Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,739
- 40,863
Hivi kuna kitu nimemiss.. maana nimesikia kuna watu wanalalamika Rais kapiga marufuku siasa. Nimetoka kuangalia hotuba yake lakini sijaona mahali alipopiga marufuku siasa. Inawezekana ametoa hotuba nzuri na ya kirafiki zaidi kwa wanasiasa. Au kuna agizo jingine limetolewa nje ya hii hotuba ya leo?
Nimeona tamko la chama cha ACT na limenifanya nikimbie haraka kusoma na kusikiliza hiyo hotuba kabla ya kutoa maoni yangu. Lakini sikusikia agizo au tamko lolote lile za kupiga marufuku siasa au kazi za siasa nchini. Nimeona Rais ametoa "ombi" ambalo ukijumlisha na aliyoyasema baadaye linaashiria tu kuwataka wanasiasa kufanya siasa nzuri zaidi bila kusababisha kukwamisha juhudi za maendeleo au kuonekekana wanaendekeza mno siasa kuliko kazi za kulijenga taifa.
Au baada ya hotuba yake Rais ametoa agizo jingine rasmi la kupiga marufuku kazi za siasa nchini? Au labda uzee ndio unazidi kasi nimeshindwa kuelewa.
Sehemu ya Hotuba: