Mbona mishahara ya wabunge haihitaji migomo

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,171
Posho za wabunge ziliongezwa. Mishahara itaongezwa kufikia mil. 10. Kila ombi la nyongeza ya mishahara ya wabunge inapopelekwa, hupitishwa bila hotuba za mwisho wa mwaka. Hawa ni zaidi ya wabunge 300 idadi ambayo ni zaidi ya jumla ya madaktari wakuu wa Wilaya na Mikoa yote Tanzania.

Elimu muhimu ni kujua kusoma na kuandika Kiswahili/Kiingereza tu.

Mbali na mishahara, hospitali yao ya rufaa iko India. Shule kwa watoto wao ni zile za private.

Sielewi sababu ya mahitaji yote haya kwa wabunge ni kwa nini hayakataliwi. Tutaendelea kwa kulipa mishahara mikubwa kwa wanasiasa tu!
 
Si ndio maana wasomi wengi (PhDs na maprofesa ) wanakimbilia ubunge na kuacha taaluma zao?
 
Back
Top Bottom