Majangaaa Mbona Majangaaa! - 2-
Binti huyo akaendelea kufanya kile alichokuwa akikifanya, mara akashtuka aliposikia mlio wa vyombo vikipasuka.
Ndiyo, Eddy alikuwa ameziachia sahani alizokuwa amezishika mikononi mwake bila ya kutarajia.
Kufuatia mlio uliotokana na kuvunjika kwa sahani hizo, Rehema alimgeukia
Eddy na kuumuliza kulikoni, ndipo kijana huyo akamwambia zilimteleza kwa bahati mbaya.
HEBU NENDA NAYO
Vipi kaka
? Rehema alimuuliza Eddy.
Aaah, sahani zimeniteleza kwa bahati mbaya
Pole sana
, alisema Rehema na kisha kuendelea kusugua visigino vyake huku akitingisha wowowo lake katika staili ile ya hamsini hamsini mia.
Majangaaa
! Eddy alisema kwa sauti ya upole na kujilazimisha kuingia ndani ya chumba alichokuwa amepanga.
Kichwani mwake alikuwa akimfikiria Rehema, akawa anajiuliza kama anaweza kuachana na wanawake wote ili awe na huyo.
Sasa hapa nitamletaje Amina, nitamletaje Anita? alijiuliza na kuwa na wasiwasi na mwonekano wa Rehema kwa kuwa alikuwa akionekana kama ni mkorofi fulani hivi.
Anaonekana mshari-mshari sana, sijui kama nitamuweza, alizidi kufikiria Eddy na kujitupa katika kitanda kilichokuwa kimemaliziwa kufungwa muda mchache na watu waliofika kumsadia.
Ghafla akiwa hapo, alisikia sauti nyingine ya msichana ikimwita Rehema.
Dada mkubwa
dada mkubwa
Abee, Rehema aliitikia kwa kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa akifahamika kama dada mkubwa ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa wakiishi wasichana wengi.
Wengi wao walikuwa wakimheshimu Rehema kutokana na umri wake na uzoefu wake katika masuala ya mapenzi, pia ndiye aliyekuwa mshauri mkuu wa kila jambo kwa mabinti wengine mtaani hapo.
Njoo uone mambo huku
, alisema msichana aliyekuwa akimwita Rehema.
Kuna nini jamani?
Patra kafumaniwa huku
, alisema msemaji huyo na miguu yake kusikika akitoka nje kwa mlango mkubwa wa upande wa barazani.
Patra
! alishangaa Rehema na kufanya binti yule kurudia kusema kwa msisitizo.
Ndiye yeye kwani mtaani kuna Patra wangapi?
Eddy alikuwa akitaka sana kumuona huyo binti mwingine ambaye alikuwa na sauti nzuri kama kinanda, akili yake ilimtuma kama angemuona angeweza kufanya uchaguzi bora kati ya Rehema na huyo binti.
Ingawaje moyoni Eddy alikuwa amekufa kwa Rehema lakini wasiwasi wake ulikuwa ni jinsi alivyokuwa amekaa kimtoto wa mjinimjini sana.
Hata hivyo hakuweza kutoka kumwangalia msichana aliyekuwa akimwita Rehema, hakutaka kuonekana kama vile ni mmbeya kwa kufuatilia mambo ya watu, akauchuna kwa kuendelea kulala kitandani pake huku akitafakari jinsi atakavyoendesha maisha yake katika makazi hayo mapya.
Mara miguu ya Rehema nayo ikapita katika chumba chake kwa kasi na kutoka nje kupitia mlango wa barazani.
Daaa huyu mtoto mkali sana lakini
, alijisemea moyoni Eddy.
****
Siku hiyo Eddy hakutoka nje, kwa kuwa ilikuwa ni jioni hakuona umuhimu wa kufanya hivyo, alikuwa ameshakula na hakujisikia kuoga. Akaamua kuendelea kulala.
Asubuhi siku ya pili, mapema sana Eddy alikuwa ni mtu wa kwanza kutoka nje, akakutana na baba mwenye nyumba na kusalimiana naye.
Za asubuhi baba?
