Mbona wamo wengi tu!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona wamo wengi tu!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 7, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  JK: Fisadi ndani ya CCM atakiona
  Martha Mtangoo, Dodoma
  Daily News; Wednesday,January 07, 2009 @21:15​

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na ufisadi hata kama ni mwanachama wa chama hicho, atashughulikiwa.

  Akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema kazi ya kuwafuatilia na kuwachunguza wanaotajwa kuhusika katika sakata hilo inaendelea.

  Alisema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika lazima lawama ziwapo, kwa sababu ni kazi ngumu na lawama katika uongozi hazikwepeki. Alisema orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa imekuwa ikipokewa na wamekuwa wakichunguzwa, kwa kuzingatia utaratibu uliopo wa kuchunguza na kamwe Serikali haiwezi kukurupuka na kuwakamata na kuwaweka ndani.

  Alisema hata mtu anayetajwa katika orodha hiyo ni lazima atendewe haki kwa kuwa zipo sheria na taratibu zinazomlinda. “Jamani tuachieni tufanye kazi na sisi tutafanya hivyo bila kumkomoa mtu yeyote na kazi itafanywa ili wanaotuhumiwa waridhike; orodha za majina tunazopewa hazipuuzwi, zinafanyiwa kazi,” alisema Rais Kikwete.

  Alisisitiza kuwa mafisadi ni lazima washughulikiwe ili nchi ipate heshima na kuwataka wanaowafahamu wasaidie kuwataja. Alisema uchunguzi unafanywa kwa muda mrefu na atakayebainika atafikishwa katika vyombo vya dola na iwapo watakaofikishwa katika vyombo hivyo hawataridhika, wako huru kwenda mahali popote kuelezea kutoridhishwa kwao.

  “Kazi hii inafanywa na iwapo watu watatuhumiwa na kuona kuwa hawakutendewa haki, waende hata mahakamani … lakini waachiwe watu na vyombo vyao wafanye kazi yao na wasiingiliwe,” alisisitiza. Pia Rais Kikwete aliwataka wajumbe wa mkutano huo, kuchagua viongozi ambao watawafaa kwa kuwa wakifanya kosa, watalijutia kwa muda wa miaka mitano kwani majuto ni mjukuu.

  Alisema ni vyema wajumbe hao wasiwachague watu kwa kuwa ni marafiki, ndugu au mashoga zao, kwa sababu tu kwamba watawafaa na kuwafadhili kwani hivyo si vigezo vya uongozi ndani ya jumuiya hiyo. “Usimchague mtu eti tu kwa sababu atakufaa, anayekufaa ni mumeo na ndugu yako, chagueni mtu ambaye atawatoa hapo mlipo na kuwapeleka katika neema,” alionya Mwenyekiti wa CCM.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama vya siasa vya Chadema, CUF, TLP na mabalozi wa nchi mbalimbali. Jana usiku, wajumbe walitarajiwa kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa Baraza Kuu, huku mchuano mkali ukitarajiwa katika nafasi ya mwenyekiti inayowapambanisha vigogo watatu.

  Nao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, Sophia Simba, wabunge wa Viti Maalumu, Janeth Kahama na Joyce Masunga. Katika hatua nyingine, vitisho na matusi viliendelea kutawala kwa baadhi ya makatibu wa mikoa na wilaya wa umoja huo, kutishiwa kukataliwa na wenyeviti wao kwa madai kuwa hawakushiriki katika kampeni.

  Licha ya makatibu hao kutishiwa kukataliwa na wenyeviti hao, pia baadhi ya wapambe wa wagombea wa nafasi za juu za UWT wamekuwa wakiwatishia makatibu hao, kuwa mgombea wao akishinda makatibu hao ‘wataipata’.

  Mwenyekiti wa UWT anayemaliza muda wake Anna Abdallah, alimweleza Rais Kikwete jana kuwa mambo hayo yameanza kujitokeza baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi katika mikoa na wilaya.

  “Jambo lingine ambalo limeanza kujitokeza baada ya kukamilika kwa uchaguzi huko mikoani na wilayani ni salamu zilizoanza kufika makao makuu, kuwa baadhi ya wenyeviti wa mikoa na wilaya wamesema hawawataki makatibu wao, kisa eti hawakushiriki katika kampeni zao za uchaguzi.

  “Na baadhi ya wapambe wamesikika wakisema mgombea wao akishinda, basi kuna makatibu wataipata,” Abdallah alimweleza Mwenyekiti huyo wa CCM. Mwanasiasa huyo mkongwe alisema mambo hayo yanasababisha makundi ndani ya CCM, kwa kuwa baadhi ya wapambe wa wagombea wa nafasi za juu walikuwa wakizunguka mikoani na kutumia fedha nyingi huku wakipata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa mikoa na wilaya wa UWT.

  Alisema matumizi makubwa ya fedha ambayo yamekuwa yakifanywa na wapambe hao, yanawakatisha tamaa wanawake wengine ambao wana nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na hivyo kukifanya chama kugawanyika. “Sasa mimi najiuliza, gharama hizi kweli kwa ajili ya uenyekiti na uongozi wa UWT au kuna la zaidi?,” alihoji na kumwomba Rais Kikwete kuwalinda wanawake walio tayari kugombea nafasi za uongozi na kuiomba CCM ikemee tabia hiyo, kwani inazaa makundi ndani yake.
   
 2. K

  Kakulwa Senior Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chanzo changu cha uhakika kinasema Waziri Simba kapigwa chini huku JK mwenyewe akitia mkono wake.
  Mwenyekiti mpya wa UWT ni mama Kahama.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Good... ! Hongera mama Kahama
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  English please...
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Where have you been recently...? Kuna issue kibao zimetokea.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Bubu, umeleta swala haswa ambalo linawagusa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini.
  Kaoro ya kutokuwepo na SERA au itikadi innayotumika katika kampeni ndiyo inazaa hizi kampeni zisizo na malengo maalum.
  Watu sasa wanachaguliwa kwa umaarufu wao na sio kwa umahiri wa utekelezaji wa sera.Kwa hiyo si jambo la kushangaza kuona hakuna msimamo wa kicham unaozungumziwa hapa ila mtu ndiyo anazungumziwa na ukikosana naye wafwa!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Umaarufu ni sehemu ya kujikampeni, hii inategemea una umaarufu wa namna gani. Kama ni mchapa kazi ama sio mchapakazi...! All in all umaarufu ni factor mojawapo katika kupata ushindi.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Naam umesema kweli tupu hapo kwamba umaarufu ni kitu muhimu katika kufanya kampeni. Kuna haja ya kujiuliza umaarufu wenyewe ni wa nini!? Ukweli ni kwamba si umaarufu wa uchapa kazi au kutetea maslahi ya Watanzania, bali ni umaarufu wa kutoa takrima na kutetea mafisadi ndani ya chama cha mafisadi. Maana hatujawasikia hata siku moja wakitoa sauti zao katika vita hii dhidi ya mafisadi.
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ..kabla ya kuja hapa na kutupa lecture za maneno matupu, angeanza kuomba bunge watunge sheria za kudhibiti money in politics na sheria ziwe wazi kuonyesha pesa wanazotumia ni kiasi gani na wanapata wapi na matumizi yote ya kampeni lazima yaeleweke, maana ndio rushwa zote zinaanzia pale na ndipo viongozi incompetent na mafisadi wanapatikana
   
Loading...