Mbowe anaidai AIR TANZANIA 2bn

Mbowe anaidai AIR TANZANIA 2bn

KirilOriginal

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2012
Posts
2,161
Reaction score
1,147
Hawa Ghasia alileta ghasia kumshambulia Mbowe kwamba anadaiwa na LAPF. Ghasia fahamu kwamba ni seriali yako unayoitetea ambayo Mbowe anawadai
2bn kupitia Air Tanzania.

Wamlipe kwanza Mbowe fedha zake.
 
Hawa Ghasia alileta ghasia kumshambulia Mbowe kwamba anadaiwa na LAPF. Ghasia fahamu kwamba ni seriali yako unayoitetea ambayo Mbowe anawadai
2bn kupitia Air Tanzania.

Wamlipe kwanza Mbowe fedha zake.

Mkiwa mna nia ya kutetea watu muwe composed sio kukurupuka tu!!!!!!!
Unaweka mazingira ya kuwa halipi sababu anadai serikali kitu ambacho sidhani kama una uhakika nacho!!!!!!

Unaweza dhani unajenga kumbe unabomoa!!!!
 
Mkiwa mna nia ya kutetea watu muwe composed sio kukurupuka tu!!!!!!!
Unaweka mazingira ya kuwa halipi sababu anadai serikali kitu ambacho sidhani kama una uhakika nacho!!!!!!

Unaweza dhani unajenga kumbe unabomoa!!!!
Maana yake ni kuwa, Wakisha net off ndipo Ghasia aje tena kujamba jamba
 
Mkiwa mna nia ya kutetea watu muwe composed sio kukurupuka tu!!!!!!!
Unaweka mazingira ya kuwa halipi sababu anadai serikali kitu ambacho sidhani kama una uhakika nacho!!!!!!

Unaweza dhani unajenga kumbe unabomoa!!!!

Unachokisema ni kweli.Kama amechukua mkopo si kosa kosa ni kutolipa!Lakini kama amechukua na amekwisha lipa kama alivyosema basi Serikali imlipe deni lake.

Sioni sababu ya kuvurugana.
 
Leta hapa na terms za mkopo

Mimi sio party katika mkataba huo kwa hivo sina hizo terms......

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.
Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.


Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo aliwai kuwa Waziri wa Fedha.Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.
Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.


Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.


Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.


Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.


Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.


NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.


"Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria," alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.


Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katika moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.


Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini
 
Hawa Ghasia alileta ghasia kumshambulia Mbowe kwamba anadaiwa na LAPF. Ghasia fahamu kwamba ni seriali yako unayoitetea ambayo Mbowe anawadai
2bn kupitia Air Tanzania.

Wamlipe kwanza Mbowe fedha zake.

Usiwe Condom, toa maelezo ya hayo madai ya Dj Mbowe!
 
kweli mikopo tanzania ni hatari

unakopa milioni 15

ndani.ya miaka 24 unalipa milioni 65

ila balance ya deni iliyobaki ni milioni 1,200

kazi kweli kweli
 
Kama kuna ukweli wa Mbowe kutotimiza ratiba ya malipo atakiwavyo na masharti ya mkopo - kwa nini hao NSSF wasichukue hatua za kimkataba badala ya kulalama? Hakukuwa na dhamana? Hakuna mahakama? Au ndio uongozi ulikula pasenti na ndiyo maana kuna kugwaya?
 
Maana yake ni kuwa, Wakisha net off ndipo Ghasia aje tena kujamba jamba

Hapana hauko sawa yaani unataka kusema kuwa halipi sababu hajalipwa!!!!!?????
Hii ni kwa mke na mume ndani sio pesa za taasisi......yaani mfuko ukonde kisa shirika/serikali haijalipa mdeni wa shirika kwani mchanganuo wa mkopo unahusisha yeye kudai kwingine!!!!??????

Kama ingekuwa hoja yako na mtoa mada ni kweli na ndio sababu hizo basi mnamuweka kwenye mzani juu ya dhamira na kuaminiwa kama kiongozi!!!!!!!

Naamini yeye asingewweza kusema kuwa halipi huku sababu na yeye anadai sehemu fulani!!!!!!
 
Unachokisema ni kweli.Kama amechukua mkopo si kosa kosa ni kutolipa!Lakini kama amechukua na amekwisha lipa kama alivyosema basi Serikali imlipe deni lake.

Sioni sababu ya kuvurugana.

Kwani serikali imesema haimlipi sababu na yeye anadaiwa na mfuko wa jamii?????!!!!!
 
Mbowe ameifilisi chadema sasa amehamia kwenye mifuko ya jamii inayoweka akiba za wastaafu..
 
Kwani serikali imesema haimlipi sababu na yeye anadaiwa na mfuko wa jamii?????!!!!!

Hapana sikuwa na maana ya kuwa sababu hajalipa basi serikali imekataa kumlipa,labda Kiswahili changu hakikueleweka vyema.

Ninamaana kwamba serikali inawajibika kumlipa na pia Mbowe anawajibika kulipa,na hata kama kampuni zake zilikopa basi aishinikize kampuni zake zilipe,ili atundee haki wanachama wa CDM kwa kulipa deni hilo.Maana wakati tunawaanyoshea vidole watani zetu CCM basi huku kwetu tuwe wasafi na weledi uliotukuka.Hivyo tu.
 
Mnajitahidi sana kumuosha Mbowe na matope!.

Kuna wengine wanajifanya watetezi wakati hata hawafamu kile wanachokitetea. Akili za kivyama ziwewakaa kwenye kope bila kufahamu kuwa Mbowe kwenye biashara zake hana vyama. Na kwa kutokuwa na vyama kwenye biashara zake, ndiyo maana kwake kwenda kunywa juice State House na dhifa mbali mbali za Kitaifa haimpi shida.

Mambo ya siasa tuyaache kwenye siasa kwa sababu tukianza kufungua a can of worms, hapatakalika.

Wajinga ndiyo waliwao!.
 
Back
Top Bottom