Mbona pori letu moja?

Mbona pori letu moja?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,146
Reaction score
829,061
Sisi ukoo wa manyani tuwabebao chawa milini mwetu na kuwahudumia kwa chakula na malazi, mbona tunatendwa mabaya tena? Tumekosea wapi? Tumemkosea nani?

Kama tatizo ni kujitangaza kwa uwazi kwamba sisi ni manyani mbona walipojiita chawa mliwasapoti? Na usajili mkawapa? Na sasa wanakula mema ya pori katika nchi ile ya kusadikika ya mfalme janja kule kwa wagagagigikoko?

Hivi hebu tuwe wakweli kati ya sisi manyani na wale machawa ni nani walau ana faida kwenye hili pori letu tukuka? Hata tukiamua kufanya sensa ya manyani na chawa watatuweza kwa wingi wetu? Na umoja wetu?

Ninini faida ya chawa kama ni kula kulala tuu?

CHAWA WANASTAWI NA KUONGEZEKA HUKU NYANI WAKIMWAGIWA SUMU NA KUUAWA!

Baba Askofu Stephen Munga anashangazwa na mwenendo wa Pori la Mkuranga! Kuwa kuna kikosi kimejitangaza kuwa ni chawa, kimeapa kupambana na kila anayemsema vibaya Malkia wa Pori, kimemwagiwa pesa nyingi kinatembea nchi nzima kumsifia Malkia.

Kikosi kingine kimejitangaza kuwa ni 'nyani' na kinalalamikia utawala wa Malkia wa Pori. Lakini kikosi hicho kinawindwa kama chui awindavyo suala ili kiangamizwe! Lakini cha kuajabia ni kuwa 'nyani' ni wengi zaidi porini kuzidi chawa!

Mwana Kondoo Ameshnda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 21 Septemba 2023; 5:40 asubuhi.
FB_IMG_1695294986211.jpg
a8628bdf71772cf2c0307aa9d061b9f9.jpg
15930c90519b4a1dac0813aff7bb8b5c.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisi wana double standard sana. Mbona hata yule Mwanadiplomasia kutoka Ethiopia alipokitaja kile chama chakavu kama chamba cha Mambuzi! Hakufanywa chochote?

Kwa nini wanaohisi kuonekana manyani, wanyanyaswe?
 
Wametuona NYANI hii slogan ni kiboko chawa wakasome
 
Walipojiita machawa, hakukuwa na tabu, wengine kujiita manyani ndo tunasakwa utadhani mwenye kustahili kuitwa jina ni chawa pekee!
Praise team akijiita hata 'papasi' haina shida mradi tu anamsifu Malkia wa Pori
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom