Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 330
- 1,244
MAISHA YA MSTAHAFU 😎
Hivi ndivyo anavyoishi mtu aliyeshinda kila kitu kwenye soka la dunia hii.
Alimpa mama yake kila alichoweza, pesa, furaha na hata umaarufu. Aliifurahia kazi yake ya soka kutoka mwanzo hadi mwisho. Alifanya makosa, lakini yalibaki kuwa sehemu ya safari yake.
Alinyakua Kombe la Dunia mwaka 2002, UEFA Champions League mwaka 2006, na Ballon d’Or mwaka 2005. Pia alishinda Copa América, Kombe la Mabara, na mataji ya ligi Hispania na Brazil.
Baada ya kustaafu, alikamatwa Paraguay mwaka 2020 kwa sakata la pasi, akapewa dhamana, na hatimaye kuondolewa mashitaka yote.
Sasa anaishi kwa amani, akisafiri, kuhudhuria matamasha, na kufurahia maisha bila presha. Dunia ya soka haitasahau tabasamu na uchawi wake alipokuwa uwanjani.
Jina lake ni Ronaldinho Gaúcho.