Mbowe apata wapinzani zaidi

Mbowe apata wapinzani zaidi

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Wanachama wawili zaidi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti wa taifa wa chama hicho inayotetewa na mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda, Benson Kigaila, aliwataja wanachama hao kuwa ni Daniel Ruvanga na Garambenela Frank.

Kabla ya kufungwa kwa zoezi la kuchukua na kurejesha fomu katika siku ya mwisho jana, mwanachama pekee aliyekuwa amechukua fomu kuchuana na Mbowe alikuwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora, Kanza Mbarouk.

Wakati akitangaza kutetea nafasi yake Alhamisi baada ya kuchukuliwa fomu na wazee wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali ikiwamo ya Kigoma, Rukwa na Njombe, Mbowe aliwahamasisha wanachama wenzake wa Chadema kwa kuwaambia kuwa wajitokeze kuchuana naye katika kuwania nafasi hiyo.

"Nimefanya kazi yangu kwa kujiamini sana, bila ya usalama wala ulinzi wa yeyote bali ulinzi wa Mungu, nawaheshimu wote wakubwa kwa wadogo, ila katu simuogopi yeyote na ndiyo maana nimekifikisha chama hapa," alisema Mbowe baada ya kupokea fomu ya kutetea nafasi yake aliyokabidhiwa jijini Dar es Salaam na mmoja wa wazee hao, Yassin Mzinga kutoka Kigoma.

Kigaila hakueleza kwa kina wasifu wa Ruvanga na Frank ambao walijitokeza katika siku ya mwisho jana kuchuana na mwenyekiti wao Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Kigaila alisema kabla ya zoezi la kurejesha fomu kufungwa katika siku ya mwisho jana, tayari wanachama 284 walikuwa wamesharejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Alisema katika nafasi nane za ujumbe wa Kamati Kuu, wanachama 58 walikuwa wameshajitokeza, miongoni mwao wakiwa ni Profesa Mwesiga Baregu, Mabere Marando, Chiku Abwao, Ansbert Ngurumo, Fredy Mpendazoe, Suzan Kiwanga na Mathayo Torongey.

Alisema kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, walioomba ni Profesa Abdallah Safari, Mussa Mabao, Martha Noah, Humprey Sambo, Winston Kulinda, Fredy Mpendazoe na Yeremiah Maganja.

Kigaila aliwataja walioomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar kuwa ni Said Mohamed Issa, Hamad Mussa Yusuf na Zainabu Mussa.

Alisema wanachama walioomba kugombea nafasi za makundi ya Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) ni 98, Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) ni 81, kundi la wazee 42 na wenye umri kati ya miaka 36 hadi 49 ni 63.

Kigaila aliwatahadharisha wanachama watakaoteuliwa kugombea nafasi walizoomba kutojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni. Uchaguzi Mkuu wa Chadema unatarajiwa kufanyika Septemba 14.

CHANZO: NIPASHE
 
Go go go cdm nendeni mkaonyeshe kwa vitendo nini maana ya demokrasia.
 
Safi, hii ni ishara ya kukua kwa demokrasia ndani ya chama, kuna vyama vingine mwenyekiti haruhusiwi kupingwa.
 
Kumbe cdm kuna usanii !!!! kwa makamu mkt sina doubt ni ushindani wa kweli lkn kwa mkt hapo mbowe ametuhadaa kwa unyeti wa kiti hicho tulipaswa kuona majina ya vigogo wanaojulikana kutoka chamani wakishindana na mbowe kama marando, lissu, mnyika na wengineo wengi ili tuone demokrasia ya kweli vinginevyo kuna kuogopana hapo au kama nimpango wa kukinusuru chama kwa uchanga na viongozi wote mlikubaliana kwa vikao vya siri it is fine vinginevyo kwa nafasi ya juu hakuna ushindani hapo
 
Chama cha kifalme kisicho na ukomo wa uongozi......ebu tafakari mrema mpaka leo mwenyekiti mbatia mpaka leo mbowe ndo usiseme au uchaga ndo tatizo nin
 
Ruvanga na Garambanela ni maboya tu na ndio watakaopitishwa.Mtu wa mwisho kurudisha fomu alikuwa mwenyekiti wa Tabora ambae hatajwi kabisa katika taarifa ya Kigaila.
 
Hii itakuwa imekata vilimilimi vya wanazi wa ACT na baba yao CCM. Tuone sasa watasema nini.o
 
Safi, hii ni ishara ya kukua kwa demokrasia ndani ya chama, kuna vyama vingine mwenyekiti haruhusiwi kupingwa.
Wewe unaumwa, mngemuacha ZITTO muone kama wangeruhusu Mbowe Kupingwa
 
Ruvanga na Garambanela ni maboya tu na ndio watakaopitishwa.Mtu wa mwisho kurudisha fomu alikuwa mwenyekiti wa Tabora ambae hatajwi kabisa katika taarifa ya Kigaila.

Umesoma kweli au una lako jambo !!?mwaka huu mtakufa na vijiba vya roho.
 
Wewe unaumwa, mngemuacha ZITTO muone kama wangeruhusu Mbowe Kupingwa

Nani kamzuia kuchukua fomu!?? Hujui fomu zilikuwa mpaka kwenye mtandao ?!! Mwaka huu mtaharisha changarawe.
 
Kumbe cdm kuna usanii !!!! kwa makamu mkt sina doubt ni ushindani wa kweli lkn kwa mkt hapo mbowe ametuhadaa kwa unyeti wa kiti hicho tulipaswa kuona majina ya vigogo wanaojulikana kutoka chamani wakishindana na mbowe kama marando, lissu, mnyika na wengineo wengi ili tuone demokrasia ya kweli vinginevyo kuna kuogopana hapo au kama nimpango wa kukinusuru chama kwa uchanga na viongozi wote mlikubaliana kwa vikao vya siri it is fine vinginevyo kwa nafasi ya juu hakuna ushindani hapo

Vipi kwa upande wa CCM yenu uliisha wahi kuona nafasi ya Mwenyekiti Taifa ikishindaniwa na mgombea zaidi ya mmoja? au mmejipa upofu na kujiondoa akili sababu tu mpo CCM.
 
Kumbe cdm kuna usanii !!!! kwa makamu mkt sina doubt ni ushindani wa kweli lkn kwa mkt hapo mbowe ametuhadaa kwa unyeti wa kiti hicho tulipaswa kuona majina ya vigogo wanaojulikana kutoka chamani wakishindana na mbowe kama marando, lissu, mnyika na wengineo wengi ili tuone demokrasia ya kweli vinginevyo kuna kuogopana hapo au kama nimpango wa kukinusuru chama kwa uchanga na viongozi wote mlikubaliana kwa vikao vya siri it is fine vinginevyo kwa nafasi ya juu hakuna ushindani hapo

jk alishindana na nani????
 
misukule ya lumumba povu la madawa ya kulevya povu kali linawatoka
 
Kuhusu nini mkui, kumpinga Mbowe?, mruhusuni na ZITTO muone moto wake

Zito ni mwehu,kiaina Zito na vibaraka wote wameelemewa na hujuma zao hazna nafasi tena!! Jamii imeshawatambua.....
 
Hao ni vibaraka wa mbowe, mpinzan wa ukweli ni Kansas Mbaruku
 
zito naye achukua fomu, tuone sasa ni nani nikisiki kweli kati yake na Mbowe!
 
Back
Top Bottom