Mbowe ataka JK avunje baraza la mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe ataka JK avunje baraza la mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jul 18, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sunday, 17 July 2011
  Geoffrey Nyang'oro


  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amemshauri Rais Jakaya Kikwete kuangalia upya baraza lake la mawaziri kutokana na hili lililopo sasa kugawanyika.

  Kauli hiyo ya Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni inakuja wakati ambao Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, akiwa juzi ameonyesha msimamo hadharani kutaka Serikali iwaombe radhi Watanzania kutokana na mgawo wa umeme.

  Pia, Sitta ametaka wahusika wachukuliwe hatua, msimamo ambao umetolewa katika kipindi ambacho Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akiendelea kukaangwa Bungeni kuhusu mgawo huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema kitendo cha viongozi wa ngazi za juu Serikalini wakiwamo mawaziri kutofautiana hadharani kunaonyesha wazi kuwa Serikali imepoteza uhalali wake.

  Tayari, Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe walishawahi kuingia katika mvutano wa wazi na mawaziri Ngeleja na Mathias Chikawe ( Ofisi ya Rais Utawala Bora), kuhusu uhalali wa tuzo ya Sh 94 bilioni kwa Kampuni ya Dowans.

  Jana, Mbowe akirejea kauli ya Sitta aliyoitoa mkoani Mbeya juzi kuhusu matatizo ya umeme nchini, alisema, "Waziri wa Nishati na Madini (Ngeleja) anatoa kauli, mwenyekiti wa kamati ya Bunge ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti ya chama (CCM) anatofautiana nayo, mbaya zaidi anakuja waziri naye anatoa kauli inayoshutumu Serikali yake.

  Kwa mtindo huu, ni dhahiri Serikali imepoteza uhalali wake,"alisema Mbowe na kuongeza:

  "Tunamtaka Rais (Kikwete) atafakari upya baraza lake la mawaziri na kisha kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuliwajibisha, kama waziri anayeingia kwenye kikao cha baraza la mawaziri anatoka nje na kutoa kauli inayotofautiana na uamuzi wa baraza zima, hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali hiyo imegawanyika."

  Akisisitiza, Mbowe alisema mawaziri ndio wanaotegemewa kutoa taarifa juu ya mipango ya Serikali ya kushughulikia matatizo yakiwa mgawo wa umeme na kueleza kuwaa kitendo cha wao kutofautiana ni hatari kwa taifa.

  Alionya kuwa kitendo hicho kinaonyesha wazi kuwa Serikali haina mkakati wa kutatua tatizo hilo na kuongeza kuwa, ukimya huo ni hatari na unaweza kuliingiza taifa kwenye vurugu.

  Katika mkutano huo, Mbowe alisema kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana ilitarajiwa kujadili kwa kina suala hilo la mgawo wa umeme unaoendelea nchini kote na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua katika kukabiliana nalo.

  Alionya kwamba, kama Serikali haitachukua hatua za kusudi za kuonyesha namna ya kutatua tatizo hilo, basi nchi itadhurika.Alieleza kuwa mgawo huo wa umeme umeliathiri taifa kwa kiwango kikubwa kutokana na kuendelea kuporomoka kwa uchumi."Hivi sasa viwanda vingi nchini vinafungwa, vijana wengi wanapoteza ajira, taifa linaporomoka kiuchumi na wakati huo huo Serikali haina majibu yanayoonyesha dhamira ya kweli ya kumaliza tatizo hilo,"alieleza.

  Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema chama chake kimeamua kuliwasilisha suala hilo la mgawo wa umeme pamoja na mambo mengine kwenye kamati kuu ili wazee washiriki kulijadili na kutoa msimamo wa pamoja wa hatua za kuchukua katika kupambana nalo.

  "Tumewasilisha hilo kwenye kamati kuu ili wazee watupatie mwelekeo na kesho (leo), tutakwenda na tamko letu Bungeni linaloonyesha msimamo wa chama kama hawatatusikiliza tutaliwasilisha kwa wananchi,"aliongeza.

  Alisema hadi sasa mgawo huo umevuruga mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano ulioandaliwa na Serikali ukielekeza kuwa uchumi ungekuwa kwa asilimia 7.2 kwa mwaka, na badala yake umeporomoka hadi asilimia 5.8.

  Aliongeza kuwa tangu mgawo huo umeanza takribani Sh 1 trilioni zimepotea, hali inayoendelea kuporomosha uchumi wa taifa ambalo ni miongoni mwa nchi maskini sana za Kusini mwa jangwa la Sahara.

  "Sisi (Chadema) tumeshauri hata kwenye hatuba yetu ya kambi ya upinzani kuwa iundwe task force (kikosi kazi) kitakachohusisha wabunge, wataalamu na watu wa kada mbalimbali ili kutafuta chanzo cha tatizo hilo na kuja na njia mbadala ya kutatua kero hiyo,"alisema Mbowe.

  Mwanasiasa huyo aliweka bayana kwamba Tanzania ni nchi yenye rasimali nyingi na haistahili kukabiliwa na kero kama hiyo inayoendelea hivi sasa .

  Katika hatua nyingine, Mbowe alieleza kuwa kamati kuu pia iliyoketi jana ilitarajiwa kumjadili Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, kutokana na kitendo chake cha kutofautiana na msimamo wa wabunge wa chama hicho Bungeni.

  Akizungumza hilo, Mbowe alisema kamati hiyo itakaa kujadili hilo na kutoa maamuzi leo kwa namna itakavyoona inafaa.

  "Chadema ni chama kinachofuata katiba yake, kinafanya maamuzi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zake, ieleweke kuwa maamuzi ya kamati siyo ya Mbowe, bali ni ya chama,"alieleza na kuongoza:

  "Tunaleta hoja hizo huku kwa wazee wetu ili waweze kujadili na kutoa msimamo, maamuzi siyo yangu ( Mbowe) ni ya kamati kuu. Kitu cha msingi ni kwamba chama bila nidhamu siyo chama, nasi ndani ya Chadema kuna taratibu zetu."

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kikao hicho pia kilikaa kujadili ripoti ya madiwani wa Arusha wanaodaiwa kukiuka taratibu za chama na kuingia mwafaka na wenzao wa CCM bila ridhaa ya chama hicho. Mwafaka huo umesababisha mtafaruku ndani ya chama hicho, kiasi cha kulazimisha kuunda kamati maalum ya uchunguzi chini ya Mabere Marando, ambayo imechunguza na kuwasilisha mapendekezo yake chamani, ambayo yalitarajiwa kujadiliwa jana.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,883
  Likes Received: 83,366
  Trophy Points: 280
  Lipumba ashangilia Rostam kung'atuka

  • Lema asema kuondoka kwake ni matunda ya CHADEMA

  na Waandishi wetu
  Tanzania Daima


  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kung'atuka kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga Rostam Aziz (CCM) ni furaha kwa kambi ya upinzani na kwamba siasa ya Tabora kwa Chama cha Mapinduzi(CCM) sasa basi.

  Profesa Lipumba alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho na kueleza kwamba mbunge huyo alikuwa nguzo ya ushindi wa CCM mkoani Tabora na kusambaratisha upinzani.

  Akifafanua namna Rostam alivyopigana kuhakikisha majimbo ya uchaguzi Tabora yanaongozwa na CCM alitoa mfano wa aliyewahi kuwa mbunge wa Bukene, Tedy Kaselabantu (UDP), alivyokihama chama chake kwa nguvu ya Rostam na kurejea CCM.

  Alimtaja mwanachama mwingine kuwa ni Abdalah Fundikira aliyekuwa muasisi wa chama cha UMD naye alihama chama hicho na kuhamia CCM.

