VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mbowe amewataka BAVICHA kutokuja hapa Dodoma na kuzuia mkutano wetu wa tarehe 23 mwezi huu. Kwakuwa Mbowe ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,BAVICHA watapaswa kutii na kutekeleza bila kujieleza.
Katazo la Mbowe lina mtego. Mbowe namjua. Ni mwanasiasa hasa. Kauli na matendo yake ya kisiasa,si ya kuyapongeza au kuyabeza kwa haraka zisizo na baraka. Mbowe amewatega watawala. Amewatega CCM. Anataka tumpongeze au kumuona ni muoga. Kwamba anatuacha tujidai tutakavyo.
Mbowe ni mwanasiasa mahiri,jasiri na mbunifu. Ameiva na kukomaa. Anajua kuwa kuachwa huru kwa CCM ni kuachwa huru wote. Anajua kuwa CCM tukifanya mikutano yetu,CHADEMA na wengineo hawatazuilika kufanya mikutano yao. Ni mahesabu ya kupata jawabu la kisiasa.
CCM hatutegeki kwa kauli ya Mbowe. Lakini,tuna hakika,atapata anachokilenga: mikutano huru ya kisiasa ya ndani na nje!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)