibia...
 
Zito au dr slaa lazima arudi mwanza, busanda na tarime, kwimba kwa reticia nyerere hayo ni majimbo yanayohitaji final touch kuyaweka kibindoni

Hapo kwimba nina wasiwasi na huyo mama Leticia Nyerere kwani wiki mbili zilizopita nilikuwa pale Hungumalwa na takribani wiki nzima nilikuwa nikiona Noah yake imepaki tu. Hajafanya mkutano hata mmoja wa ukweli na huko mgombea wa ccm anakubalika zaidi kwani anamchango mkubwa kwa wananchi. Kuna haja ya viongozi wa juu kwenda huko hizi siku mbili tatu.
 
huu muda mnaoutumia kudanganya watu ndio utakaowacost chadema, hamna kitu kama hicho hapa arusha!
Acha ujinga wewe fika pale NMC uone nyomi ya watu, inawezekana ni mmoja ya watu niliopata kuongea nao njia nikiwa naelekea Unga lmt wana lalamika kwamba viongozi wa chadema wakija arusha huwa hawatoi matangazo ya kutosha mimi mwenye nilisha sahau kama leo Mbowe atakuwepo Arusha mpaka nilipo ona hapa JF ndipo nikaenda pale NMC..Watu ni wengi Nimebahatika kuchukua picha naangalia jinsi ya kutuma mana sina cable na mimetumia simu..
 
mi naona Steven Nyerere anatosha kuweka mambo sawa Tarime,Mwanza,Busanda na kwa leticia Nyerere
 
Pata picha
 
Attachments

  • mbowearusha.jpg
    mbowearusha.jpg
    38.7 KB · Views: 966
  • mbowearusha3.jpg
    mbowearusha3.jpg
    54 KB · Views: 1,071
  • mbowearusha12.jpg
    mbowearusha12.jpg
    31.3 KB · Views: 183
naambiwa kule Mtwara watu ni wengi sana hivyo tujiandae kwa mabadiliko tarehe 31 -10-2010..ila usisahau kwenda kupiga kura usimsahau jirani yako......
 
habari hizi si za ukweli ndo kwanza wanapita hapa uhuru road na magari yasiyozidi ishirini auchini yake, hakunala zaidi wala mji haujatetemeka wala hakukuwa na matangazo ya kutisha, na pia watu wamekuwa wakiwaonyeshea alama ya ccm kila wananyoosha antena , maana ccm imeshika chanel zote. Isitoshe ni wengi wao ni wakazi wa moshi waliokuja na mbowe. msidanganye watu ni kama msafarawa harusi ya hali ya chini tu.

Kweli ukipenda chongo unaona kengeza.
 
Kazi tunamalizia bado ya kuweka tick na count down.Mwaka huu CCM watajuta kutufahamuuuuuuuuu!!!!
 
habari hizi si za ukweli ndo kwanza wanapita hapa uhuru road na magari yasiyozidi ishirini auchini yake, hakunala zaidi wala mji haujatetemeka wala hakukuwa na matangazo ya kutisha, na pia watu wamekuwa wakiwaonyeshea alama ya ccm kila wananyoosha antena , maana ccm imeshika chanel zote. Isitoshe ni wengi wao ni wakazi wa moshi waliokuja na mbowe. msidanganye watu ni kama msafarawa harusi ya hali ya chini tu.

Pole mama una jina kama la kike vile basi pole tena mama!!! Nimeongea na jamaa yangu yuko arusha anasema jimbo linatetemeka sasa wewe unakuja na sera gani hizo?? CCM mmekwisha mwaka huuu hamna chenu tena.
 
huu muda mnaoutumia kudanganya watu ndio utakaowacost chadema, hamna kitu kama hicho hapa arusha!
Kisu kunako nyama huuma sana. Karibu tarehe 1 tusheherekee wewe kuvuka mpaka na kuacha wale wa kijani na njano. WELCOME HOME
 
Back
Top Bottom