Mbona wenye mamilioni ya chanjo bado wako lockdown na wanakufa

Mbona wenye mamilioni ya chanjo bado wako lockdown na wanakufa

una hoja nzito mleta mada na kwa nini hawaruhusu watu wao na ndege zao kwenda popote duniani wakati watu wao wamechanjwa? mbona ukipata chanjo ya homa ya manjano unaruhusiwa kwenda popote duniani?

Hii chanjo ni feki waruhusu waliochanjwa kuja Tanzania kutalii nk .Mbona mashirika yao ya ndege yako lockdown?

Waruhusu waliochanjwa kuja kutalii kama wanaamini chanjo yao
Hapo sasa
 
Waliochanjwa huko hawazidi hata 30% ya population yao. Kwa sasa hakuna mwenye uhakika nguvu ya hiyo chanjo inaisha lini ili mtu adungwe tena

Chukua tahadhari. Corona ipo na inaua vibaya
 
Mbona wenye Chanjo wako Lockdown na wanakufa?
Kwa maelezo yako haya ni kuwa hakuna haja basi ya kuwa na chanjo wala tiba au kinga ya magonjwa mengine kama malaria, pumu, vidonda vya tumbo n.k kwa kuwa tu wanaougua magonjwa hayo huwa wengine wanakufa/
 
Hakuna nchi iliyochanja watu wake wote duniani kwani zoezi bado linaendelea
Kuna nchi ndio kwanza robo ya population ndio wamechanja
Kweli bado watu wanakufa ila wamepungua sana
Kuchanja ni hiari sio lazima ila tunakoelekea itakuwa kusafiri ni lazima uwe na chanjo kama Saudia walivyoanza
 
Malengo ya chanjo hizi, ni nchi husika kuendelea kuwa vinara wa Uchumi duniani na Wala hawatajali athari ya wengine,

Swali moja tu!!

Maana ya chanjo ya gonjwa husika ni kuwa mtu aliyechanjwa Kwa namna moja ama nyingine hawezi tena kuambukizwa na hayo maradhi!!

Kwa nini iwe ni Lazima watu wote wachanjwe?

Kwa nini hata waliochanjwa Bado hawana uhakika wa kutokuambukizwa tena?

Kwa nini waliochanjwa hawawezi kuchangamana na wengine na bado wanavaa Barakoa na kujilockdown?

Chanjo hizi ni Nani ambaye atatwambia kuwa hazina uwezo wa kuulinda mwili usiambukizwe tena tukamwelewa ni Nani???

Wanaoziuza licha kuwa wamechanjwa,bado wangali wakivaa Barakoa, anayeuziwa eti anaamini atapona!!!

Haki ya Nani Africa inaporwa huku inajiona!!!

Ni kweli hatuna utaalamu Sana kujitengenezea tiba, Je, hata maswali ya kuwauliza watengemezaji hatuna??

Corona ni mtaji wa wawatu
 
Hii vita ya uchumi inashirikisha nani na nani?? Na sie TZ tumo?
hivi sasa mataifa makubwa yanasuguana juu ya matumizi ya chanjo ipi itumike,
Ujerumani hawataki, Ufaransa n.k,
kwa kifupi hawaaminiani kabisa juu ya suala la chanjo ya korona,
kwa kifupi tahadhari ni muhimi sana ktk suala la chanjo.
suala la chanjo ya korona bado ni jimbo linahitaji mjadala makini sio kukurupuka.
kuna hatari ya kulishwa matango pori.

Tujihadhari na chanjo ya kuletewa.
Tusikubali kuwa majaribio ya chanjo.

huenda hizi chanjo zinazotolewa hivi sasa kwa mataifa mengine madhara yake tutakuja kuyaona baada ya miaka 10 mpaka 15.

Chanjo za majaribio kwa wananchi wetu NO.
 
Hamjui chanjo ni kinga na wala haitibu korona?Kwa hiyo waliopo salama wakichanjwa hawataugua bali wenye korona tayari itabidi watibiwe ndio wawe na guarantee ya kutougua tena. By the way huwezi kuchanja wananchi wote.
Acheni kupotosha watu nyinyi.
Ukiwa unakinga Kwa nini uendelee kuvaa Barakoa, ujifungie n.k huoni kwamba hiyo siyo kinga tena?
 
Cha kuchekesha wanaosema chanjo ya COVID19 ni feki hawajawahi kutengeneza hata chanjo ya kideri cha kuku toka mwaka 1961 walivyopata uhuru.
Watuletee hizo nyungu wanazojifukiza huko kwa waganga wa kienyeji kama kweli zinafaa kwa chanjo.
 