  Alisema Rostam alikuwa pia na nguvu kubwa katika chaguzi mbalimbali ambapo hata katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho uongozi wote hadi mtu amtake yeye ndipo ashinde. "Kwa kweli ni uamuzi mzuri ambao Rostam ameuchukua kwa upande wa upinzani maana kutokana na nguvu yake kubwa hata mwanachama mwingine ndani ya CCM alikuwa hawezi kupata nafasi hata wa upinzani alikuwa hawezi kupata nafasi ingawa chama cha CUF kilijitahidi kusimamisha mgombea ambaye alipata kura 11,000 jambo ambalo lilionyesha kuwa na ujasiri licha ya kuwa alikuwa maskini," alisema Profesa Lipumba.

  Tatizo la umeme

  Kuhusu suala hilo, Profesa Lipumba alisema kuwa tatizo la umeme ni janga la kitaifa kwa sasa hivyo amewataka Watanzania kujiandaa na anguko la uchumi kutokana na tatizo la umeme linaloendelea nchini.

  Kwa mujibu wa Profesa Lipumba ambaye ni mchumi, takriban Watanzania wote wanatumia nishati ya umeme katika kujiingizia kipato hivyo tangu kutokee kwa tatizo la umeme maisha ya Watanzania wengi yatakuwa duni hivyo aliwataka kujiandaa kwa anguko la uchumi linaloinyemelea nchi.

  Mwenyekiti huyo alisema hatma ya nchi kwa sasa inakokwenda ni kubaya na kwamba tatizo la umeme lilianza tangu mwaka 2006 lakini hadi sasa serikali imekuwa ikisuasua na miradi yote inayozungumzwa na serikali kuwa si ya uhakika.

  Alisema serikali haina mipango wala mkakati wa kuwaondolea tatizo la umeme Watanzania huku akitolea mfano serikali ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 300 kutoka Mtwara Mnazibay ambayo imezungumzwa lakini haijaingizwa pia katika grid ya taifa na kwamba hadi leo haijafanyika hivyo.

  Alisema serikali pia imeshindwa kutumia maporomoko ya maji kutoka sehemu mbalimbali ambayo yangesaidia kufua umeme wa megawati 300 na kuwaondolea wananchi adha ya kutokuwa na umeme.

  Alisema serikali haina mkakati wa kweli kutatua tatizo la umeme akatolea mfano pia katika miradi ya uzalishaji umeme Kinyerezi akisema ni mwaka wa tatu sasa serikali imekuwa ikiizungumzia lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.

  Profesa Lipumba alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuzingatia mapendekezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba(CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, kuhusu mikakati mbalimbali ya kutatua tatizo la umeme nchini.

  Alisema inaonekana dhahiri kuwa tangu January alipokuwa katika ofisi ya Ikulu alikuwa akimshauri Rais mambo mengi ya msingi lakini amekuwa akipuuzwa hali ambayo inaendelea hadi sasa.

  "Serikali inatakiwa kusikiliza mapendekezo ya January Makamba lakini sio ya Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja ambayo hayana tija na wala hayatekelezeki jambo ambalo linawafanya Watanzania kuishi bila furaha," alisema Lipumba.

  Alisema mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010 alimkabidhi Rais Ilani (manifesto) ya chama chake ambayo ilikuwa na mapendekezo ya kutaka kuundwa kwa bodi mpya ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na katika mapendekezo hayo alitaka igawanywe katika makampuni matatu ambayo ni uzalishaji wa umeme, usambazaji wa umeme na ukusanyaji wa fedha katika masoko mbalimbali.

  Alisema endapo TANESCO itakuwa na mfumo huo kutakuwa na uhakika hata wa kujiendesha kwa kuwa itakuwa inakusanya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali ambao ni watumiaji wakubwa na wadogo wa umeme.

  Ugonjwa wake

  Akizungumzia ugonjwa wake Lipumba alisema tayari ameshafanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la mshipa unaounganisha figo na bandama lililokuwa likimkabili.