Nzuri tu, umeamkaje?
Sijambo, shikamoo.
Marhaba
tena afadhali umewahi kwenda kuoga ukichelewa hapa
utajuta, baba mwenye nyumba alisema na kumpongeza Eddy aliyebaki na maswali kibao baada ya kusikia kauli hiyo.
Huku akishindwa kupata jibu, Eddy moja kwa moja akaingia msalani na kumaliza haja zake muhimu na kisha kuelekea bafuni.
Lilikuwa ni bafu la kiswazi ambalo ungeweza kuchungulia na kumuona mtu wa nje kwa kupitia pachipachi za mlango na sehemu za kidirisha kidogo.
Akaanza kujimwagia maji. Hazikuchukua hata dakika tano akasikia milango ikigongana, akaacha kujimwagia maji na kuchungulia nje.
Walikuwa ni wasichana watatu, mmoja alikuwa ni mrefu na mwembamba lakini pamoja na wembemba wake, alikuwa amejengeka vyema katika kiuno kwani alikuwa amekatika na kuwa na kiuno kama cha nyigu.
Mwingine alikuwa ni mnene, mfupi kiasi lakini alikuwa na mvuto wake kutokana na rangi ya mwili wake ambayo ilikuwa ikingaa kwa weusi wake.
Wa tatu alikuwa ni msichana mrefu na mnene ambaye kwa harakaharaka Eddy aliweza kumbaini kuwa ni yule aliyekuwa akimwita Rehema jana yake na kumwambia kwamba Patra kafumaniwa.
Wote watatu walikuwa wakigombania kuingia msalani lakini kwa kuwa yule msichana mrefu na mnene alikuwa na nguvu zaidi yao, akawawahi na kwenda kuingia msalani.
Alipofanikiwa kuingia msalani, wala hakuchelewa kwa kuwa alikuwa amevaa khanga, aliweza kujiachia na kuanza kumwaga haja ndogo kama kuachia bomba la maji huku akisema maneno ya kuwananga wenzake aliokuwa amewashinda.
Kujiachia kwake bomba la maji litiririke bila ya mpangilio, Eddy akajua kuwa huyo binti hakuwa amepata mafunzo ya kutosha.
Eddy alikumbuka siku moja aliwahi kuambiwa na jimama moja kwamba anayekwenda haja ndogo kwa staha ni yule anayejua kujibana na kujiachia taratibu bila ya kusikika sauti kama vile mbwa au ngombe.
Hata hivyo, Eddy alikuwa amempenda msichana huyo, ingawaje moyo wake ulikuwa pia umedondokea kwa Rehema. Akawa anasisimka kwa jinsi alivyokuwa akiiachia bomba lake kwa fujo.
Daaa! Huyu naye sijui ni mtoto wa mwenye nyumba? alijiuliza.
Hadi alipokuwa akitoka, Eddy aliendelea kumwangalia kupita upenyo, badala ya huyo wakaendelea wasichana wengine waliokuwa wakigombea naye kuingia msalani.
Baada ya hapo, wakafuatia wengine wengi ambao kwa jumla yao wangeweza hata kufikia timu ya mpira wa miguu.
Eddy alishangaa wote hao walikuwa wakiishi vipi katika nyumba hiyo, kama vile haitoshi akajiuliza mbona jana yake wakati alipokuwa akifika, hakuwaona.
Majangaaa, jamani mbona Majangaaa!, alisema Eddy kimoyomoyo wakati alipotoka nje na kukutana na wasichana hao kibao wakiwa wamejipanga uwani kwa ajili ya kwenda kuoga.
Samahani kaka naomba sabuni
alisema yule msichana wa kwanza aliyewawahi wenzake kwenda msalani akimwambia Eddy.
Bila wasiwasi, Eddy alisema na kumkabidhi binti huyo sabuni yake ya kuogea.
Daa! Unaanza kujipendekeza kwa mgeni, alisema msichana mwingine na kuwafanya wengine nao waongeze maneno yao kedekede ambayo hata hivyo binti yule hakuyajali.
Itaendelea Alkhamisi ijayo..............