Cha kuchekesha wanaosema chanjo ya COVID19 ni feki hawajawahi kutengeneza hata chanjo ya kideri cha kuku toka mwaka 1961 walivyopata uhuru.
Hahaha wao wataalamu wa kucheki ubora tuu 🤣🤣🤣
 
RAIS Dkt #MAGUFULI HAJAKATAA CHANJO YA #KORONA, AMBACHO HATAKI NI MAJARIBIO YA CHANJO KUFANYIKA KWA WANANCHI WAKE, MBONA WENYE MAMILIONI YA CHANJO BADO WAKO #LOCKDOWN NA #WANAKUFA Ni #Joseph #Yona

Rais Dkt Magufuli hajakataa Chanjo ya Korona na Rais Dkt Magufuli anajua alitendalo, Watanzania Ugonjwa wa Korona umeanzia China na Wachina wameanua Tanga la Korona.
Na Tambueni Rais wetu Mpendwa Dkt Magufuli alishajiridhisha kwani waliongea kwa simu na Rais wa China, Lakini waziri wa mambo ya nje wa China #Wang #Yi tulimuona Chato pamoja na mambo mengine Lazima aliteta na Rais Dkt Magufuli Kuhusu Korona na Lazima walibadilishana Mawazo iliishaje kwao, So Rais Dkt Magufuli anajua Mengi, hataki tuwe miili ya majaribio, Mbona wenye Chanjo wako Lockdown na wanakufa?

Chanjo Au Majaribio Ya Dawa Ya Korona(Clinical Trial)?

#PFizer ni kampuni kubwa na maarufu ya tafiti ya madawa nchini Marekani na maarufu pia kufanya majaribio ya Dawa zake barani Afrika.
Katika kutafuta Chanjo ya Korona 2020 wameshirikiana na Kampuni ya Ujerumani BioNTech(Pengine katika Kujikosha) huku wakidai Chanjo yao ina ufanisi wa 95%
Na 11/12/2020 walipewa ruksa na FDA(USA) kutumika rasmi kama Chanjo.

Ni nani PFizer .
Mwaka 1996 katika Jimbo la Kano nchini Nigeria ulizuka ugonjwa wa #Menengetics" haraka kampuni ya PFizer ikatengeneza dawa na Kisha hatua ya majaribio ya dawa hio(Clinical Trials) wakaenda kuifanya kwa watoto nchini Nigeria huko Kano.
Jambo hili lilipelekea watoto kadhaa kupoteza maisha na kesi hii kupelekwa mahakamani.
Ni Mwaka 2009 PFizer ikaomba kesi ifanyike nje ya Mahakama na kulipa Jimbo la Kano dola za kimarekani milioni 75 na familia za watoto waliopoteza maisha(watoto 4) dola za marekani 175,000.

Kwa nini wanapenda kuja Kujaribu Afrika ?
Swali hili analijibu Mwandishi Joseph Conrad katika kitabu chake Cha " Heart of Darkness 1989 .
Mwandishi anasema wazungu wanaamini sisi waafrika sio watu kamili(tuko tofauti Sana na wao)na tunafaa sana kufanyiwa majaribio ya dawa na hasa Chanjo na mengine Kama hayao(kwa maneno yangu).

Kabla ya leseni ya chanjo(Approval and licence) Kuna hatua muhimu tatu ile ya maabara(Exploratory Stage) ambayo huchukua muda mrefu sana(miaka 2 mpaka 3).
Sijui hawa kwa nini wamewahi wakati Chanjo za HIV, Malaria nk zina miaka bado watu wako mahabara.
Halafu huja hatua ya majaribio kwa wanyama(Pre clinical stages) na mwisho hatua ya majaribio kwa mwanadamu (Vacine Trial) hapa hufanyika kwa hatua kuu tatu,Kwanza huanza kwa watu wachache(20-80),Kisha hujaribiwa kwa watu mamia na baadae kwa watu maelfu.

Kimsingi kampuni zote za dawa na chanjo hupenda hizi hatua za mwisho kufanyia Afrika na wapo tayari kutoa mamilioni kama fidia kutokana na maafa yatakayotokea.
Na kutokana na kukithiri kwa rushwa na utawala wa Ovyo katika nchi nyingi Duniani Jambo hili hukubaliwa.

Na wanapotokea watawala wenye kujielewa Kama Rais wetu Dkt Magufuli mambo huwa magumu na wakati mwengine nguvu na hila hutumika.