  Alisema anamshukuru Mungu kupona salama lakini alieleza kushangazwa na taarifa alizozisikia kupitia vyombo vya habari kwamba alikuwa mahututi.

  "Mimi nilikuwa nasumbuliwa na mshipa unaounganisha figo na bandama na tayari nimeshafanyiwa operesheni na kwamba sijawahi kuwa mahututi hata siku moja na sasa nimekuwa mzima wa afya," alisema Profesa Lipumba.

  Alisema kuwa hata hivyo licha ya kufanyiwa operesheni hiyo nchini India ameambiwa asifanye kazi nzito kwa muda wa mwezi mmoja ili afya yake iendelee kujiimarisha zaidi. Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari viriripotiwa kuwa mwenyekiti huyo wa chama pamoja na Waziri wa Maji ambaye pia ni mbunge wa Rungwe, Profesa Mark Mwandosya, walifanyiwa upasuaji katika hospitali moja nchini India ijulikanayo kama Apollo iliyopo mjini Hyderabad.

  Mtikila na Rostam

  Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ameitaka CCM na serikali yake kutoridhika kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), badala yake imtafute popote alipo na kumfikisha mahakamani kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema hatua hiyo imetoa fursa kwa CCM kuhakikisha wanamfungulia kesi Rostam, kutokana na sakata la kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ambayo ilichota mamilioni ya fedha kupitia akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kinyume cha sheria.

  Alisema hatua ya CCM kuanzisha dhana ya ‘Kujivua Gamba' bado haina nguvu kutokana na serikali yake kushindwa kuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha kunakuwepo na misingi imara ya kidemokrasia kuliko ilivyo sasa.

  "Pamoja na Rostam kujiuzulu, bado Watanzania wanajiuliza je na mtandao uliomwingiza madarakani Rais Kikwete, umevunjwa au ndio wamemtoa Rostam kafara halafu wanasikilizia upepo kwa Watanzania namna gani watachukua hatua?

  "Bado kuna ombwe kubwa la uongozi ndani ya CCM na hata serikalini, kutokana na kutokuwa na uzalendo uliotukuka kwa viongozi wetu wa sasa na kwa hili sitaogopa kukamatwa na katu sitanyamaza hadi mbele za Mungu," alisema Mchungaji Mtikila.

  Alieleza kuwa sambamba na hatua hiyo, bado kuna kundi la wana mtandao wapo katika harakati za kuhakikisha Lowassa anakuwa Rais wa nchi katika awamu ijayo huku wakisahau misukosuko iliyompata wakati akiwa Waziri Mkuu hivyo kusababisha ajiuzulu.

  Pamoja na mambo mengine, Mtikila alitangaza rasmi kupeleka maombi Umoja wa Maifa (UN) ya kutaka Tanganyika kuwa taifa huru kuliko ilivyo sasa ambapo inaendelea kunyonywa na upande wa pili wa nchi (Zanzibar).

  Alisema tayari ameshawasiliana na wanasheria wake kwa ajili ya kuandaa hoja za kisheria ambazo ataziwasilisha mapema mwaka huu mbele ya vikao hivyo vya UN. "Katika hili kuna baadhi ya viongozi wa CCM, ninashirikiana nao na wengi wao wameahidi kunipa kila aina ya mchango ili kutimiza lengo hili na DP; tutasimama nalo hadi hatua ya mwisho … na kama kuna Watanzania wanataka kuniunga mkono kwa kunichangia nawakaribisha kwa moyo wao wa kuidai Tanganyika yao iliyo huru," alisema Mtikila.

  Lema na Rostam

  Akizungumzia kujiuzulu kwa Rostam, mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alisema hayo ni mafanikio ya CHADEMA kwa kuwa yaliyoshuhudiwa katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam baada ya kutajwa mafisadi 12 yameanza kutekelezwa.

