Mbona Mrema anamuunga mkono Rais Magufuli akiwa TLP! Wanaohama wana ajenda za siri?

Najiuliza tu, mbona mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema alianza kumuunga mkono mstaafu Kikwete na sasa anamuunga mkono Rais Magufuli lakini akiwa huko huko TLP. Sasa iweje hawa wanasiasa vijana tena wengine wageni tu siasani wasijifunze kwa Mrema na badala yake wanalitia taifa hasara kwa kurudia uchaguzi?!!! Ni wakati sasa wa CCM kuwa macho isijekuwa hawa jamaa wana ajenda ya siri. Ni hayo tu!
Siasa za Tanzania michosho hazina tena mvuto Ni hasara na kupoteza muda kuzijadiri!

Ebu fikiria lijitu linajiona kuwa ubunge ni wa kwake wakati lilibebwabebwa na chama likaupata kisha linajitoa kwa sababu limehongwa au linatafuta sifa!

Hii inapelekea kutojua mwanasiasa ni yupi na mfanyabiashara ni yupi!!
 
Nimetoa mfano huo kwa sababu unafanana na hali iliyopo kwenye vyama, kwa mfano msigwa aliongea kwenye magic fm kwamba kazi ya chadema ni kuchochea wananchi waione serikali haifai,katika hali kama hiyo inawezekenaje kuunga mkono kwa vitendo serikali bila kuonekana msaliti? Tumeshuhudia mialiko mingi ya uzinduzi wa miradi mbali wabunge wa upinzani wakisusia je ukiwa unaunga mkono Serikali ukishiriki zinduzi za namna hiyo utakuwa salama? Wale waliovaa vitambaa midomoni bungeni inawezekanaje mwingine akatae kuvaa kitambaa kama hakubaliani? Mifano ni mingi ambayo inaonyesha wazi kuwa haiwezekani kabisa na mwisho wake lazima utafukuzwa chama kwa vyoyote mwenye msimamo thabiti lazima ajitoe.

Ukipiga propaganda lazima uwe na uhakika na usemacho. Huyo meya wa Dar ambaye ni cdm sio mara moja au mbili ameshiriki uzinduzi mbali mbali na nimemuona kwa macho yangu. Meya wa Arusha pia nimemshuhudia kwa macho yangu akiwa kwenye uzinduzi wa barabara ya Arusha Tengeru. Hapa unachojaribu ni kuichafua cdm na wala hatuoni shida kwani kwenye ushindani unaweza kumpaka matope mshindani wako. Ila kumpaka matope sio kwa gharama ya kupindisha hata ukweli unaoonekana. Hayo unayoyaona bungeni ni aina ya kupinga jambo fulani na huwa linafanyika kwa muda fulani. Ila kwakuwa kuna ulimbukeni ama nakisi ya demokrasia ndio maana mnaona shida baadhi ya mbinu za kupinga jambo.

Huwa tunaona wanaccm wakiunga kila kitu na hakuna anayeweza kusimama na kupinga waziwazi, je ni kweli uwezo wa kufikiri wa wanaccm ni aina moja? Je ni kweli kila kinacholetwa na serekali ccm huwa haioni walakini? Nimeona unaserereka toka juu kwa post za upotoshaji. Tunakuona na hatujalala kama unavyodhani. Fanya propaganda upendavyo na sisi tunakubali maana ndio demokrasia lakini ukipotosha ukweli tunakuumbua.
 
1.Wanawanunua
2.wanawapigania waingie katika nafasi za maamuzi
3.watawanunua tena kubadili katiba mkulu aongezewe muda
SIwaamini A kina bashite
m
 
Ukipiga propaganda lazima uwe na uhakika na usemacho. Huyo meya wa Dar ambaye ni cdm sio mara moja au mbili ameshiriki uzinduzi mbali mbali na nimemuona kwa macho yangu. Meya wa Arusha pia nimemshuhudia kwa macho yangu akiwa kwenye uzinduzi wa barabara ya Arusha Tengeru. Hapa unachojaribu ni kuichafua cdm na wala hatuoni shida kwani kwenye ushindani unaweza kumpaka matope mshindani wako. Ila kumpaka matope sio kwa gharama ya kupindisha hata ukweli unaoonekana. Hayo unayoyaona bungeni ni aina ya kupinga jambo fulani na huwa linafanyika kwa muda fulani. Ila kwakuwa kuna ulimbukeni ama nakisi ya demokrasia ndio maana mnaona shida baadhi ya mbinu za kupinga jambo.

