Waliomualika walikosea, walitakiwa kumualika LowassaWakuu,
Leo nilialikwa kwenye harambee ya KKKT dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Longuo - Moshi ambapo walikua na harambee ya ujenzi wa kanisa, na mgeni rasmi alitegemewa kuwa Mbunge wa Hai, Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Haikaeli Mbowe.
Lakini cha kushangaza, Mh. Mbowe hakuweza kuhudhuria harambee hiyo pamoja na kukubali kuwa mgeni rasmi tangu awali, na taarifa nilizopata ni kwamba Mh. Mbowe alitoa taarifa ya kutokuhudhuria siku moja kabla ya harambee bila hata ya kutuma muwakilishi.
Kwa kweli katika hili Mwenyekiti wangu ameni let down sana as I always believe that he is a man of his words!!
hivi angepataje muwakilishi ili hali alijiandaa mwenyewe kuja na akapata dharura, waandaaji hawajalalamika kwa vile walikuwa na plan bhapakuwa na haja ya kukubali kama alijua haji halafu kama alipata udhuru ghafla si angetuma muwakilishi? Kwa nini aliwaacha watu waliokua wanamtarajia njia panda?
hapakuwa na haja ya kukubali kama alijua haji halafu kama alipata udhuru ghafla si angetuma muwakilishi? Kwa nini aliwaacha watu waliokua wanamtarajia njia panda?
Babu Asprini heshima kwako.
Hivi mtu aliyekubali awali halafu anakujulisha Jumamosi kwamba hataweza kuhudhuria hiyo harambe ya Jumapili unamchukuliaje?
Unaweza kweli ukampata mgeni rasmi mwingine ndani ya muda huo. Try to be objective babu!
1. Wewe sio mlutheri....mfano alialikwa baba askofu Martine Shao kushiriki kwenye harambee lakini kutokana na kubanwa na majukumu alimtuma askofu mmojawapo wa dayosisi amwakilishe.....
achane kutetea ujinga, mtu akifanya vibaya aongelewe kwa ubaya wake, msilete ushabiki wa kitoto hadi mnajisifu kwa kutukana. Huyu jamaa ni kiongozi wa Nchi lazima atimize alichokubali kukifanya
1. Wewe sio mlutheri
2. Hii habari hata kama ni kweli utakuwa umesimuliwa na aliyekusimulia hukumwelewa sawasawa
3. Dayosisi huwa na askofu mmoja tu na nivigumu sana kwa askofu wa dayosisi kumpata askofu wa dayosisi nyingine KUMTUMA akamwakilishe kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa in absence ya askofu mwenyeji. Jipange upya dogo
Mambo yanayohusisha binadamu lazima kuwe na Plan B mkuu. Binadamu wakati wowote ule chochote chaweza kumtokea. Shughuli kubwa kama hiyo Plan B muhimu mkuu.
BTW sababu za Mbowe kushindwa kufika hazikueleweka au hazina mashiko?
Hujui kwamba pale dayosisi kuna maaskofu wawili wanaosaidianaga na askofu mkuu? Ngoja niwaulize wanaofahamu jina la askofu alokuja nitakwambia mkuu.
By the way mimi nilialikwa kama Mbowe, usharika wangu ni Kijitonyama mkuu.
Turudi kwenye topic, tunazungumzia Mbowe kukacha harambee!!