Mwaka 2014 wakati walipiko wa Ebola Afrika Magharibi zaidi ya sampuli za damu 250,000 zilikusanywa toka kwa wagonjwa na makampuni makubwa ya dawa ya ulaya ili kufanya tafiti za dawa na chanjo.
Mpaka leo USA na Ufaransa wanashindwa kutoa majibu ni wapi zilipo hizo sampuli.
Ukweli ni kwamba zimetumika kuwapatia mamilioni ya pesa katika tafiti zilizopelekea kutengenezwa kinachoitwa Tiba ya Ebola.
Wanadai kutokana na sababu za kiusalama hawawezi kuzirejesha sampuli hizi.View attachment 1717109View attachment 1717110View attachment 1717112


Pumba kama hizi hutoka kwa ZERO brains pekee
 
una hoja nzito mleta mada na kwa nini hawaruhusu watu wao na ndege zao kwenda popote duniani wakati watu wao wamechanjwa? mbona ukipata chanjo ya homa ya manjano unaruhusiwa kwenda popote duniani?

Hii chanjo ni feki waruhusu waliochanjwa kuja Tanzania kutalii nk .Mbona mashirika yao ya ndege yako lockdown?

Waruhusu waliochanjwa kuja kutalii kama wanaamini chanjo yao
Ama kweli wajinga ndio waliwao!!!!!! Kwanza ni nani alokwambia kuwa watu wao wote wameshachanjwa kwa wakati huu? Kwa nini jamani hamsomi taarifa angalau kutoka WHO kabla ya kufyatuka kuja hapa na hoja zisizo na kichwa wala miguu. watu wao wataruhusiwa kusafiri tena mara tu pale zoezi zima la kuwachanja wananchi wote kukamilika. Kadhalika kwa sababu kumekuwepo na covid variant kadhaa, ipo haja ya wananchi wao kutahadharishwa nchi gani kutotembelea.

Ama kwa point yako ya ugonjwa wa manjano, narudia tena kwa nini hutafuti facts kwanza? labda ni Tanzania tu ambayo inawaruhusu waliopigwa chanjo ya homa ya manjano kwenda kila wanapotaka, lakini kwa wenzetu ukiangalia katika official websites zao zinazotoa taarifa za kusafiri, wameweka list ya nchi ambazo ziko free na homa ya manjano, nchi ambazo mtu anatakiwa kuwa na hadahri na homa ya manjano, na nchi ambazo za kuepuka kutokana na kuwepo homa ya manjano.
 
Cha kuchekesha wanaosema chanjo ya COVID19 ni feki hawajawahi kutengeneza hata chanjo ya kideri cha kuku toka mwaka 1961 walivyopata uhuru.

Mkeo anapokuwa anakupikia kila siku, sio kwamba wewe huwezi kupika, labda utakuwa mjinga na mpumbavu eti siku akitoka utalala njaa, kibaya zaidi kama utakuwa hata huwezi kuhoja pindi chumvi anapoizidisha kwenye mboga, kazi yako wewe ni kutafuna tu hata kiwe chakula kibovu unakulaga Tu

Basi wewe ni mwehu!!

Dawa zetu zimewekewa mazingira magumu kupitishwa na shilika linalolinda masilahi Yao ili tuonekane hatuwezi kutengeneza dawa,

Okey, Fanya kwamba hatuwezi, Je wanapotengeneza Sisi tusihoji hata kama kuna mazingira ya Sisi kuuliza usalama wa dawa zao???
 
RAIS Dkt #MAGUFULI HAJAKATAA CHANJO YA #KORONA, AMBACHO HATAKI NI MAJARIBIO YA CHANJO KUFANYIKA KWA WANANCHI WAKE, MBONA WENYE MAMILIONI YA CHANJO BADO WAKO #LOCKDOWN NA #WANAKUFA Ni #Joseph #Yona

Rais Dkt Magufuli hajakataa Chanjo ya Korona na Rais Dkt Magufuli anajua alitendalo, Watanzania Ugonjwa wa Korona umeanzia China na Wachina wameanua Tanga la Korona.

Na Tambueni Rais wetu Mpendwa Dkt Magufuli alishajiridhisha kwani waliongea kwa simu na Rais wa China, Lakini waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi tulimuona Chato pamoja na mambo mengine Lazima aliteta na Rais Dkt Magufuli Kuhusu Korona na Lazima walibadilishana Mawazo iliishaje kwao, So Rais Dkt Magufuli anajua Mengi, hataki tuwe miili ya majaribio, Mbona wenye Chanjo wako Lockdown na wanakufa?

Chanjo Au Majaribio Ya Dawa Ya Korona(Clinical Trial)?

