Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Masamila

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2014
Posts
6,506
Reaction score
7,472
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
 
Reactions: SMU
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Wataalamu wa sheria watusaidie kulifafanua hili. Sheria inamzuia mtu aliyetumikia kifungo, sijui hapa kwa mtu aliyelipa faini inakuwaje!
cc: Petro Mselewa
 
alimshambulia wakala wa CCM baada ya kuiba kura uchaguzi uliopita.ila sio lazima awe mbunge
 
Sidhani kwa sababu mwka juzi mbunge wa Mbarali( CCM) alihukumiwa kifungo au faini kwa kumpiga mkt wa kijiji alilipa faini na anaendelea kuwa mbunge.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977, kifungu cha 67(2)(c) kinasema;

Kwa kukusaidia zaidi, Katiba imeenda mbele zaidi kwenye kifungu cha 67(7)(b) na kusema,
''ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa badala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo hautahesabiwa''.

Changanua hayo maelezo na ulinganishe na hakumu!
 
Baada ya mahakama ya Hai kumuhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe kifungo cha mwaka mmoja au kulipa milioni moja baada ya kumshambulia msimamizi wa kituo cha uchaguzi kwenye jimbo la hai, sasa inaonekana uamuzi huo wa mahakama umemnyima usingizi kwani utamnyima fursa ya kuchaguliwa kuwa ama mbunge au rais. Hivyo amekata rufaa mahakama kuu kupinga uamuzi huo.
 
Mh.Rage kipindi cha FAT alikula mvua kadhaa

Alishinda rufaa iliyofuta ile adhabu japo alikuwa amekwisha toka kwa msamaha wa rais. Sasa Mbowe aanze mchakato wa rufaa leo nadhani itasikilizwa August na maamuzi yatatoka January. UKAWA ingejipanga tu kumsimamisha mgombe mwingine hapo Hai na Mbowe akimshika mkono hata Mbuzi anashinda.
 
Precedence ya mtikila Yeye alienda jela 1 year kwa uchochezi. Hakuwa na faini. Na aligombe urais. What matters, kwa katiba ya sasa.. mtikila hakufungwa jela/ wala mbowe hakuhukumiwa kwa utovu wa uaminifu; kwa kukwepa kodi wala kwa kuvunja maadili ya viongozi wa umma. precedence ya mtikila kwa lugha nyepesi ilitengeneza sheria ambayo inabidi ifuatwe kisheria inaitwa case law
 
mods huu uzushi hauvumiliki

cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Hivi ww mbugila wapinzani wakifanya kosa basi ndy inakuwa mwimbo wa taifa.
nyie magamba chenge ali fanya nini?
ndomana mnachezewaga vichapo ila hamkomi
 
Pole mtoa mada kwa ujinga ulip nao na kutushirikish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…