Mbowe ataka uchunguzi kifo cha kiongozi wa CHADEMA, Daniel John

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
pic+mbowe.jpg

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13,2018 amesema John alitoweka siku moja iliyopita.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.

Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi kesho Februari 14,2018. Mbowe amesema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari.

Mbowe amesema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi.

Amesema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito.

Kuhusu Mallya amesema alipigwa panga kichwani na alivunjwa mkono. Mbowe ametaka polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Mallya aliyekuwapo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari amesema walikuwa wakitembea na John ndipo waliposimamishwa na kuingizwa ndani ya gari.

Amedai alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipozinduka alijikuta ufukweni alikojikokota hadi barabarani ambako alipata msaada wa bajaji na alikwenda Hospitali ya Mwananyamala alikotakiwa kuwa na taarifa ya Polisi ambayo aliipata Kituo cha Polisi Oysterbay.


Chanzo: Mwananchi
 
Inawezekana ni CHADEMA ndio wapo nyuma ya hili....
Hapa kuna maswali ya kujiuliza sana......Why Daniel John na Mallya afu apone Mallya
Kwanin Kifo cha John kiwe kwenye Senario ambayo imekuwa IKIPIGIWA KELELE SANA na ikiwahusisha USALAMA.......Hapa ni mchezo umechezwa...Eti mwili umeokotwa ufukweni.....
Kwanini MBOWE kajiwaisha sana kwenye MEDIA......as if ni mtu ambaye alikuwa anajua mchezo mzima
Mbowe pona pona yake ya UENYEKITI ni kushinda jimbo la KINONDONI sasa haya matukio ya mauaji ni KUTAFUTA huruma.....
Mbowe hii lazima na wewe uchunguzwe..........
 
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi: Kiongozi wa CHADEMA ambaye ni katibu kata, kata ya Hananasif, jijini Dar Es Salaam, ndugu Daniel John, amepatikana akiwa amefariki dunia.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 13-2-2018, Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe, amesema Daniel John alipotea siku moja iliyopita.

Mbowe amesema, walitoa taarifa polisi, na walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi.

Mwili huo ulitambuliwa na mke wa marehemu (John) na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kushiria alipigwa na kitu chenye uzito.

Reginald Mallya, ni mtu ambaye alikuwa na marehemu kwa mara ya mwisho, na anadai alijikuta ufukweni mwa bahari.

Akitoa ushuhuda, Mallya amesema walikuwa wakitembea pamoja na marehemu na walisimamishwa na kuingizwa kwenye gari. Anasema alipigwa hadi kupoteza fahamu, na alipozinduka, alijikuta ufukweni mwa bahari ndipo akajikokota hadi barabarani ambapo alipata msaada wa bajaji na alikwenda hospitali ya Mwananyamala ambako alitakiwa kuwa na taarifa ya polisi ambayo aliipata kituo cha polisi Oysterbay.

Kamanda wa polisi, kanda ya Dar Es Salaam Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hiyo, lakini anawasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni

Chanzo gazeti la Mwananchionline
Mbowe ataka uchunguzi kifo cha kiongozi wa Chadema
 
Back
Top Bottom