Huwa tunaona wanaccm wakiunga kila kitu na hakuna anayeweza kusimama na kupinga waziwazi, je ni kweli uwezo wa kufikiri wa wanaccm ni aina moja? Je ni kweli kila kinacholetwa na serekali ccm huwa haioni walakini? Nimeona unaserereka toka juu kwa post za upotoshaji. Tunakuona na hatujalala kama unavyodhani. Fanya propaganda upendavyo na sisi tunakubali maana ndio demokrasia lakini ukipotosha ukweli tunakuumbua.
Kuna baadhi ya matukio wanasusa ushahidi upo na hata juzi wamesusia michezo ya bunge kwa kuwaambia wachezaji wao wajitoe, twende kwenye logic ya kawaida je Inawezekana mbunge wa chadema aipende ccm halafu aonyeshe wazi? Haiwezekani ndio maana wanahama simple! Na hii sio kwa chadema tu hata ccm huwezi kuwa na mapenzi na chadema uweke wazi unaitwa msaliti na unafukuzwa kama Sophia simba alivyofukuzwa hiyo iko wazi sijui unabisha nini?
 
Hizo ni pombe ambazo ki-nib cha whisky ni bora kuliko keni la kimpunu au kibuku. Lakini siasa ni watu na kama huamini muulize Lamwai.
Siasa si watu,bali siasa ni watu wenye akili timamu,wenye kutumia logic kuhusu mustakabali wa taifa, na si kama wale wasiotumia critical thinking wasemao kuwa wanaacha ubunge ili kumuunga mkono Rais.Je Rais akimaliza muda wake wataenda kumuunga mkono nyumbani?Ni upungufu wa fikra kwa MTU mzima kuunga utashi wa mtu na kuhama ulipo,badala ya kuunga mfumo wenye future kwa taifa,na si mfumo mapokeo,bali ni mfumo yakinifu.Kwakweli magonjwa ya akili barani Afrika yanasumbua sana.
 
Kuna baadhi ya matukio wanasusa ushahidi upo na hata juzi wamesusia michezo ya bunge kwa kuwaambia wachezaji wao wajitoe, twende kwenye logic ya kawaida je Inawezekana mbunge wa chadema aipende ccm halafu aonyeshe wazi? Haiwezekani ndio maana wanahama simple! Na hii sio kwa chadema tu hata ccm huwezi kuwa na mapenzi na chadema uweke wazi unaitwa msaliti na unafukuzwa kama Sophia simba alivyofukuzwa hiyo iko wazi sijui unabisha nini?
Kumuunga mkono Rais Magufuli haimaanishi wewe una mapenzi na CCM!
 
Najiuliza tu, mbona mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema alianza kumuunga mkono mstaafu Kikwete na sasa anamuunga mkono Rais Magufuli lakini akiwa huko huko TLP. Sasa iweje hawa wanasiasa vijana tena wengine wageni tu siasani wasijifunze kwa Mrema na badala yake wanalitia taifa hasara kwa kurudia uchaguzi?!!! Ni wakati sasa wa CCM kuwa macho isijekuwa hawa jamaa wana ajenda ya siri. Ni hayo tu!
Leo hii mnamtolea mfano mrema. Kwanza mnatamani na yeye ajiunge ukawa. Muacheni Mzee wa watu mlimsimanga na li MBA*TI*A lenu Leo mnaanza kumnukuu. Kufeni kivyenu.
 
Wana Sacco's mnaweweseka kweli kwani si kila mtu na utashi wake au
Mmenunua wana ccm kama lowasa na Sumaye Leo nyarandu yaan hao ni mapapa wa siasa sisi tunanunua vidagaa tu bado mnaona wivuuuu na bado
 
Hilo ni tendo dogo halionyeshi upinzani wowote zaidi ya kujitengenezea political mileage lkn walitoa wakati hajaanza kutawala, ni kitu kisichowezekana kwa mbunge wa upinzani kuita press kama zile za kukosoa na kuunga mkono na labda kuwataka watu wa jimbo lake na watanzania kwa ujumla wamsupport rais kama wanavyowashawishi wananchi wampige brake rais.
Ndio maana tunasema mbunge kuhama chama ni ufisadi tu mbona Hamad Rashid ni waziri ktk serikali ya CCM lakini hajahama chama!
 
Leo hii mnamtolea mfano mrema. Kwanza mnatamani na yeye ajiunge ukawa. Muacheni Mzee wa watu mlimsimanga na li MBA*TI*A lenu Leo mnaanza kumnukuu. Kufeni kivyenu.
Karibu mgeni lakini jifunze kutumia lugha za kistaarabu hapa Jf si sawa na huko FB!
 
Back
Top Bottom