  "Watanzania walipotajiwa mafisadi 12 katika taifa hili na kutakiwa kuwajibika walibisha; sasa leo wameanza kuingia mitini, waondoke sisi tuchukue jimbo letu ili tuwe wabunge 49 mjengoni," alifafanua Lema.
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  'Bush Lawyer' Mtikila anaenda kupingana na Mkataba wa Kimataifa wa Muungano kwenye Chombo Cha Kimataifa, si mchezo!
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hizi ni habari mchanganyiko? Mbona stori mbili zimeletwa kwenye thread moja?
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Mimi napata raha sana hawa wajinga wajinga wanavyonyukana hadharani.Na hapa ndiyo ukilaza wa JK unapodhihirika wazi, yaani waziri kutoka kwenye baraza lake la mawaziri anaipiga madongo serikali na yeye yupo anakenua kenua mijino yake, hata angekuwa mzee Ruxa na upole wake lazima angewafukuza kazi Sitta na Mwakyembe, kweli JK ni kulu daba.
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  NAAAAAAAAAAAAAM CDM NGOMA YAKE WATU WAZIMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kwa kuwa nyakati usema CCM yaaitaji watu wanaofikili kwa haraka sana na kutenda kwa haraka sana.Ukweli ni kuwa CCM iliitaji na yaitaji kufanya mabadiliko ya baadhi ya Mawaziri hili kuondoa wale ambao WALIPANDIKIZWA na hivyo kugeuka kuwa KIKWAZO CHA MAENDELEO WAKIHANGAIKA KUMTUMIKIA ALIYEWAFIKISHA HAPO WALIPO BADALA YA KUMSIKILIZA ALIYEWAPA MAMLAKA HAYO.

  Kwa kujua kuwa ni lazima JK alitikise Baraza lake Chadema wameichezea shilingi ya CCM kwenye tundu la choo.Maamuzi yoyote sasa hivi ya kubadilisha Baraza la Mawaziri itakuwa ni NGOMA ILIYOPIGWA NA CDM.Lakini ukweli CCM wangeicheza wao mapema pasi Mlio wa Sauti ya Ngoma ya Chadema.Lakini kwa kuwa walijitia Pamba masikio leo itabidi kuicheza kwa Mwangi.Na hivyo kuzalisha maono kwenye jamii kuwa CCM wanafuata Maagizo ya CDM.Na wananchi wa sasa sio wa mwaka arobaini na saba mbongo zao zinakopi watafika sehemu wanahalalisha maamuzi ya CDM kufumba na kufumbua CCM Itakuwa chali.

  Lakinii yote hiyo ni picha ya tabia ya CCM kutokwenda na wakati mpaka ukweli unapojili.Ukweli CCM ilipaswa kufanya mabadiliko na kuteua viongozi wengine siku nyingi sana.Lakini kwa kuwa HAWANA CHA KUPOTEZA sasa inabidi waonekana kana kuwa wamefuata maagizo ya CDM.

