CUF Ngangari
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 273
- 51
ATETEA WAWEKEZAJI UTALII WAKATI ALIWAKATAA KADCO, MAMA KILANGO ACHACHAMALIA WENYE MAHOTELI.
Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambaye pia ni mbunge wa Hai Freeman Mbowe (chadema) amegeuka 'kinyonga'.
Mbowe aligeuka kinyonga jana kwa kuwatetea wawekezaji wakati akitetea maslahi ya Mlima Kilimanjaro ambako ndiko asili ya kwao. Mbowe alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma wakati akichangia bajeti ya maliasili na utalii ya mwaka 2011/2012 akiwa ametangaza MASLAHI YA BIASHARA YAKE YA UTALII PIA.
Mbowe ambaye ana hoteli ya kitalii kwao Moshi, alisema hali ya uchafu wa kinyesi inahatarisha afya watu wanaotunza mlima huo. Hatua ya Mbowe kuwafagilia wawekezaji katika sekta ya utalíi ilipokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wengi waliokuwa wanafuatilia mjadala wa bunge katika luninga wakimuona kinyonga. Walimwona kinyonga kwa kupalilia maslahi yake wakati aliwapiga vita wawekezaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) akitaka meneja mzungu aliyepo, aondolewe akidai anaitia KADCO hasara.
Mbowe alisisitiza mzungu huyo aondolewe akidai KADCO haitoi gawio katika Halmashauri ya Hai ambako ni jimbo lake la uchaguzi. Ni ukinyonga huo wa kutaka mwekezaji mzungu wa KADCO aondoke akidai wawekezaji hao hawana lolote, lakini mjadala wa jana ulizusha gumzo kuhusu mbowe na kumfanya aonekane kama kinyonga baada ya kuwafagilia wawekezaji wakiwamo wa nje akitaka waje wengi. Alifikia kiasi cha kukariri hutuba ya Baba wa taifa. mwl Julius Nyerere kuhusu uendeshwaji wa raslimali za taifa hasa utalii ya mwaka 1961 alisema ilitolewa siku nne kabla hajazaliwa.
Habari kamili soma JAMBO LEO. la 18 agosti 2011