#PFizer ni kampuni kubwa na maarufu ya tafiti ya madawa nchini Marekani na maarufu pia kufanya majaribio ya Dawa zake barani Afrika.

Katika kutafuta Chanjo ya Korona 2020 wameshirikiana na Kampuni ya Ujerumani BioNTech(Pengine katika Kujikosha) huku wakidai Chanjo yao ina ufanisi wa 95%.Na 11/12/2020 walipewa ruksa na FDA(USA) kutumika rasmi kama Chanjo.

Ni nani PFizer .
Mwaka 1996 katika Jimbo la Kano nchini Nigeria ulizuka ugonjwa wa #Menengetics" haraka kampuni ya PFizer ikatengeneza dawa na Kisha hatua ya majaribio ya dawa hio(Clinical Trials) wakaenda kuifanya kwa watoto nchini Nigeria huko Kano. Jambo hili lilipelekea watoto kadhaa kupoteza maisha na kesi hii kupelekwa mahakamani.

Ni Mwaka 2009 PFizer ikaomba kesi ifanyike nje ya Mahakama na kulipa Jimbo la Kano dola za kimarekani milioni 75 na familia za watoto waliopoteza maisha(watoto 4) dola za marekani 175,000.

Kwa nini wanapenda kuja Kujaribu Afrika?
Swali hili analijibu Mwandishi Joseph Conrad katika kitabu chake Cha " Heart of Darkness 1989 . Mwandishi anasema wazungu wanaamini sisi waafrika sio watu kamili (tuko tofauti Sana na wao) na tunafaa sana kufanyiwa majaribio ya dawa na hasa Chanjo na mengine Kama haya (kwa maneno yangu).

Kabla ya leseni ya chanjo (Approval and licence) Kuna hatua muhimu tatu ile ya maabara (Exploratory Stage) ambayo huchukua muda mrefu sana(miaka 2 mpaka 3).

Sijui hawa kwa nini wamewahi wakati Chanjo za HIV, Malaria nk zina miaka bado watu wako mahabara. Halafu huja hatua ya majaribio kwa wanyama(Pre clinical stages) na mwisho hatua ya majaribio kwa mwanadamu (Vacine Trial) hapa hufanyika kwa hatua kuu tatu,Kwanza huanza kwa watu wachache(20-80),Kisha hujaribiwa kwa watu mamia na baadae kwa watu maelfu.

Kimsingi kampuni zote za dawa na chanjo hupenda hizi hatua za mwisho kufanyia Afrika na wapo tayari kutoa mamilioni kama fidia kutokana na maafa yatakayotokea. Na kutokana na kukithiri kwa rushwa na utawala wa Ovyo katika nchi nyingi Duniani Jambo hili hukubaliwa.

Na wanapotokea watawala wenye kujielewa Kama Rais wetu Dkt Magufuli mambo huwa magumu na wakati mwengine nguvu na hila hutumika.

Mwaka 2014 wakati walipiko wa Ebola Afrika Magharibi zaidi ya sampuli za damu 250,000 zilikusanywa toka kwa wagonjwa na makampuni makubwa ya dawa ya ulaya ili kufanya tafiti za dawa na chanjo.

Mpaka leo USA na Ufaransa wanashindwa kutoa majibu ni wapi zilipo hizo sampuli. Ukweli ni kwamba zimetumika kuwapatia mamilioni ya pesa katika tafiti zilizopelekea kutengenezwa kinachoitwa Tiba ya Ebola.
Wanadai kutokana na sababu za kiusalama hawawezi kuzirejesha sampuli hizi.​


View attachment 1717109View attachment 1717110View attachment 1717112
JPM for Life. Kanyaga Twende
 
Luwa na chanjo ya aina yoyote ile haikufanyi wewe kujiachia tu eti hutapata maradhi hapana kazi ya hiyo chanjo ni kupunguza uwezekano wa wewe uliyechanjwa kupata magonjwa kwa haraka . Ili kuifanya chanjo yako iwe na maana zaidi unapaswa kuchukua tahadhari zaidi kama vile kabla ya hujapata chanjo ili kulinda maisha yako na maisha ya wengine kwa asilimia ikiwezekana 100% .
 
Mbona husemi watawala wanaosema wanamtuamini Mungu ndio wanaongoza kuwa na misafara mirefu yenye silaha nzito na jamming devices ?

Pia watawala hao hao gharama za msafara wao analipa mwanachi huyo huyo aliye kijijini na anakunywa maji kisima kimoja na mbuzi wake ilhali pesa hiyo ingekwenda kumaliza tatizo la maji kijijni kwake
 
Back
Top Bottom