Mbona Mrema anamuunga mkono Rais Magufuli akiwa TLP! Wanaohama wana ajenda za siri?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,376
2,000
Najiuliza tu, mbona mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema alianza kumuunga mkono mstaafu Kikwete na sasa anamuunga mkono Rais Magufuli lakini akiwa huko huko TLP. Sasa iweje hawa wanasiasa vijana tena wengine wageni tu siasani wasijifunze kwa Mrema na badala yake wanalitia taifa hasara kwa kurudia uchaguzi?!!! Ni wakati sasa wa CCM kuwa macho isijekuwa hawa jamaa wana ajenda ya siri. Ni hayo tu!
 
Lubebenamawe

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,367
2,000
Itikadi ya chama cha Mrema inaruhusu kumuunga mkono Mheshimiwa Rais ila itikadi za vyama vingine haviruhusu kumuunga mkono Mh. Rais hata kama jambo analofanya ni la manufaa kwa umma. Itikadi Chadema ni kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali. Ukiwa chadema ukitangaza kuunga mkono juhudi za serikali utafukuzwa uanachama.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Najiuliza tu, mbona mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema alianza kumuunga mkono mstaafu Kikwete na sasa anamuunga mkono Rais Magufuli lakini akiwa huko huko TLP. Sasa iweje hawa wanasiasa vijana tena wengine wageni tu siasani wasijifunze kwa Mrema na badala yake wanalitia taifa hasara kwa kurudia uchaguzi?!!! Ni wakati sasa wa CCM kuwa macho isijekuwa hawa jamaa wana ajenda ya siri. Ni hayo tu!

Wangefanya hivyo pia mngewaita Wasaliti na kuwataka wahame!
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Ni tafsiri mbovu tu ya neno "upinzani" linalotumiwa na CDM ndiyo maana , unaona na kushangaa kuwa hao wengine wako na mubashara kabisa na Rais na wakati uo huo wanamkubali Rais na serikali yake pale inapofanya mambo mazuri.

Ni kama Zito ZK , nawe huwa anakubali mambo ya rais wakati mwingine anapinga kwa hoja (baadhi ya mambo ZKK huwa na hoja na akapinga) na siyo mara zote anakuwa anapinga kila kitu.

Huo ndiyo upinzani duniani kote tatizo Africa hasa Tanzania wapinzani wanadhania kuwa wao sasa kazi yao ni kupinga kila jambo.

Hiyo inakuwa , siyo maana na tafsiri sahihi ya siasa za vyama vingi na upinzani bali inakuwa ni fujo.
Kwa hiyo, wanaohama wanashindwa kupongezwa serikali pale inapofanya jambo zuri kwa sababu mlengo wa CDM hauruhusu kabisa habari hiyo ya kutoa pongezi au kukubaliana na serikali/ au Rais kwa kila jambo.

Ila hasa, mwaka huu wa 2017 ndiyo wamezidisha hiyo tabia ya kupinga kila kitu.

Na ni tabia na jambo ambalo ni baya kabisa kwa ustawi wa nchi hata na democracy na ndiyo maana hata sasa serikali kuu na taasisi ya urais nayo imeamua kuwapuuza hao CDM and the likes kwa sababu ya nidhamu yao kutokuwa nzuri kwa mstakabali wa nchi yetu na hadi usalama wa Taifa Letu.
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,755
2,000
Baadhi ya vyama vimepiga marufuku wafuasi kumuunga mkono rais ama kutambua jema lolote la serikali yake hadharani.

Msigwa alisema siku ile channel 10 kuwa wapo kwa ajili ya kuwashawishi wananchi waione serikali iliyopo haifai.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,376
2,000
Ni tafsiri mbovu tu ya neno "upinzani" linalotumiwa na CDM ndiyo maana , unaona na kushangaa kuwa hao wengine wako na mubashara kabisa na Rais na wakati uo huo wanamkubali Rais na serikali yake pale inapofanya mambo mazuri.

Ni kama Zito ZK , nawe huwa anakubali mambo ya rais wakati mwingine anapinga kwa hoja (baadhi ya mambo ZKK huwa na hoja na akapinga) na siyo mara zote anakuwa anapinga kila kitu.

Huo ndiyo upinzani duniani kote tatizo Africa hasa Tanzania wapinzani wanadhania kuwa wao sasa kazi yao ni kupinga kila jambo.

Hiyo inakuwa , siyo maana na tafsiri sahihi ya siasa za vyama vingi na upinzani bali inakuwa ni fujo.
Mfano Sugu, Lema na Msigwa wao kazi yao kupinga tu!
 
chikundi

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
8,163
2,000
Najiuliza tu, mbona mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema alianza kumuunga mkono mstaafu Kikwete na sasa anamuunga mkono Rais Magufuli lakini akiwa huko huko TLP. Sasa iweje hawa wanasiasa vijana tena wengine wageni tu siasani wasijifunze kwa Mrema na badala yake wanalitia taifa hasara kwa kurudia uchaguzi?!!! Ni wakati sasa wa CCM kuwa macho isijekuwa hawa jamaa wana ajenda ya siri. Ni hayo tu!
Mrema ni mwenyekiti anaamua anavyotaka lkn chadema kuna mwenye nyumba,mpangaji lazima afuate mashart ya mwenye nyumba la sivyo atafukuzwa mchana kweupe, ili uwe salama lazima uhame kwanza.
 
Jaimee

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
2,632
2,000
Mambo mengine ni yakipuuzi sana,kwani Rais alichaguliwa na ccm peke yao?Sasa hao wachumia tumbo wanamdanganya nani? Maana inaonyesha kabisa kuwa Rais alichaguliwa na watu wengine toka vyama mbalimbali na wasio na vyama.Kwahiyo hii hoja ya kuhama eti ndiyo kumuunga mkono siyo sahihi kabisa,bali njaa ndizo zinawapeleka huko.Swali rahisi ni je, atakapomaliza muda wake na wao watamaliza muda wao ktk siasa?Hoja za kizembe kwelikweli!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom