Mbowe Aokoa Jahazi bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe Aokoa Jahazi bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Matola, Feb 11, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] Mbowe aokoa jahazi bungeni
  • Hoja yake yazima mvutano wa CCM, CHADEMA

  na Waandishi wetu, Dodoma


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, jana alitumia hekima kumaliza mvutano mkali wa hoja kati ya wabunge wa upinzani na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyowezesha kupitishwa kwa marekebisho ya mabadiliko ya katiba.
  Mvutano huo wa hoja ulisababishwa na hatua ya wabunge wa CCM kupinga pendekezo la kuwataka wakurugenzi wa halmashauri ndiyo wawe wasimamizi wa mikutano ya Tume ya Katiba itakayokuwa ikiratibu maoni ya mabadiliko ya katiba.
  Wabunge wa CCM ambao walionyesha wazi mwelekeo wa kuwa na ajenda moja walikuwa wakitaka wakuu wa wilaya ndiyo wawe na wajibu huo badala ya wakurugenzi wa halmashauri.
  Msimamo huo wa wabunge wa CCM ulikuwa ikipingwa vikali na wabunge wa CHADEMA ambao kwa maoni yao waliiona hoja hiyo ya kuwataka wakuu wa wilaya kuwa iliyokuwa ikilenga kukinufaisha chama hicho tawala.
  Akizungumza kabla ya Mbowe kusimama na kutuliza mambo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), aliita hatua hiyo ya wabunge wa CCM kuwa inayoibua mkanganyiko.
  Lissu katika hoja yake alisema wakurugenzi wa halmashauri walikuwa ni watu wenye uwezo na waliokuwa wanafaa kutumiwa na Tume ya Katiba badala ya wakuu wakuu wa wilaya ambao kupiganiwa kwao kunalenga kulinda maslahi ya CCM.
  Mvutano kuhusu hoja hiyo iliyokuwa ikigusa kifungu cha 17 cha marekebisho hayo ya sheria, ulianza juzi hatua ambayo ilisababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria na Katiba kabla ya kurejea na mapendekezo mapya jana.
  Hoja hiyo iliporudishwa tena bungeni jana ilikuja na mapendekezo ya kuwajumuisha wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kwa pamoja katika kazi ya kuratibu kazi za tume ya katiba.
  Kabla ya suala hilo kupelekwa katika Kamati ya Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema, alisema ili kila upande uonekane mshindi katika suala hilo, kifungu hicho kinapaswa kuwaruhusu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutumiwa na Tume ya Katiba, kuitisha mikutano ya maoni.
  Akisoma maafikiano ya kamati na pande husika jana, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Angela Kairuki (CCM), alisema wamekubaliana na marekebisho yaliyopendekezwa na AG, ya kuwekwa kwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri.
  Hata baada ya maoni hayo ya kamati, mvutano kati ya wabunge wa CCM na wale wa upinzani uliendelea kuwa mkali hadi pale, Mbowe aliposimama na kutoa kauli ambayo iliwatuliza wabunge anaowaongoza.
  “Wakurugenzi wa halmashauri ni watendaji wa serikali ya CCM, wanaosimamia shughuli za maendeleo ya wananchi…inasikitisha kuona kwamba wabunge wa CCM hawawaamini watumishi hawa wa serikali,” alisema Mbowe na kuongeza: “Wabunge wa upinzani tunalazimika kuweka rekodi kukubali marekebisho ya Mwanasheria Mkuu yapite…lakini utamaduni huu tunaojenga humu ndani, wa kufunika kombe mwanaharamu apite utatugharimu baadaye.
  “Wabunge wenzangu wa upinzani tukubali jambo hili limalizike kwa sababu lazima tufike sehemu tu-compromise (turidhie), twende tukatunge katiba ambayo itadumu zaidi ya miaka 100 bila kujali kuwapo kwa CCM au CHADEMA,” alisema Mbowe.
  Baada ya Mbowe kumaliza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Steven Wassira, alisimama na kumpongeza kwa kutumia hekima na busara kuwashawishi wenzake.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. A

  Ahakiz Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha wajidai tu lakini huu ndio mwisho
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kansa ya wingi wa wabunge wa CCM bungeni.
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,164
  Likes Received: 10,512
  Trophy Points: 280
  chezea watu na intelijensia zao...
  viva Mbowe , viva CDM.
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndio mwanzo wa CCM-C...
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaaani kwa kweli hawa jamaa huwa wanafanya home work zao sawa sawa sana ... i love them
   
 7. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  **** kitu sjaelewa, naomba fafanuzi..
  "kwamba consesus ni kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa wilaya wote watahusika au wakuu wa wilaya pekee?"
  Naomba msada.
   
 8. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye nyota umeandika matusi
   
 9. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  badala ya kuandika kuna akaandika ****
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Apology!
  sincerely ni chenga za keyboard. sikuinote. Samahanini JF.
  Naomba sasa mnijuze basi!
   
 11. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Hivi kwanini vagina inaruhusiwa lakini ukiandika kwa kiswahili inakuwa censored?
   
 12. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  naona labda kwa kiswahili linaumiza sana ila kwa kiingereza linaonekana la kawaida kwa sababu wote ni waswahili au labda kwa kiingireza ni sawa na ili neno ngojea ni andike kwa continuous tense badala ya simple tense ili unipate fresh nikiandika kwa simple linakuwa censored hebu angalia ****ing
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Maslahi ya taifa ni muhimu sana kuliko yale ya CCM na CHADEMA!
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  KUMAliza
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kingleza: vagina---invaginate
  Kiswazi: ku** ----Kumaliza
   
 16. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hii thread inabidi ianzishwe upya.
  Imekuwa chitchat
   
 17. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kwa mara ya kwanza nilimuona Aikael akiongea kwa HISIA KALI SANA mpaka nikaogopa. nilihisi anataka kufanya maamuzi magumu ya kutoka nje tena. Ila kiukweli alifanya swala la msingi sana maana Tundu alishawafanya kitu mbaya CCM na hali ya hewa ilishachafuka pale bungeni
   
 18. t

  tenende JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hili ni neno la kawaida isipokuwa si mahali pake wala si tusi.
   
 19. Wazo la kabwela

  Wazo la kabwela JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2013
  Joined: Feb 13, 2013
  Messages: 1,312
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Dj mbowe.
   
Loading...