Du mimi ni hii Signature yako tuu
unafanya ziara jimboni kwa helikopta halafu unawachangisha wananchi mia mia zao eti unajenga chama, wizi mtupu!!!!!!!!
yaani BABANGU nakomaGA kabisa kuijua Siasa kumbe ni biashara!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Abarikiwe sana Mwenyekiti Mbowe... Ingawa anaongoza mapambano ya CDM kuingia ikulu, lakini ni wazi kwamba ameongoza vyema harakati za upinzani nchini. Hata kama CDM haitaingia ikulu, au hata kama yeye hatashuhudia ikiingia ikulu, lakini historia itabaki kuwa alikuwa mmoja wapo wa viongozi mahiri wa upinzani aliyewahi kutokea Tanzania hadi sasa...
Nchi inakuwa na raisi mmoja tu kwa wakati mmoja, lakini inakuwa na viongozi wa vyama vya upinzani kadhaa wakati wowote... Kwa sasa, na kwa historia ya nchi hii, Mbowe ndiye kinara kati ya wenyeviti wa vyama vya upinzani zaidi ya 18. Pamoja na kuwapo na wenye elimu kubwa sana zaidi yake, Mbowe amewapiku wote na kudhihirisha kipaji kikubwa cha kuongoza alicho nacho.
Namuombea maisha marefu na afya njema, ili siku moja apate nafasi ya kushuhudia kwa macho yake mabadiliko yale ambayo amekuwa akitapigania.
Viva Mwenyekiti wa ukweli...
Mwnyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.
Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.
Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.
Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.
Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.
Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.
Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali.
Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe, alisema.
Kiongozi huyo alisema wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.
CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa, alisema.
Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.
Chanzo: Tanzania Daima
MY TAKE:
Hii inaonyesha siasa za Africa ni ngumu na nizakidhalimu maana watu wanaviziana h ata kwa kuuwana.
umaarufu wa Mbowe hauhitaji magumashi mengine , Lukosi hata ukichanganya umaarufu wa ukoo wako wote na majirani zenu , fufueni hata waliokufa , hamtaweza kufika hata robo ya umaarufu wa mbowe .
NTUZU kwetu ni ndoto za mchana MytopiaMtu ukimpa tisheti na kofia na akinamama ukiwapa Khanga ikifika siku ya kupiga kura hawezi kukupigia kura atakwenda kupiga atakwenda kuchagua atakapo! Yani huo ndo ukweli! Lakini mtu akikuchangia japo ata kama ni coin" siku ya uchaguzi lazima akamchague yule aliemchangia! Hawezi kabisa kuharibu kula Yake kwa kuchagua mtu tofauti huu ni Ukweli usiopingika ni sawa na kiongozi alieingia madarakani kwa kununua uongozi na kusapotiwa kifedha na matajiri, akiupata uongozi kazi Yake kubwa itakua ni kujilipa na kulipa fadhila za hao waliomuwezesha kupata uongozi na si kuwatumikia wananchi Na maslahi ya inchi! Hapo ndipo wanakuja sasa kua na majina ya Mafisadi na utawala usio wa haki sawa! Na kukandamiza wanyonge na kuzima sauti za watetezi wa haki kwa nguvu kwa kutumia dola na hata kumwaga damu! Tujaribu kuyatafakari maneno mazuri ya Waziri mkuu mstaafu Mh Fredriki Sumaye anayosema juu ya wanasiasa wanaoingia ikulu kwa fedha na Ndio hao wanaozuia wanasiasa wenzao wasiingie ikulu kwa mtutu wa Bunduki! Viva Chadema
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?
KIONGOZI hilo nalo neno, kuanzia kwa katibu na sasa m/kiti na Mbunge wa viti maalum Arusha wameoana na sasa bibi huyo yuko Dubai. Angalia mh. wewe kama kioo cha watu unafanya utumbo huo huoni noma. kweli tunaupinzani feki
I really find this message of Mbowe very confusing. Tumesikia eti hati gari lake ameandika maneno kama anaacha usia, au mtu ambaye ana hatimaya ya kuuwawa au kufa kimazingara.
Kufa ni wajibu, lakini hapa naona kama vile umma unatayatishwa kwa jambo fulani baya kinachojulikana na wachache ndani ya Chadema.
Huyu Bw anahitajika kupeleka ushahidi polisi lile bomu la arusha, kwa hivyo anajua kuna tegemeo la kushikwa na kufungiliwa hatia. so why not prepare the people by feeding them wrong information and win them to your side. Nina imani serekali imejiweka tayari na hata jiingiza kwenye huo mtego wa panya
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?