  HONGERA CDM ni MWANZO MZURI KITAELEWEKA!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Lakini mlitaka hawa wajinga waongee nini Mbeya zaidi ya kujichongea wenyewe, Mbeya si Kama kwa watani wangu wa Dodoma, Shinyanga, Pwani, Mtwala huko mbeya kunawatu wanafikilia sana wakuu lazima mkubali tuu! Ila JK nae kazidi sasa kama anadhani anajenga chama ndo anazidi kubomoa!
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  mwenyekiti wa wa CHADEMA, Freeman MBOWE anamshauri JK kuangalia upya baraza lake la mawaziri, Naomba ninukuu gazeti la mwananch la 18.07.2011 uk4, "tunamtaka Rais atafakari upya baraza lake la mawaziri na kisha kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kiliwajibisha, kama waziri anaeingia kwenye kikao cha baraza la mawaziri anatoka njee na kutoa kauli inayotofautiana na uamuzi wa baraza zima, hiyo ni ishara tosha kuwa serikali hiyo imegawanyika"
  my take: hoja mawaziri kutoa kauli inayotofautiana na uamuzi wa baraza zima.... Shibuda alitoa kauli inayotofautiana na wabunge wote wa chadema kuhusu posho- mpaka sasa hakuna hatua aliochukuliwa, JE shibuda kutoa kauli tofauti ni ishara tosha kuwa CHADEMA imegawanyika?
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  bado haijafika hata saa nne kwa saa za huko tanzania....anza kwenda hosptali kupima malaria....kikao cha kamati kuu kimeamua nini jana juu ya shibuda...wakati unaenda hosp pita kwnye vibanda vya magazeti usome....
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  AIsee
  kamati kuu kumuundia kamati ya kumchunguza SHIBUDA ndio HATUA? toka Mnyika apendekeze kwa KK juu ya shibuda So kuunda TUMe ndio hatua? toka Shibuda alopoke ni hatua gani amechukuliwa? tume si hatua... So kwanini asingemshauri Rais aunde tume ndogo kufatilia kama yeye alivyofanya?
  My take Shibuda ang`olewe
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu tolerance ya chama kwa kiongozi waliyetofautiana ni tofauti na ya serikali! Waziri anaongoza sekta nzima kwenye nchi na kutofautiana na wenzake ni kuonesha wazi kabisa kwamba hata malengo yao ni tofauti jambo ambalo linaathiri utekelezaji wa majukumu waliojiwejea. Halafu waziri yeyote anapoongea jambo lolote inakuwa ndio kauli ya serikali tofauti na kwenye chama. Kutofauti ni sawa na wewe kutofautiana na utendaji wa mkono kwenye mwili wako!
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  craaaaaaaaaaaaaaaaap
   
 13. K

  Kalambo Junior Senior Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ulevi ni mbaya sana!
   
 14. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kuna 'ministerial responsibility' ambapo mawaziri wote hutakiwa kuwa na kauli moja, hii ni tofauti na kutofautiana kwenye vyama. Waziri akitofautiana na wenzie ni lazima ajiuzulu kama alivyofanya lyatonga miaka ya 90. Chadema haina mawaziri, hata mawaziri vivuli shibuda si mmoja wao. Hata wasipomchukulia hatua haitakua kwamba chama kimegawanyika. au unataka kusema msimamo nape na lowassa ni sawa?
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Ishu ya Shibuda na ishu ya mawaziri ni ishu mbii tofauti. Hata athari zake ni mbili tofauti. Uwe unajaribu kutumia akili japo kidogo, ukitumia makalio kufikiri ndo unaleta upupu kama huu
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hili jambo lilifafanuliwa vizuri sana na Dr Slaa jana taarifa ya habari saa 2 usiku. sasa wewe umeamka hujapata hata ghahawa hujafanya hata uchunguzi nini kinaendelea umekimbilia kubonyeza keyboard hahaa haaaaa........ Great Thinker

   
 17. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha ulevi hapo huyo jamaa amesema kweli huwez kutoa soln ya tatizo kwa mwenzio wakati nawe una tatizo kama hilo. Kama mnakumbuka muafaka wa Arusha kama isingekuwa hapa JF Kupiga kelele ule muafaka ungeendelea na hata baadhi yenu mlishaanza kuukubali.
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Popo vipi aisee asubuhi yote hii ...?
   
 19. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Edson hii nimeipenda sana,

  Lakini pia Pompo anapaswa kuelewa kuwa waziri huwa anakula kiapo/anaapishwa ikiwa ni pamoja na:
  1. kulinda katiba
  2. kutotoa siri za baraza la mawaziri na hapa ndipo collective reponsibility inapokuja
  3. utii kwa Rais

  Ni wazi haiwezekani Shibuda-mbunge anayelindwa na kanuni za Bunge alinganishwe na waziri ambaye ni mwakilishi wa mkuu wa nchi na ameapa utii kwake.
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hivi katika vile vigezo vya Kitila Mkumbo, wewe ulipata alama ngapi?
   
Loading...